Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Habari za Jumapili!
Leo napenda kuwahusia TRA Dodoma na Tanzania nzima kwa ujumla!
Naomba msikae ofisini, chukueni mda wenu kutembelea maeneo ya biashara iwe Kwa kusema au kwa kutosema, ili muone na kufanya ufuatiliaji juu ya matumizi ya mashine za Efd.
Nimekuwa Dodoma tena kwa wiki nzima na kusema kweli nimeshuhudia maeneo mengi ya Dodoma ikiwemo maeneo ya mjini, Kwa waziri mkuu, sabasaba na hata kisasa maduka mengi sana yanafanya biashara sana lakini hawatoi risiti za efd. Hili limeniumiza sana kwa kweli.
Najua Mama Samia amewaambia msibambike watu kodi Ila hajawaambia sasa mlale na muache kufuatilia suala la ulipaji kodi hapa Tanzania.
Nimekuwa na Safari nyingi za Dodoma hivi karibuni na kusema kweli sijapenda hali niliyoiona hasa kwa wafanyabiashara kutotoa risiti na wengine ukiwadai wanakuonesha mashine za efd sikuwa zimejaa vumbi kiashiria kuwa hata hazitumiki.
Naomba katika kuhakikisha nchi yetu inafanya vizuri kiuchumi, muwe serious kwenye suala la kukusanya kodi, msilegee hata siku moja kwenye
1. Kuelimisha watu juu ya kukusanya kodi kupitia matangazo ya Tv na Radio
2. Kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa mara kwa Mara mitaani juu ya matumizi ya mashine zenu za kodi ( efd machine)
3. Naomba kama mnaona hamna nguvu kazi ya kutosha, basi amueni kushirikiana na serikali za kata/ mitaa katika kufuatilia na kukagua matumizi ya efd machines.
Tanzania ni yetu sote na lazima wote tuhakikishe kila mtu anatimiza wajibu wake ili tupate maendeleo ya kweli.