TRA customs Dar es Salaam ni uozo mtupu; ivunjwe

TRA customs Dar es Salaam ni uozo mtupu; ivunjwe

Mkombozi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2008
Posts
844
Reaction score
476
Kwanza naomba nitangulize shukrani zangu za dhati kwa watakaochangia kwa hoja za nguvu. Ni dhahiri kwa njia moja ama nyingine hamna ambaye haathiriki na operations/kazi za TRA Customs. Vitu vingi vinavyotoka nje lazima vipitie mchakato wa clearing ambayo hufanyika Customs pale LONG ROOM (DSM), TANGA, MTWARA.

Kwa serikali makini sana, ni dhahiri kua mapato mengi yatapatika Customs, sijui Tanzania ikoje hii. Ila Customs ya Dar es Salaam yaani Long Room ni uozo mtupu. Watu wanateseka sana na utendaji wa wafanyakazi wa TRA Customs, mimi ni mwathirika mmojawao.

Wameanzisha utaratibu wa HELP DESK, unakuta watu wanaowaweka pale wanajibu kila kitu wakati hawafahamu chochote, kuingia ndani hauruhusiwi kabisa. Kibaya zaidi unapeleka documents za kufanyiwa kazi zinachukua wiki zaidi ya Tatu, meli iko bandarini, mizigo imekaa inaendelea kuchargiwa storage fees. Kuenda upande wa exemption ndio kabisaa utakuta wafanyakazi wanakunywa chai, wanapiga stori, mara ametoka, mara ameenda kusali, unaandika barua inachukua wiki Tatu kujibiwa. Imenisikitisha sana. Hapo hapo serikali inalalamika mapato.

Ninawaomba TRA customs officers wajirekebishe, sisi ni walipa kodi, wengine wanalipa kodi kubwa sana halafu wanatunyanyasa. HEP DESKI halina msaada wowote kwa mlipa kodi, wafanyakazi wa CUSTOMS DSM hawafanyi kazi inavyotakiwa. Ikiwezekana wafukunzwe Customs iundwe upya.

Najua mpo wengi mmekutana na uozo mwingine, mfano unaleta mzigo una documents zote, mpaka supplier amesema ndio bei niliyomuuzia, wanakwambia sio bei yake, wanaongeza ili tu ulipie kodo zaidi.
 
Sasa unashukuru watakao changia hoja za nguvu ili iweje? Hoja ni hoja
Kama mie umenikatisha tamaa kuendelea kusoma niliposoma mwanzo

Haya sina hoja ya nguvu bali nina hoja za insiders
 
Back
Top Bottom