TRA: Hatuhusiki na ukusanyaji wa Kodi kupitia LUKU

TRA: Hatuhusiki na ukusanyaji wa Kodi kupitia LUKU

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Screenshot_20240702-142910_1.jpg

"Suala la ukusanyaji wa kodi za jengo kwa kutumia mita za LUKU ulishahamishwa kutoka TRA kwenda kwenye halmashauri na manispaa na majiji, imerudishwa serikali za mitaa.

TRA haihusiki tena na ukusanyaji wa kodi kupitia hizo LUKU." - Paul Walalaze, Meneja Elimu kwa Mlipakodi TRA alipoulizwa na Swahili Times kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya ongezeko la makato kwenye kununua umeme

PIA SOMA
- Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya
 
Kupata ujasiri kama wa Gen Z kwa kizazi hiki cha Tz, Haiwezekani, wewe muda wote ni simba yanga, yaani kama vile ndio maisha yao ya kila siku
Gen Z imekuja baada ya FIFA kuifungia Kenya kushiriki soka kwa miaka 5. Kabla ya hapo nao walikuwa wanajadili Gor Mahia, Sofa Paka, n.k.

Kwa kuwa Simba imeingia mdudu, tuombe Yanga pia iingie mdudu ili ifike mahala watu wote waache kushabikia mpira.
 
Wala sio sababu, nimeishi kenya, hakuna wajinga kama hapa bnana!! Hilo hata jomo kenyata alimwambia Nyerere!! Wewe nchi gani masikini kwenye radio toka asubuhi hadi usiku ni vipindi vya michezo tu!!??
 
"Suala la ukusanyaji wa kodi za jengo kwa kutumia mita za LUKU ulishahamishwa kutoka TRA kwenda kwenye halmashauri na manispaa na majiji, imerudishwa serikali za mitaa.

TRA haihusiki tena na ukusanyaji wa kodi kupitia hizo LUKU." - Paul Walalaze, Meneja Elimu kwa Mlipakodi TRA alipoulizwa na Swahili Times kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya ongezeko la makato kwenye kununua umeme

PIA SOMA
- Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya
Mbona tume piga simu huduma kwa wateja Tanesco tukaambiwa mfumo wa kukata tozo uko TRA? Na kwamba malalamiko yaelekezwe huko TRA?
Hii nchi ni nani wa kuamini?
 
Kupata ujasiri kama wa Gen Z kwa kizazi hiki cha Tz, Haiwezekani, wewe muda wote ni simba yanga, yaani kama vile ndio maisha yao ya kila siku
Kwa taarifa tu Gen Z ni kizazi ambacho hakitabiriki.

Mfano , chunguza familia kadhaa za jirani yako au katika mishe mishe, utakuja kugundua ndiyo kizazi kinachotukana hadi wazazi wao ( hakina UTU).
 
Kwenye hili wale kunguni wa mama kuuchapa mwingi wamesalimika au nao wamekubali kuungana kuumia na wengine?

M
IMG-20240628-WA0014.jpg
aana sijaona bandiko la kunguni wakuu wa humu aidha kutoa PONGEZI/KUKOSOA kodi hiyo mpya.

Vipi mama ameupiga mwingi hapo au amepigwa mwingi?

Cc:Lucas Mbwa Wa Shamba

Bcc:The Sunk Cost Fallacy/Choice Variable
 
Kwa kifupi kodi ya jengo imekuwa shilingi 24,000/= kwa mwaka kutoka 12,000/=! Ni maelekezo toka kwa waziri wa fedha, ukiona vipi hamia marekani.
 
Hapa ni kujilaumu ni ujinga wetu wenyewe ukiongozwa na kile chama pendwa.

Chochote kinachotokea katika mwaka wa fedha mpya lazima kimo kwenye bajeti kuu ya serikali na kimepitishwa na wabunge. Ndio kusema hicho kipengele wali-skip na wabunge kupiga makofi?

Hebu kila mtu amuulize mbunge wake kama anajua ongezeko hilo?

Mwaka kesho tujitahidi wabunge wa upinzani wawe wengi bungeni kwa sababu wao angalau walikuwa wanapata muda wa kuchambua mambo mbalimbali kwa kina!

Ndio tujifunze kufuatilia mambo muhimu ya nchi badala ya Simba na Yanga. Uzwazwa wa wananchi wa Tanzania ni mtaji wa wanasiasa!
 
Dawa ya serikali hii ni Gen Z tu. Sasa kama haihusiki Tanesco wanakusanya kwa niaba ya nani?
Gen Z ya bongo kama mnawategemea imekula wa chuya,,,,watu wapo bize wanasaka mishangazi na madanga labda msubirie generation एफ
 
Kupata ujasiri kama wa Gen Z kwa kizazi hiki cha Tz, Haiwezekani, wewe muda wote ni simba yanga, yaani kama vile ndio maisha yao ya kila siku
Nikiangalia mazezeta ya Yanga Tangu jana hadi leo yanavyoshangilia kusajiliwa Chama ndiyo utaelewa kwa nini Jomo Kenyatta alimwambia Nyerere anatawala maiti. Ni vigumu sana vijana wa Kitanzania kufikia ufahamu na ujasiri wa Gen Z.
 
Back
Top Bottom