TRA: Hatuhusiki na ukusanyaji wa Kodi kupitia LUKU

TRA: Hatuhusiki na ukusanyaji wa Kodi kupitia LUKU

Kwa taarifa tu Gen Z ni kizazi ambacho hakitabiriki.

Mfano , chunguza familia kadhaa za jirani yako au katika mishe mishe, utakuja kugundua ndiyo kizazi kinachotukana hadi wazazi wao ( hakina UTU).
Hata kama ni hivyo lakini kwa wanachokifanya kenya kinaenda kuwasaidia wananchi wote kwa ujumla!! Kwani hoja zao mfano mbona maisha yanazidi kuwa magumu tu kwa wananchi wa chini wakati wanasiasa wanazidi kutajirika?!! Mafisadi yanatamba tu!! H
 
Waziri w pesa n CHURA kunakitu kati yao!!

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Hata kama ni hivyo lakini kwa wanachokifanya kenya kinaenda kuwasaidia wananchi wote kwa ujumla!! Kwani hoja zao mfano mbona maisha yanazidi kuwa magumu tu kwa wananchi wa chini wakati wanasiasa wanazidi kutajirika?!! Mafisadi yanatamba tu!! H
Ni kwel ndiyo wanasaidia.
Nia yangu ilikuwa ni kumuelewesha mtoa mada kwamba ni kizazi kisichotabirika kimaamuzi.

Mimi mwenyewe nakiona kama kizazi cha kuogopwa hasa kwa hao mafisadi (ndio maana nikamtolea mfano wa UTU katika jamii yetu).
Vizazi vilivyotangulia ni rahisi kuvipoza jazba kwa kumpa maneno ya kidini au kuwatia uoga lakini hichi kizazi kipya yajayo yanafurahisha.

Ni muda sasa wa viongozi wetu kurekebisha sera na kuwatazama hawa vijana.
 
Basi huko Halmashauri hizo fedha zinapigwa sana.
 
Tanesco ni Gateway tu ya kukusanyia mapato ,kama TRA hawakusanyi basi wanakusanya hao walinaokusanya mbadala wa TRA...Means tanesco badala ya kupeleka TRA basi now wanapeleka huko waliopelekeza ,hiyo kauli haiondoi makato ya kila mwezi bado yataendelea tu.
 
Kwahyo mpk sasa muhusika wa hayo makato ya 2000 hajulikani...mhh hii nchi inachosha sana...
 
Kwanza inakatwa kama Deni kwa hiyo hionekani clear kama kodi , pili hii kodi kwanini haikusanywi na TRA ?

Kwa anaejua

Screenshot_20240702-142910_1.jpg
 
Du hii serikali inatuibia sana sisi watanzania! hiyo tozo ya Luku ni wizi wa waziwazi kwa sababu ununuzi wa umeme mteja anakatwa VAT ambayo ndiyo kodi halali ya kwenda serikalini. Lakini wanapolazimisha hiyo kodi nyingine ya 2000 ni double taxation kwa mteja huyo huyo mmoja. Huu wizi haukubaliki hata kidogo, mwigulu na sa100 mwisho wao utakuwa mbaya sana ndani ya taifa hili.
 
"Suala la ukusanyaji wa kodi za jengo kwa kutumia mita za LUKU ulishahamishwa kutoka TRA kwenda kwenye halmashauri na manispaa na majiji, imerudishwa serikali za mitaa.

TRA haihusiki tena na ukusanyaji wa kodi kupitia hizo LUKU." - Paul Walalaze, Meneja Elimu kwa Mlipakodi TRA alipoulizwa na Swahili Times kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya ongezeko la makato kwenye kununua umeme

PIA SOMA
- Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

Hapa kuna manyagunyagu inabidi tupite kwa uangalifu mkubwa
 
Haya ni maajabu ya..........TRA, wakusanya kodi ktk SERIKALI ya TANGANYIKA/TANZANIA, leo wanakataa kuhusika, looh! Hayaetitegemee kuambiwa sasa kuwa walioamua kupandisha Kodi ya MAJENGO kuwa ni El shabaab wa SOMALIA au ISIS wa wapi vilee? Au watasema DP WORLD wa DUBEI, au mfalme wa SAUD ARABIA, aah, nisisahau huwenda watakuwa WACHINA au WA SOUTH KOREA?
Wajameni bagosha inatosha, wengine Burundi hatuna nauli kabisa kabisa!
Wale jamaa zetu kwa akina Onyango na Kalonzo Musyoka yaani Genetion - Z hawaji kutusaidia? Mbona tuna udugu wa damu damu
 
"Suala la ukusanyaji wa kodi za jengo kwa kutumia mita za LUKU ulishahamishwa kutoka TRA kwenda kwenye halmashauri na manispaa na majiji, imerudishwa serikali za mitaa.

TRA haihusiki tena na ukusanyaji wa kodi kupitia hizo LUKU." - Paul Walalaze, Meneja Elimu kwa Mlipakodi TRA alipoulizwa na Swahili Times kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya ongezeko la makato kwenye kununua umeme

PIA SOMA
- Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya
Sawa na je hao Tanesco wameiwekaje na inaenda wapi?

Je mnahusikaje na yule ofisa wenu aliyekutwa na Bil 7 ndani ya nyumba mnalisemeaje hilo nalo????!!
 
Hii nchi ingekua nyumba ya kupanga ningehama. Kikundi kidogo cha wateule kimetugeuza mazuzu.
 
Naomba mifumo yenu muiweke sawa, maana huwezi kukwambia mwananchi kuwa anadaiwa tozo zaidi ya 20,000 kwenye MITA na Kila mwezi anaponunua umeme tozo zinakatwa?
 
Back
Top Bottom