Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Matatizo ya mashine za EFD yapo ya aina nyingi tangu umiliki wake mpaka katika matumizi.
Ukichunguza sana utagundua hizi mashine kama hazifanyi kazi ya kukushanya kodi peke yake bali na kumnyonya mfanyabishara. Hali hiyo ndiyo inayopelekea kufukuzana baina ya watumishi wa TRA na walipa kodi
1. Nikianza kwenye ulazima wa kumiliki hizi mashine hakuna mchanganuo wa uhakika juu ya nani anastahiki kuanza kutumia na nani sio lazima. Kuna wafanyabiashara hulazimishwa kununua mashine hizo wanapoanza tu biashara japo mitaji yao ni midogo sana na hata hajapata wateja katika biashara yake.
2.Umiliki huo hauzingatii aina ya biashara anayofanya mfanyabiashara.Kuna biashara kwa kweli haziendani na matumizi ya mashine hizo ambazo ni rahisi kuharibika.Mfano biashara sehemu za maji maji na vumbi.
3.Kanuni na kampeni kwa mlipa kodi ni kuwa ukiuza toa risiti na ukinunua dai risiti.Maana yake ni kuwa hata ukiuza kitu cha shilingi 100 mteja ana haki ya kudai risiti na una wajibu wa kumtolea risiti
Iwapo unauza shilingi 10000 kwa siku na biashara yako ni hiyo ya 100 mia basi kwa siku unaweza ukafikia kiwango cha risiti 1999 ambacho ndicho kiwango kinachofanya mashine ijae na kulazimika kununua nyengine.
4.Mashine ikiharibika unatakiwa utoe taarifa na kuitengeneza haraka.Kinyume chake ufunge biashara.
Sasa mashine zenyewe nyingi ni mbovu sana.Hazihimili vishindo na matengenezo ni ghali si chini ya 59,000/.Kwanini zisiagizwe mashine za matumizi yasiyokuwa na mazonge na ufundi ikawa ni kitu huru ukiondoa mifumo ya kielektronic ambayo itabaki kwao TRA.
4.Kuna taarifa kwamba mashine ukinunua unarejeshewa pesa.Urejeshwaji wa pesa hizo ni kitu hewa na hautekelezwi au urasimu wake unachosha.
Na kama kweli upo utaratibu huo basi hiyo pesa inayorejeshwa kwa kujaa mashine halafu ikastahiki kutupwa ni pesa ya walipo kodi.Kwanini TRA wasiagize mashine ambazo zikijaa zinafutika na kuendelea kutumika badala ya kuzitupa.