TRA hamjawatendea haki INTERNS wenu

TRA hamjawatendea haki INTERNS wenu

Huu Uzi bado upo ,Mungu ajalie vijana tupate maarifa ya kujishuhulisha na tupate kaz
 
Mkataba ukiisha hupaswi kuonekana eneo la kazi. Ni amri kutii sheria bila shuruti.

Vijana walipewa mkataba wa miaka miwili na kila mwezi walilipwa laki nne na nusu (450,000) per month. Kwa miaka miwili hiyo ni sawa na milioni kumi na laki nane. 10,800,000.

Muulize kijana pesa zote hizo kapeleka wapi? Ilipaswa wakimbizwe kabisa. Tatizo la wabongo hawana shukrani.
una uelewa mdogoo sana yanii... kwa hiyo mtu akilipwa laki 4 na nusu kwa mwezi unaona ni hela ya maana sababu miaka miwili itakuwa ni mil 10 😀 😀 😀 ukiajiriwa utaelewa labda kama ni mwanamke unatumia hela za mumeo
 
Jana wakati natoka kazini, nilipata wasaa wa kupitia maeneo yangu ya kujidai TABATA. Kwa bahati nilikutana na kijana mmoja ambaye nilimfahamu kupitia kazi zetu hizi.

Kwa bahati mbaya sana alinijulisha kuwa wamesitishiwa mikataba yao, mbaya zaidi ni kwamba wameambiwa mwisho ni IJUMAA yaani jana na ifikapo J3 hawaruhusiwi kuingia kazini.

Sikuona tatizo kwa vijana wale kumaliza mkataba ila njia iliyotumia kuwapa ujumbe haikuwa sawa, na hasa ukizingatia wangeweza kupewa Barua inayaonesha kuwa kuwa Tar fulani itakuwa mwisho wao.

Inafahamika wazi wale vijana haikuwa ajira lakini kwanini msikae nao na kuwaeleza kwa usahihi? Kwanini muwape stress za ghafla kiasi hiko.

Mamlaka ya Mapato ni taasisi kubwa mno, hivyo utoaji wa taarifa lazima uzingatie pia haki za hao watu.

Mwisho naomba mkae nao muwape hata darasa la namna ya kuishi bila zile kazi, maana nimeona hapa kijana ameshindwa hadi kula chakula.

Nawasilisha.
unajua kuna vitu siyo mpaka uambiwe au ufundishwe. nadhani hawa vijana ni wasomi na wamebahatika kufanya kazi ya mpito hapo TRA ni fursa iliyokuwa nzuri mno kuzidi kapat elimu kwa vitendo. Kumbuka kuna vijana wengi hawana ajira na hawakubahatika hata kuapata nafasi ya ajira za mpito. Sasa tra navyojua mimi kazi yake ni kukusanya makokotoo leo tena ianze kazi za kufundisha namna ya kukaa kitaa bila kazi? mbona vijana mnaniangusha ? kuna wenzenu hata shule hawajaenda ila wamepambana na Mungu kawasimamia na wamefaniiwa . umepewa mkataba wa mwaka ulishindwa nini jipanga kiakili na hata kuweza fanya saving angalau kidogo. tena ilikuwa ni nafasi nzuri kujifunza hata kodi wanatozaje . Mgeweza hata kuanzisha kusaidia watu kurejista TIN na kujipatia kipato ila inaonekana kujiongeza hawezi anakuja lalamikia huku.
 
Back
Top Bottom