TRA: Hatukumtuma Sabaya kukusanya kodi

TRA: Hatukumtuma Sabaya kukusanya kodi

Rais Magufuli alisema hadharani na mawaziri walisema hadharani kwamba Rais anatupigia simu kutoa maelekezo usiku, msikitini, Jumapili, siku ya Iddi, muda wowote, kufanya lolote. Utamwambia nipe maandishi?

Foregn Minister Kabudi aliagizwa akashughulikie migogoro ya ardhi Ifakara, mnakumbuka ? Kabudi angemwambia JPM nipe maandishi?

Jaji wa Mahakama Kuu most likely ameshaagizwa kitu na Jaji Mkuu ambacho Jaji Mkuu amemwambia kwenye simu hiki kitu kinatoka kwa Rais. Jaji atasema nipe maandishi ?

Kwa hiyo Jaji anaelewa how the innards of the regime operates. Hawawezi kumfunga miaka 30 kwa kufanya kitu ambacho wao wenyewe wanafanya hata leo hii. Huo ndio mfumo. Watawala wetu huwa hawapindishi taratibu za mfumo hata siku moja, never!

Sabaya anapaswa kutoa a detailed and credible narrative ya maongezi yake na Rais, na kutaja majina ya liasons wa Rais ambao walikuwa kwenye mlolongo. His State House contacts and Inteligence handlers.

Sabaya anapaswa kuleta mahakamani high profile retirees, wazee waliofanya kazi na Ikulu, waseme mahakamani kwamba 90% ya maagizo ya Rais ni ya mdomo. Sabaya baba yake alikuwa presidential appointee pia ( RC ? ), hawezi kukosa hizo connections and support.

Sabaya anapaswa kumwambia wakili aombe secluded sidebar ( majadiliano ya siri mahakamani) ambapo atamtajia jaji makachero wa TISS ambao walikuwa wanampa Rais taarifa na wanampa yeye taarifa wapi pa kuvamia.

Anything less than such legal efforts is incompetent representation.
Rais anapoongea, huwa kuna wanaoandika.
 
Rais anapoongea, huwa kuna wanaoandika.
Notes za presidential aids ni useless kama Rais ametoa direct order hapo hapo jambo lifanyike.

Kuna siku JPM alikuwa frustrated na Lukuvi. Akamwambia Waziri wa Mambo ya Kigeni “wewe Kabudi baki hapa tatua huu mgogoro wa ardhi haraka”!

Unadhani Kabudi aliondoka Morogoro that night kwenda ofisini kwake Dodoma kusubiri barua ya maagizo ? Bosi anakutuma kwa mdomo ubishe ?

Mnafanya kazi wapi nyinyi watu ?????
 
K
TRA haikuwa mamlaka ya uteuzi ya Lengai Ole Sabaya

Mamlaka ya juu ilikuwa inajua na ilibariki operesheni hiyo

Waziri wa fedha wa wakati huo alikuwa anajua na kubariki zoezi zima

Gavana wa benki kuu alikuwa anafahamu na alitambua kazi nzuri kwa kumpongeza hadharani (In a televised record)

Kama hakutumwa na makusanyo alifanya na kukabidhi ama mamlaka iliyomtuma au hazina kwanini walizipokea?

Mashahidi wanatakiwa kuongezeka (waziri wa fedha na mipango wa wakati huo) ( gavana wa benki kuu), (katibu mkuu hazina na mlipaji mkuu wa serikali), kiongozi wa wilaya au mkoa husika zoezi lilikofanyikia walikuwa na taarifa na hawakuzuia.

Hata mamlaka iliyopo sasa ilikuwa na taarifa lakini hakuna hata mmoja aliyetoa notisi ya kujiuzulu kwa kutoridhika na operesheni iliyokuwa inafanyika.

Huyo kijana Lengai Ole Sabaya aachiwe samba na Freeman Aikaeli Mbowe WAACHIWE wote maana kesi zao zimegubikwa na chuki za kisiasa
Katika watu wasiofikiri kumbe nawewe umooo?
 
Notes za presidential aids ni useless kama Rais ametoa direct order hapo hapo jambo lifanyike.

Kuna siku JPM alikuwa frustrated na Lukuvi. Akamwambia Waziri wa Mambo ya Kigeni “wewe Kabudi baki hapa tatua huu mgogoro wa ardhi haraka”!

Unadhani Kabudi aliondoka Morogoro that night kwenda ofisini kwake Dodoma kusubiri barua ya maagizo ? Bosi anakutuma kwa mdomo ubishe ?

Mnafanya kazi wapi nyinyi watu ?????
Elewa ninachoongea, hata kama ni direct orders, mchukua note ni lazima afanye kazi yake. Wewe unadhani baada ya kumuagiza vile Kabudi hayakuwekwa kwenye maandishi? Pamoja na utekelezwaji wake kuanza lakini kwenye maandishi lilishawekwa na siyo swala la kusubiri barua bali ni swala la kumbukumbu ya maagizo aliyotoa rais, pia kwa ajili ya ufuatiliaji.
 
Rais Magufuli alisema hadharani na mawaziri walisema hadharani kwamba Rais anatupigia simu kutoa maelekezo usiku, msikitini, Jumapili, siku ya Iddi, muda wowote, kufanya lolote. Utamwambia nipe maandishi?

Foregn Minister Kabudi aliagizwa akashughulikie migogoro ya ardhi Ifakara, mnakumbuka ? Kabudi angemwambia JPM nipe maandishi?

Jaji wa Mahakama Kuu most likely ameshaagizwa kitu na Jaji Mkuu ambacho Jaji Mkuu amemwambia kwenye simu hiki kitu kinatoka kwa Rais. Jaji atasema nipe maandishi ?

Kwa hiyo Jaji anaelewa how the innards of the regime operates. Hawawezi kumfunga miaka 30 kwa kufanya kitu ambacho wao wenyewe wanafanya hata leo hii. Huo ndio mfumo. Watawala wetu huwa hawapindishi taratibu za mfumo hata siku moja, never!

Sabaya anapaswa kutoa a detailed and credible narrative ya maongezi yake na Rais, na kutaja majina ya liasons wa Rais ambao walikuwa kwenye mlolongo. His State House contacts and Inteligence handlers.

Sabaya anapaswa kuleta mahakamani high profile retirees, wazee waliofanya kazi na Ikulu, waseme mahakamani kwamba 90% ya maagizo ya Rais ni ya mdomo. Sabaya baba yake alikuwa presidential appointee pia ( RC ? ), hawezi kukosa hizo connections and support.

Sabaya anapaswa kumwambia wakili aombe secluded sidebar ( majadiliano ya siri mahakamani) ambapo atamtajia jaji makachero wa TISS ambao walikuwa wanampa Rais taarifa na wanampa yeye taarifa wapi pa kuvamia.

Anything less than such legal efforts is incompetent representation.
Wewe advocate umefafanua vizuri sana
 
TRA haikuwa mamlaka ya uteuzi ya Lengai Ole Sabaya

Mamlaka ya juu ilikuwa inajua na ilibariki operesheni hiyo

Waziri wa fedha wa wakati huo alikuwa anajua na kubariki zoezi zima

Gavana wa benki kuu alikuwa anafahamu na alitambua kazi nzuri kwa kumpongeza hadharani (In a televised record)

Kama hakutumwa na makusanyo alifanya na kukabidhi ama mamlaka iliyomtuma au hazina kwanini walizipokea?

Mashahidi wanatakiwa kuongezeka (waziri wa fedha na mipango wa wakati huo) ( gavana wa benki kuu), (katibu mkuu hazina na mlipaji mkuu wa serikali), kiongozi wa wilaya au mkoa husika zoezi lilikofanyikia walikuwa na taarifa na hawakuzuia.

Hata mamlaka iliyopo sasa ilikuwa na taarifa lakini hakuna hata mmoja aliyetoa notisi ya kujiuzulu kwa kutoridhika na operesheni iliyokuwa inafanyika.

Huyo kijana Lengai Ole Sabaya aachiwe samba na Freeman Aikaeli Mbowe WAACHIWE wote maana kesi zao zimegubikwa na chuki za kisiasa
Hebu tumia akiri basi. Kisheria rais hana mamlaka ya kumtuma yeyote kukusanya kodi ispokuwa kamishna tu. Shida wabongo wengi akiri hamna ndo mana mnaburuzwa
 
KAIMU Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Arusha, Kayobio Majogoro(41), ameieleza mahakama kwamba ofisi yake haikuwa na taarifa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya, kuongoza kikosi kazi maalumu kwenda kukusanya kodi katika Jiji la Arusha.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa Serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga mbele ya hakimu mkazi, Patrisia Kisinda shahidi huyo amedai kuwa kwa mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kuunda kikosi kazi maalum ni kamishna mkuu wa TRA. Ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa mkuu wa wilaya hawezi kuwa na jukumu la kukusanya kodi.

Katika shauri hilo la uhujumu namba 27,2021, washtakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Chanzo: Nipashe
Huyu mtoto anatolewa kafara
 
Mawakili wa Sabaya bila shaka watawaburuza kortini mama Samia na bwana Isidory Nzabayanga Ntizobangizwa Mpango wakamtete Sabaya

Ila hawataenda maana wanajua kibao kitawageukia kwani kimsingi hawana mamlaka kisheria kuagiza hizo task force za kinyang’anyi nyuma ya pazia.
Mbona hili jina si miongoni mwa majina ya kiTanzania !. “Nzabayanga Ntizibangizwa”🙄🙄🙄
 
TRA haikuwa mamlaka ya uteuzi ya Lengai Ole Sabaya

Mamlaka ya juu ilikuwa inajua na ilibariki operesheni hiyo

Waziri wa fedha wa wakati huo alikuwa anajua na kubariki zoezi zima

Gavana wa benki kuu alikuwa anafahamu na alitambua kazi nzuri kwa kumpongeza hadharani (In a televised record)

Kama hakutumwa na makusanyo alifanya na kukabidhi ama mamlaka iliyomtuma au hazina kwanini walizipokea?

Mashahidi wanatakiwa kuongezeka (waziri wa fedha na mipango wa wakati huo) ( gavana wa benki kuu), (katibu mkuu hazina na mlipaji mkuu wa serikali), kiongozi wa wilaya au mkoa husika zoezi lilikofanyikia walikuwa na taarifa na hawakuzuia.

Hata mamlaka iliyopo sasa ilikuwa na taarifa lakini hakuna hata mmoja aliyetoa notisi ya kujiuzulu kwa kutoridhika na operesheni iliyokuwa inafanyika.

Huyo kijana Lengai Ole Sabaya aachiwe samba na Freeman Aikaeli Mbowe WAACHIWE wote maana kesi zao zimegubikwa na chuki za kisiasa
Unajua Kazi ya commissioner wa TRA?!!..Mkuu wa wilaya anaenda kutafuta Kodi?!!.. Alikua na wakaguzi wa Mapato?!!...Tufukirie zaidi!!
 
TRA naona ni wanafiki tuu vitu vyote alivyofanya Sabaya tulikua tunaona ITV hasa lile la maduka ya Moshi alivyoenda na baadhi ya maafisa wa TRA nilishangaa sana ila sikuona taarifa yeyote kutoka TRA kupinga leo wao tena wanakuja kupinga waliekuwa wanamtuma wakati watu washaumia..kwa hiyo Nchi hii mtu yeyote anaweza kufanya operations za kihuni na mamlaka husika zinakaa kimya mpaka watuhumiwa wapelekwe mahakamani..
 
Hakuna video iliyowahi kuonyesha Sabaya alikuwa na maofisa wa TRA kwenye hii ujangili wake ambao ndio msingi wa kesi rather walikuwa no wahuni ambao hata sio watumiaji wa serikali na ndio hao ameshtakiwa nao.

Hebu jiulize mbona dereva wake hajashtakiwa au kuunganishwa na Sabaya ingali alikuwa kwenye hiyo kampeni bubu?

Huyo bwana Hana pa kushika maana aliyemshikilia kamba imekatika watu walikuwa wanamsubiria tu kamba ikatike.

Mwenzie Makonda alipoa mapema maana nae angekuwa ananyea debe kama angeendelea upuuzi wake
 
KAIMU Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Arusha, Kayobio Majogoro(41), ameieleza mahakama kwamba ofisi yake haikuwa na taarifa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya, kuongoza kikosi kazi maalumu kwenda kukusanya kodi katika Jiji la Arusha.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa Serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga mbele ya hakimu mkazi, Patrisia Kisinda shahidi huyo amedai kuwa kwa mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kuunda kikosi kazi maalum ni kamishna mkuu wa TRA. Ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa mkuu wa wilaya hawezi kuwa na jukumu la kukusanya kodi.

Katika shauri hilo la uhujumu namba 27,2021, washtakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Chanzo: Nipashe
Huyu lazima ale mvua za kutosha
 
TRA naona ni wanafiki tuu vitu vyote alivyofanya Sabaya tulikua tunaona ITV hasa lile la maduka ya Moshi alivyoenda na baadhi ya maafisa wa TRA nilishangaa sana ila sikuona taarifa yeyote kutoka TRA kupinga leo wao tena wanakuja kupinga waliekuwa wanamtuma wakati watu washaumia..kwa hiyo Nchi hii mtu yeyote anaweza kufanya operations za kihuni na mamlaka husika zinakaa kimya mpaka watuhumiwa wapelekwe mahakamani..
Nchi ina mifumo ya hovyo sana mkuu
 
Notes za presidential aids ni useless kama Rais ametoa direct order hapo hapo jambo lifanyike.

Kuna siku JPM alikuwa frustrated na Lukuvi. Akamwambia Waziri wa Mambo ya Kigeni “wewe Kabudi baki hapa tatua huu mgogoro wa ardhi haraka”!

Unadhani Kabudi aliondoka Morogoro that night kwenda ofisini kwake Dodoma kusubiri barua ya maagizo ? Bosi anakutuma kwa mdomo ubishe ?

Mnafanya kazi wapi nyinyi watu ?????

Maagizo ya bosi nje sheria taratibu na kanuni ni batili, kwamba utii kila kitu bila kujali taratibu
 
kwani Gavana nae anakinga ya kutokushitakiwa,kwanini asipande kizimbani kutoa ushahidi kesi ikaisha mbona bongo kunakua na mlolongo mrefu huku mtu akisota rumande na hakuna hata anaejali bali watu wako buzy kumtetea mbowe wao aachiwe huru eti mpaka ushahidi utakapo kamilika mbona kwa watu wengine wala hawapigi kelele.Shame on upinzani wa Tz
 
Ingekuwa US ,nchi inaendeshwa kwa verbal instructions, Trump mpaka leo angekuwa President. Revisit Governor being told to find 11000 votes
 
Back
Top Bottom