Tangu Uhuru Pombe huwa haipunguziwi kodi.
Tulitegemea kodi ipunguzwe kwenye Mafuta ya Chakula, Mafuta ya Petrol na umeme.
Kupunguza kodi kwenye bidhaa za starehe ni jambo lisilowanufaisha wananchi wa chini walio wengi.
Hata hivyo nchi hii ina maskini wengi sana hivyo kutegemea kodi bila serikali kuja na mipango mikubwa ya kitaasisi ni kuwaumiza wananchi huku watawala wakiendelea kuwa na maisha ya juu zaidi.
Sikuona kodi zikiongezwa kwenye mishahara mikubwa.
Nilitegemea wale wenye mishahara zaidi ya mil. 4 wakiongezewa kodi kufikia 15 % na wale wenye mishahara chini ya mil. Wakipunguziwa kufikia 5% ili waweze kuendana na ugumu wa maisha na mfumuko wa bei.
Eti kodi ya majengo.
Mtu amejinyima kwa miaka kujenga kanyumba kake halafu anakwapuliwa kodi wakati kila kifaa alichojengea kililipiwa kodi. Hii ni dhulma kubwa sana. Viwanja vyenyewe havikupimwa wala ahavipimwi bure.
Tujiulize tangu Uhuru NHC wamejenga nyumba ngapi kwa ajili ya wananchi wa kawaida ?
Limekua ni shirika la kusimamia na kutafuna kodi za nyumba zilizoachwa na mkoloni na zile chache za mwalimu Nyerere. Hivi leo hii kila Halimashauri ingekua na nyumba mia tano mpaka elfu moja za NHC na kuwapangishia watu wa kada mbali mbali ,serikali ingekusanya mabilioni ya pesa kila mwezi na kuzidi kujenga majumba na makazi bora kwa watanzania wote huku watu wakiwa na uwezo wa kuendesha maisha yao.
Ni nchi gani iliyoweza kuendeleza watu wake bila kuwa na mpango bora wa makazi kwa watu wake.
Shirika la nyumba lipo kama kichaka cha watu kujificha na kula pesa za umma. Hatuoni majengo mapya ya kuwapangishia watu wengi wanaohitaji nyumba bora za kupanga.
Jiji jipya la Dodoma tulitegemea pasiwe na vibali holela vya watu kujenga vibanda binafsi na kupoteza ardhi kubwa kwa makazi duni badala ya kujenga nyumba bora zinazomilikiwa na NHC ili Serikali ipate mapato na wananchi wanaohamia Dodoma wasiwe wananyonywa kwa kuongezewa kodi kiholela kwenye makazi duni uswahilini.
Miaka ijayo tutakua na taifa la mabwana na watwana.
Mabwana ndio wale walojiuzia nyumba zote za serikali badala ya kujenga nyumba bora kwa watu wake wote ili wapangishe kwa bei nafuu.
Tunakamua watu kodi halafu tunalazimidha vijana kwenda JKT kupoteza fedha za umma kwa kulala kwenye matope badala ya kuwapeleka kule Mpanda ,Lindi, Tanga,Morogoro, Manyara, Ruvuma, n.k na kuanzisha mashamba makubwa kama yale yaliyoanzishwa na serikali bunifu ya Mkoloni na mpaka Leo miaka mia na hamsini bado yanatumiwa na vizazi vyetu kupata ajira na pato la ndani na nje.
Hivi kutumia mabilioni ya pesa kurusha vijana kichura inasaidia nini wakati hakuna ajira na mapori yamejaa tele tatizo ni mitaji na zana za kilimo kama matrekta na magreda ya kusawazisha mapori na kuwachimbia visima virefu na mofereji kisha wanaachiwa wataalam toka Sua badala ya walimu wa JKT kurusha vijana kichura na kuwafanya wawe wazalendo feki wasio na ajira wenye roho za kihalifu kama akina Sabaya.
Nchi yenye ardhi kubwa kama hii na Jeshi la kujenga Taifa na la uchumi kutegemea kodi ya nyumba za watu maskini wa kule manzese ,magomeni ,Mbagala, vijijini na line za simu ni laana kubwa sana tunaitafuta toka kwa Mungu.
Matokeo yake wakubwa wanashindana kujimilikisha ardhi kwa sababu wana fedha nyingi zisizo na kazi. Ndio maana hawawazi namna bora ya kuitumia ardhi kubwa tuliyo nayo kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha kuzalisha Chakula Afrika Mashariki na kati na kuuza mpaka Asia na Uarabuni.
Badilikeni watendaji wa Serikali na wabunge wa CCM msiwaze kodi kwa watu wale wale tu. Kila kitu kitapanda bei kwa kupandisha kodi ya mawasiliano ,umeme na Petroli anayeumia ni mwananchi wa chini.
Tunakwama wapi wateule wa Serikali wanawaza kodi tu tena wanapanga mipango ya nchi wakiwa wamelewa ndio maana wanapunguza kodi kwenye pombe na sigara.
Kwa nini tusitafute soko la mazao kama Bangi na Mirungi nje ya nchi na Iwe ni marufuku kuuza ndani lakini Iwe ni halali kuuza nje kwa mabeberu wanaohitaji ili kukuza uchumi wetu?
Kodi ipo tangu enzi za mitume kwa ajili ya mabeberu wanaotawala ili waishi maisha mazuri kwa migongo ya wanyonge.