Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
KAIMU Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Arusha, Kayobio Majogoro(41), ameieleza mahakama kwamba ofisi yake haikuwa na taarifa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya, kuongoza kikosi kazi maalumu kwenda kukusanya kodi katika Jiji la Arusha.
Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa Serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga mbele ya hakimu mkazi, Patrisia Kisinda shahidi huyo amedai kuwa kwa mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kuunda kikosi kazi maalum ni kamishna mkuu wa TRA. Ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa mkuu wa wilaya hawezi kuwa na jukumu la kukusanya kodi.
Katika shauri hilo la uhujumu namba 27,2021, washtakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.
Chanzo: Nipashe