TRA: Hatua ya kuzuia akaunti ya mlipakodi ni ya mwisho kabisa ambayo hufanyika baada ya mlipakodi kutotimiza matakwa ya sheria ya kulipa kodi

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
TRA: MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWAKUMBUSHA WALIPAKODI
KUTEKELEZA WAJIBU WA KULIPA KODI KWA MUJIBU WA SHERIA

Dar es Salaam, 18 Mei, 2024:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inapenda kuwakumbusha walipakodi kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kulipa kodi kwa hiari na wakati, ili kuepuka usumbufu na migogoro isiyo ya lazima.

Ifahamike kwamba, TRA hutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ambayo ni kukadiria, kukusanya na kuhasibu mapato yote ya serikali, kusimamia kwa makini na ufanisi sheria zote za kodi,
kuishauri Serikali kuhusu sera za mapato ya Taifa, kudhibiti udanganyifu na ukwepaji kodi na kuinua kiwango cha uwajibikaji wa kulipa kodi kwa hiari. Majukumu yote haya hutekelezwa kwa kuzingatia misingi ya Weledi, Uwajibikaji na Uadilifu.

Mamlaka ya Mapato Tanzania hutumia njia mbalimbali za kisheria ili kukusanya mapato na madeni ya
kodi zikiwemo kuwakumbusha na kuwaita wote wenye madeni ya kodi kukaa nao mezani kwa ajili ya
kujadili namna ya kulipa kodi zao. Njia hii, huishia kwa kuingia mikataba ya kulipa madeni hayo kwa awamu.

Hatua ya kuzuia akaunti ya mlipakodi ni ya mwisho kabisa ambayo hufanyika baada ya mlipakodi kutotimiza matakwa ya sheria ya kulipa kodi, kuvunja mkataba wa makubaliano aliyoingia na TRA ya kulipa kodi kwa awamu au kukaidi wito wa kufika ofisini. Hatua zinazochukuliwa kabla ya kuzuia akaunti ya mlipakodi ni pamoja na: -

1. Ni kumuandikia mlipakodi Hati ya Madai (Demand Notice) ambapo mlipakodi hupewa muda
wa kutosha wa kulipa deni lake la kodi au kufika katika ofisi inayomhudumia kwa ajili ya
majadiliano ya namna ya kulipa kodi husika.

2. Mlipakodi asipotekeleza hatua ya kwanza, hatua ya pili hufuata ambayo ni kumuandikia
barua ya kumkumbusha kutimiza wajibu wake wa kulipa kodi na kumtaka alipe kodi anayodaiwa au afike ofisini kwa majadiliano.

3. Mlipakodi asipotekeleza hatua zote tajawa hapo juu, Kifungu cha 67 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Tax Administration Act) inampa mamlaka Kamishna wa TRA kutoa hati ya uwakala wa ulipaji kodi (Agency Notice) ambayo hupelekwa kwa mtu au taasisi inayomiliki fedha au mali za mlipakodi ambayo hutumika kama wakala wa mlipakodi na kutakiwa kulipa deni hilo la kodi kwa niaba yake. Kwa taarifa hii, TRA inawasihi walipakodi wote kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari na wakati, wale wenye changamoto za madeni ya kodi kufika katika ofisi za TRA zinazowahudumia kwa lengo la kujadili namna ya kutatua changamoto hizo.

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"
Imetolewa na;

IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO
Task_aa87b44df5e8f640.jpg
 
Viongozi wengi wa TRA wilyani na mikoani wamekuwa wakitumia kama fimbo kukusanya kodi kwa nguvu.

Hiko kifungu kinampa mamlaka kamishna. Lkn unakuta afisa tu anakitumia.

Nadhani mamla ya hiyo kifungu ibakie kwa kamishna yeye mwenyewe, uone kama watafanya huu uhuni kwa wafanya biashara.
 
TRA: MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWAKUMBUSHA WALIPAKODI
KUTEKELEZA WAJIBU WA KULIPA KODI KWA MUJIBU WA SHERIA

Dar es Salaam, 18 Mei, 2024:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inapenda kuwakumbusha walipakodi kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kulipa kodi kwa hiari na wakati, ili kuepuka usumbufu na migogoro isiyo ya lazima.

Ifahamike kwamba, TRA hutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ambayo ni kukadiria, kukusanya na kuhasibu mapato yote ya serikali, kusimamia kwa makini na ufanisi sheria zote za kodi,
kuishauri Serikali kuhusu sera za mapato ya Taifa, kudhibiti udanganyifu na ukwepaji kodi na kuinua kiwango cha uwajibikaji wa kulipa kodi kwa hiari. Majukumu yote haya hutekelezwa kwa kuzingatia misingi ya Weledi, Uwajibikaji na Uadilifu.

Mamlaka ya Mapato Tanzania hutumia njia mbalimbali za kisheria ili kukusanya mapato na madeni ya
kodi zikiwemo kuwakumbusha na kuwaita wote wenye madeni ya kodi kukaa nao mezani kwa ajili ya
kujadili namna ya kulipa kodi zao. Njia hii, huishia kwa kuingia mikataba ya kulipa madeni hayo kwa awamu.

Hatua ya kuzuia akaunti ya mlipakodi ni ya mwisho kabisa ambayo hufanyika baada ya mlipakodi kutotimiza matakwa ya sheria ya kulipa kodi, kuvunja mkataba wa makubaliano aliyoingia na TRA ya kulipa kodi kwa awamu au kukaidi wito wa kufika ofisini. Hatua zinazochukuliwa kabla ya kuzuia akaunti ya mlipakodi ni pamoja na: -

1. Ni kumuandikia mlipakodi Hati ya Madai (Demand Notice) ambapo mlipakodi hupewa muda
wa kutosha wa kulipa deni lake la kodi au kufika katika ofisi inayomhudumia kwa ajili ya
majadiliano ya namna ya kulipa kodi husika.

2. Mlipakodi asipotekeleza hatua ya kwanza, hatua ya pili hufuata ambayo ni kumuandikia
barua ya kumkumbusha kutimiza wajibu wake wa kulipa kodi na kumtaka alipe kodi anayodaiwa au afike ofisini kwa majadiliano.

3. Mlipakodi asipotekeleza hatua zote tajawa hapo juu, Kifungu cha 67 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Tax Administration Act) inampa mamlaka Kamishna wa TRA kutoa hati ya uwakala wa ulipaji kodi (Agency Notice) ambayo hupelekwa kwa mtu au taasisi inayomiliki fedha au mali za mlipakodi ambayo hutumika kama wakala wa mlipakodi na kutakiwa kulipa deni hilo la kodi kwa niaba yake. Kwa taarifa hii, TRA inawasihi walipakodi wote kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari na wakati, wale wenye changamoto za madeni ya kodi kufika katika ofisi za TRA zinazowahudumia kwa lengo la kujadili namna ya kutatua changamoto hizo.

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"
Imetolewa na;

IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO
View attachment 3027684
Asante sana kwa taarifa hii na hiki hasa ndicho nachokifahamu sheria inavyosema sasa wenzangu nadhani tumepata picha hapa kuwa kumbe kuna taratibu za kufata.Ndiyo kusema kumbe kuna muda ambao ikishindiakana hapo sawa maana wengi walikuwa wanasema kwamba wanakuja na kufunga tu.Hii ni taarifa muhimu kushare na wadau wengine
 
17 October 2024

KAMISHNA MKUU WA TRA ATOA UFAFANUZI WA KINA, ALIPOKUTANA NA WAKUU WA MABENKI TANZANIA

View: https://m.youtube.com/watch?v=J1sxDYQI3Xk
Ambapo kamishna mkuu TRA aelezea jinsi mabenki yatakavyotumiwa kukusanya kodi kutoka akaunti za mteja ni hatua zipi na ni nani mwenye mamlaka ya mwisho kuiambia benki kuhusu kukusanya kodi kutoka akaunti ya benj8 ya mtaja
 
Back
Top Bottom