TRA: Hatuhusiki na kupotea kwa mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi

CHADEMA imekosa hoja kabisa. Yaani TRA imteke mtu ili nini? Huyu Boni si ndo alisema Lissu anafanya uhaini kwa kuutaka uenyekiti?
Watekaji pia huvaa koti la TRA...ndio kisa na maana wakalambwa mawe palee Tegetani
 
Kwa sasa ukikutana na TRA...piga mawe tu kuba baba zao
 
Ukikubali kubebwa na watu wanajitambulisha kuwa ni mamlaka yoyote ya serikali basi unakubali kifo. Pambana, bora ufie hapohapo ijulikane!
 
Aisee inasikitisha sana yaani mtu anatoka mzima kutoka kwenye familia yake harafu baadae anarudi maiti pana watu hawauawi namna hiyo mtakuja kusema hapa baadae..
 
Baada ya taarifa za kupotea kwa Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi ambaye hakurudi nyumbani kwake toka alipoingia kazini December 11, 2024 Jijini Dar es salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haihusiki na swala la kupotea kwa Mfanyabiashara huyo.
View attachment 3177009
Taarifa hii ya TRA inakuja baada ya Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kuandika kuwa Ulomi amesema aliondoka Sinza kwenda Mbagala Bandari kavu kukagua kontena lake baada ya kuitwa na Watu wa TRA kwa ajili ya ukaguzi.

Taarifa ya TRA imeeleza yafuatayo "Ni Wakala wa Forodha peke yake ndiye anayewajibika kusimamia taratibu zote za kiforodha za uondoshaji wa mizigo Bandarini kwa niaba ya Muagizaji Mzigo na sio Muagizaji wa mzigo"

"Kwa mujibu wa kumbukumbu zetu, Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi alichagua Kampuni ya Wakala wa forodha ya TWENDE FREIGHT FORWARDERS LIMITED kupitia barua yake kwa TRA December 5 2024 kuwajibika kuondosha mizigo yake Bandarini kulingana na taratibu za forodha, kwa misingi hiyo TRA imekuwa ikifanya kazi na Wakala wake ambaye bado hajakamilisha taratibu za kiforodha kuondosha mizigo husika"

"TRA haijawahi kumuita wala kufanya naye kazi Mfanyabiashara huyo katika Ofisi zake kwa jambo lolote, suala la kutoonekana kwa Mfanyabiashara huyo ni jambo la Kipolisi ambalo TRA haihusiki nalo" - imeeleza taarifa ya TRA.View attachment 3177008

Pia, Soma:

Mfanyabiashara Ulomi apotea, familia na Polis wanamtafuta

Polisi waanza kumtafuta Ulomi anayedaiwa kupotea
TRA Tanzania ndio mkome kujidai mapolisi, kukimbiza magari ya watu usiku wa manane
 
Ni hatari sana kuihusisha TRA na haya masuala ya utekaji.
Mbona hao hao TRA walikiri kuhusika kwenye sakata la kakamata (a.k.a utekaji) wa mtu na gari yake Tegeta, tena usiku?!

Ukute wale wawakilishi wa TRA wangefanikiwa kumkamata yule jamaa angeshakata moto
 
  • Masikitiko
Reactions: Tsh
Nchi imekuwa na watu wenye roho za kuzimu wamejaa ushetani sana
 
Juzi walijinasibu kama wana mamlaka na hawahitaji order ya mahakama leo wanadai hawahusiki wao wana deal na wakala tu sio muagiza mzigo/Gari why Ile X6 walimfuata owner na sio wakala
Tena walienda kumkamata usiku!!!
 
Baada ya taarifa za kupotea kwa Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi ambaye hakurudi nyumbani kwake toka alipoingia kazini December 11, 2024 Jijini Dar es salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haihusiki na swala la kupotea kwa Mfanyabiashara huyo.
View attachment 3177009
Taarifa hii ya TRA inakuja baada ya Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kuandika kuwa Ulomi amesema aliondoka Sinza kwenda Mbagala Bandari kavu kukagua kontena lake baada ya kuitwa na Watu wa TRA kwa ajili ya ukaguzi.

Taarifa ya TRA imeeleza yafuatayo "Ni Wakala wa Forodha peke yake ndiye anayewajibika kusimamia taratibu zote za kiforodha za uondoshaji wa mizigo Bandarini kwa niaba ya Muagizaji Mzigo na sio Muagizaji wa mzigo"

"Kwa mujibu wa kumbukumbu zetu, Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi alichagua Kampuni ya Wakala wa forodha ya TWENDE FREIGHT FORWARDERS LIMITED kupitia barua yake kwa TRA December 5 2024 kuwajibika kuondosha mizigo yake Bandarini kulingana na taratibu za forodha, kwa misingi hiyo TRA imekuwa ikifanya kazi na Wakala wake ambaye bado hajakamilisha taratibu za kiforodha kuondosha mizigo husika"

"TRA haijawahi kumuita wala kufanya naye kazi Mfanyabiashara huyo katika Ofisi zake kwa jambo lolote, suala la kutoonekana kwa Mfanyabiashara huyo ni jambo la Kipolisi ambalo TRA haihusiki nalo" - imeeleza taarifa ya TRA.View attachment 3177008

Pia, Soma:

Mfanyabiashara Ulomi apotea, familia na Polis wanamtafuta

Polisi waanza kumtafuta Ulomi anayedaiwa kupotea
What a painful ending? 😭
IMG-20241216-WA0010.jpg
 
Mbona hao hao TRA walikiri kuhusika kwenye sakata la kakamata (a.k.a utekaji) wa mtu na gari yake Tegeta, tena usiku?!

Ukute wale wawakilishi wa TRA wangefanikiwa kumkamata yule jamaa angeshakata moto
Inasikitisha mkuu
 
Back
Top Bottom