TRA: Hatukumtuma Sabaya kukusanya kodi

TRA: Hatukumtuma Sabaya kukusanya kodi

Mwenye mamlaka ya kuunda kikozi kwa ajili ya kukusanya kodi ni kamishna wa TRA... Mamlaka nyingine yoyote hata kama ni ya uteuzi, HUWA ZINAAGIZA MWENYE MAMLAKA YA KUFANYA HIVYO AFANYE... na si kuunda wenyewe
anasema alitumwa na Mzee, kwani TRA si ipo chini ya Mzee.
 
Sabaya alikuwa mwizi tuu aliyevaa shati la kijani kuhalalisha uhuni wake. Na merehemu nae kwakuwa alikua muhuni akawa anamkingia kifua. Mungu siyo jumanne kafa kamwachia msala bwamdogo hili ni somo kwa tuliobaki.
 
TRA haikuwa mamlaka ya uteuzi ya Lengai Ole Sabaya

Mamlaka ya juu ilikuwa inajua na ilibariki operesheni hiyo

Waziri wa fedha wa wakati huo alikuwa anajua na kubariki zoezi zima

Gavana wa benki kuu alikuwa anafahamu na alitambua kazi nzuri kwa kumpongeza hadharani (In a televised record)

Kama hakutumwa na makusanyo alifanya na kukabidhi ama mamlaka iliyomtuma au hazina kwanini walizipokea?

Mashahidi wanatakiwa kuongezeka (waziri wa fedha na mipango wa wakati huo) ( gavana wa benki kuu), (katibu mkuu hazina na mlipaji mkuu wa serikali), kiongozi wa wilaya au mkoa husika zoezi lilikofanyikia walikuwa na taarifa na hawakuzuia.

Hata mamlaka iliyopo sasa ilikuwa na taarifa lakini hakuna hata mmoja aliyetoa notisi ya kujiuzulu kwa kutoridhika na operesheni iliyokuwa inafanyika.

Huyo kijana Lengai Ole Sabaya aachiwe samba na Freeman Aikaeli Mbowe WAACHIWE wote maana kesi zao zimegubikwa na chuki za kisiasa
Serikali haifanyi kazi kwa "hear say" kijana .Ole sabaya anaposema alipata amri kutoka juu aoneshe uthibitisho wa barua au documents zinazomuonesha kuwa aliagizwa. Mahakamani hakufanyiki maigizo na serikali haifanyii kazi maneno matupu.
 
KAIMU Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Arusha, Kayobio Majogoro(41), ameieleza mahakama kwamba ofisi yake haikuwa na taarifa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya, kuongoza kikosi kazi maalumu kwenda kukusanya kodi katika Jiji la Arusha.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa Serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga mbele ya hakimu mkazi, Patrisia Kisinda shahidi huyo amedai kuwa kwa mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kuunda kikosi kazi maalum ni kamishna mkuu wa TRA. Ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa mkuu wa wilaya hawezi kuwa na jukumu la kukusanya kodi.

Katika shauri hilo la uhujumu namba 27,2021, washtakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Chanzo: Nipashe
Hadi mawe yatamkana
 
Ila nyie asa mtu uko mkoa mwingine unaenda mkoa mwingine yani viherehere vingine bhana acha yamkute ya kumkuta.....

watu kam hawa ni kama wale watoto wakorofi unakut litoto limenasa kwenye tube la tairi ya gari asa ukijiuliza kafikafikaje uko, alikua anatafuta nini uko unaishia kuchoka na kucheka kama sio kukasirika..[emoji38]
 
TRA haikuwa mamlaka ya uteuzi ya Lengai Ole Sabaya

Mamlaka ya juu ilikuwa inajua na ilibariki operesheni hiyo

Waziri wa fedha wa wakati huo alikuwa anajua na kubariki zoezi zima

Gavana wa benki kuu alikuwa anafahamu na alitambua kazi nzuri kwa kumpongeza hadharani (In a televised record)

Kama hakutumwa na makusanyo alifanya na kukabidhi ama mamlaka iliyomtuma au hazina kwanini walizipokea?

Mashahidi wanatakiwa kuongezeka (waziri wa fedha na mipango wa wakati huo) ( gavana wa benki kuu), (katibu mkuu hazina na mlipaji mkuu wa serikali), kiongozi wa wilaya au mkoa husika zoezi lilikofanyikia walikuwa na taarifa na hawakuzuia.

Hata mamlaka iliyopo sasa ilikuwa na taarifa lakini hakuna hata mmoja aliyetoa notisi ya kujiuzulu kwa kutoridhika na operesheni iliyokuwa inafanyika.

Huyo kijana Lengai Ole Sabaya aachiwe samba na Freeman Aikaeli Mbowe WAACHIWE wote maana kesi zao zimegubikwa na chuki za kisiasa
Labda alitumwa kukusanya KODI RUSHWA na siyo kodi ya kawaida inayojulikana na watu wote...!
 
TRA haikuwa mamlaka ya uteuzi ya Lengai Ole Sabaya

Mamlaka ya juu ilikuwa inajua na ilibariki operesheni hiyo

Waziri wa fedha wa wakati huo alikuwa anajua na kubariki zoezi zima
Mantiki kali! Bila shaka rais wa taifa na waziri wa fedha walfuatilia habari za duka la rejareja na risiti zake!! Maana sisi sote tunajua hawana kazi nyingine au muhimu zaidi, sivyo?
 
anasema alitumwa na Mzee, kwani TRA si ipo chini ya Mzee.

Fuso - timu ili iwe halali kisheria lazima iuende na mamlaka halali! Mamlaka halali ya kuuna timu yako na Kamishna wa TRA. Ingeweza kuwa halali pia kama ingeonekana kuundwa na mzee lakini kamishna kairidhia angalau kwa maandisha.

Leo akiulizwa Sabaya alisimikwa namna gani katika timu hiyo iliyokuwa na yeye na walinzi wake atabaki kusema “niliambiwa na mzee”. Mahakamani “i said he said” haikuwahi kuwa uthibitisho usiokuwa na mashaka! Inakuwaje timu hii ya kukusanya kodo isiwe na hata mmoja wa TRA??[emoji15]
 
Arusha. Kaimu meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Kayobyo Majogolo(41) ambaye ni shahidi wa pili katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita ameieleza mahakama kuwa kwa mujibu wa sheria anayepaswa kukusanya kodi ni mamlaka hiyo tu.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa Serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga mbele ya hakimu mkazi, Patrisia Kisinda shahidi huyo amedai kuwa kwa mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kuunda kikosi kazi maalum ni kamishna mkuu wa TRA.

Ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa mkuu wa wilaya hawezi kuwa na jukumu la kukusanya kodi.

Katika shauri hilo la uhujumu namba 27,2021, washtakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya

shahidipic.jpg
 
View attachment 1950953
Anadharirisha jezi ya Yanga huyo. Aivue, alavae jezi yake ya Simba.
 
Back
Top Bottom