Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Baada ya taarifa za kupotea kwa Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi ambaye hakurudi nyumbani kwake toka alipoingia kazini December 11, 2024 Jijini Dar es salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haihusiki na swala la kupotea kwa Mfanyabiashara huyo.
Taarifa hii ya TRA inakuja baada ya Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kuandika kuwa Ulomi amesema aliondoka Sinza kwenda Mbagala Bandari kavu kukagua kontena lake baada ya kuitwa na Watu wa TRA kwa ajili ya ukaguzi.
Taarifa ya TRA imeeleza yafuatayo "Ni Wakala wa Forodha peke yake ndiye anayewajibika kusimamia taratibu zote za kiforodha za uondoshaji wa mizigo Bandarini kwa niaba ya Muagizaji Mzigo na sio Muagizaji wa mzigo"
"Kwa mujibu wa kumbukumbu zetu, Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi alichagua Kampuni ya Wakala wa forodha ya TWENDE FREIGHT FORWARDERS LIMITED kupitia barua yake kwa TRA December 5 2024 kuwajibika kuondosha mizigo yake Bandarini kulingana na taratibu za forodha, kwa misingi hiyo TRA imekuwa ikifanya kazi na Wakala wake ambaye bado hajakamilisha taratibu za kiforodha kuondosha mizigo husika"
"TRA haijawahi kumuita wala kufanya naye kazi Mfanyabiashara huyo katika Ofisi zake kwa jambo lolote, suala la kutoonekana kwa Mfanyabiashara huyo ni jambo la Kipolisi ambalo TRA haihusiki nalo" - imeeleza taarifa ya TRA.
Pia, Soma:
• Mfanyabiashara Ulomi apotea, familia na Polis wanamtafuta
• Polisi waanza kumtafuta Ulomi anayedaiwa kupotea