TRA fuatilieni hii kampuni ya wachina inayoitwa Hiview International Co Ltd, wanakwepa kodi sana

Walikuandikiaje risit ya kihuni hvi nawewe ukakubali kujuchukua hata invoice hakuna, risit haina muuri official brother uliyataka mwenyewe katika hlo
 
hajawahi kuwepo kabisa na ukileta mambo ya professionalism kwenye biashara za Tanzania utapotea mapema sana kwenye scene, do what you do to survive, siri ya biashara za bongo unapaswa kumjua mtu anayemjua mtu, information is akey
Kwa tafsiri rahisi inaitwa “CONNECTION”
bila matumizi ya huu mkakati biashara lazma ikushinde mapema sana!

Na katika huo mfumo lazma kutoa elfu 10/20/30 ni kawaida sana! Usiwe mkono wa birika tu😅
 
Pole sana kuna sehemu ulizembea waka take advantage
 
Wameanza kukupiga kwenye receipt.. Huoni receipt yenyewe wamekupa fake.. ingetakiwa wakupe EFD receipt. Hiyo ya kampuni yao ni kwa ajili ya record zao tu.
 
Kuna matatizo mengine wafanya biashara tunayatafutaga wenyewe, awa jamaa nimefanya nao biashara muda sasa na wakati wote wananipa TRA receipt na delivery note zikiwa proper. Labda ulitaka kuuziwa bila VAT matokeo yake ndo ayo. Kuna wakati unaweza pokea simu toka kwa mteja akiwa Mwanza au Geita, ukimpa bei anakwambia iyo bei ndo tunauziwa huku, unajiuliza inakuwaje wanapata kwa bei kama ya hapa Dar na apo umeweka margin ya 5000 tu kusudi usukume mzigo, kumbe wanauziwa na watu wale wa nataka mzigo usio na risiti. Kama ulifanya kila kitu kwa usahihi basi nenda polisi then wachina wataonesha kwenye report yao ya Z-report ya siku kama walikuuzia au lah!
 
Mchina anakunyonya anakuachia manyoya

Biashara na mchina anataka apate yeye tu

Ova

Janja janja nyingi ndio maana hata wafanyabiashara wanaofuata mzigo ulaya au hata uarabuni wanapata pesa iliyonyooka mapema kuliko wanaojichosha kwenda china
 
Tatizo kampuni ishakuwa wanaona wateja wapya ni takataka tu
Kampuni bado changa sana,wanaimport kontena 5 tu kwa mwezi,wenzao wakina artan,Binex au Nas wanaingiza kontena karibu 80 kwa mwezi . sijajua kwa nin wana hizi tuhuma.
 
Kampuni bado changa sana,wanaimport kontena 5 tu kwa mwezi,wenzao wakina artan,Binex au Nas wanaingiza kontena karibu 80 kwa mwezi . sijajua kwa nin wana hizi tuhuma.
Wanaanza kulewa sifa
 
Ulikuwa unataka mtelemko ukapata mserereko
Alitoka Dar hadi Mwanza halafu mwanza arudi Dar ,wakati Dar ndio kuna kila kitu,huyu ni muongo hizi ndio dili zake na si ajabu anajua sana kuwa huko Mwanza Waxhina wanakwepa ushuru na hawatoi risiti ila mzigo unauziwa bei poa isiyo ya risti za EFD sasa leo kakamatwa anaanza kuimba wakati anajua fika hiyo biashara na nina wasiwasi kuwa jamaa huu ndio mchezo wake ila safari hii kashtukiwa.
 
Haha ngoja niwasalimie kwa jina la jamhuri,siku hizi ni kama hakuna mwenyewe si ajabu wamekimbilia kwenye tozo huku kwingine wameachia mianya sasa hao ni watu wa vikampuni vya mfukoni sijui hali ikoje kwa wafanyabiashara wenye maamuzi,sijui wale waliobadili majina ya kampuni na kuwa wafadhili wa timu ya mpira ya nyikani sasa si ndio wanaogelea wakiongozwa Chalinze one
 
Sijapewa mkuu.jamaa mwanzo walikua wanataka 4m vinginevyo wanataifisha mzigo.ndio tukashushana hadi 1.5.
Pole sana.

Hapa Transporter na hao wa kujiita TRA lao moja Mkuu. Kiufupi walikuchezea mchezo amazing. Hata Mchina ukimlalamikia ni ngumu kukuelewa, kwamba umepigwa fine na TRA afu huna kielelezo chochote? Ataku refund vipi?
 
Taarifa hii haina ukweli, taarifa za kuchafua kampuni au wafanyakazi kwa makusudi binafsi si tabia nzuri na inaleta mijadala isiyo na afya. maana hakuna mteja wa Mwanza aliyehudumiwa siku hiyo na kupewa receipt inayoonekana kufojiwa sahihi ya mfanyakazi wa Kampuni ya Hiview, kughushi sahihi ya mtu ni kosa kisheria, anaefanya hivi anakosea, hakuna malipo yaliyopokelewa kwa utaratibu ambao ofisi inautumia.

Kitabu cha risiti kilichoambatanishwa sahihi yake imeghushiwa na si risiti ya kuuzia bidhaa, ni risiti inayothibitisha kua kiasi flani cha fedha kimepokelewa toka kwa mteja sokoni hasa kwa wateja wanaokopeshwa bidhaa ambao wakati waliponunua walipatiwa invoice na efd yake.

Kampuni inamifumo madhubuti ya kufanya biashara na inasaidia sana wateja wake kuweka mifumo ya biashara na ushauri wa compliancies, angekuwa ni mteja halali wa Hiview International Co Ltd asingetoa tuhuma mitandaoni angefuata taratibu zinazofahamika.

Kitabu kilichokuwa kinatumika chenye mfululizo wa namba hizo kilishafungwa matumizi yake kutokana na mfanyakazi alokua anakitumia kuachishwa kazi kwa sababu mbalimbali.

Nia ya thread hii ni visasi ambavyo kimsingi vinalengo binafsi. Ni vizuri kila mtu kuepuka uzushi mtandaoni ili kulinda afya ya hii forum, kuepuka kujiingiza katika jinai bila sababu, kuepuka kudharirisha watu kwa makusudi na nia ovu dhidi ya Kampuni. Hizi tuhuma zina lengo la kuifanya Hiview isiendelee na mikakati ya kiushindani sokoni.

Haya ni matokeo ya watu walofanya ouvu kwenye kampuni na kujihami wasichukuliwe hatua.
 
BIASHARA NYINGI NA WACHINA NI RISK KUBWA.

SASA JARIBU KUJA KUNUNU MABATIBOMBA, NDANI YA MIAKA MIWILI JIPANGE KUJA KUBADIRISHA.
 
Nyie wababaishaji sana.
Matairi yenu ni feki,nimenunua matairi yamekaa siku mbili tu yakabasti yote.
Me nashauri sio TRA tu wawashughulike,hata TBS nao wawashughulikie.
Halafu hamna customer care nzuri kabisa,kuanzia huyo meneja wenu mpaka wafanyakazi wa chini.wote zero brain.





 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…