TRA itoe motisha kwa walipa kodi

TRA itoe motisha kwa walipa kodi

DidYouKnow

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,229
Reaction score
1,950
Mimi sio mchumi wala mbobezi wa tabia za binadamu. Natoa ushauri kama lay person.

Toka TRA ianze kufanya kazi mnamo Julai 1, 1996 kumefanywa maboresho madogo sana ya upande wa kuzitambua tabia za walipa kodi. Ni kweli kwamba duniani kote wafanyabiashara wengi hawapendi kulipa kodi, na kuna nchi ambazo kodi husumbua hata wananchi wa kawaida, na wengine hudiriki kuhama nchi zao. Sisi kama Watanzania ninaamini tunaweza tengeneza Taifa la watu wenye kupenda kulipa kodi.

Bahati mbaya sheria/kanuni/miongozo zinazotumika na TRA ili kufanikisha makusanyo ya kodi, zote zimekuwa zinatumia uimarishaji hasi (negative reinforcement) kuhakikisha watanzania na wageni wanalipa kodi. Hizi negative reinforcement zikifikia pabaya huhusisha kufunga akaunti za wafanyabiashara na hata vifungo kwa wakosaji.

Kwenye negative reinforcement mtu anatii kufanya kitu maagizo fulani hata kama hayapendi kwa hofu ya kichocheo cha kuchukiza (aversive stimulus) au matokeo hasi (negative outcome). Negative reinforcement ni kama mchezo wa Tom & Jerry.

Pamoja na kutumia negative reinforcement na kupata mafanikio, matokeo makubwa yatapatikana zaidi tukiongeza kutumia uimarishaji chanya (positive reinforcement) kukusanya kodi zaidi.
Mfano
1. Toa punguzo la asilimia ya bei/kodi kwa mtu anayenunua kitu fulani dukani na kupata risiti.
2. Kuweka kitambulisho au cheti kwenye duka/ofisi ya mlipa kodi wazuri ili kila mteja akione na ikiwezekana kiwe na Barcode hata mteja akitaka ku scan anapata uthibitisho.
3. Kuongeza matumizi ya manunuzi ya bila cash kwa kutoa motisha ya matumizi ya kadi na simu ambayo ni rahisi ku kufuatilia manunuzi, na hapa pesa ya TRA iwe inakatwa juu kwa juu. Makato ya huduma za malipo za simu yawe madogo na yananane kwa kampuni zote.
4. Hesabu nyingi za mlipa kodi ziwe moja kwa moja kupitia makato ya juu kwa juu ya TRA

Negative reinforcement itaendelea kuwepo, mfano kwa kuongeza kodi kwa baadhi ya manunuzi ambayo sio essential yanayofanywa kwa kutumia cash kuanzia kiasi fulani cha pesa.

Lakini pia ajira za TRA zihusishe taaluma mbalimbali, wale wanaopaswa kuongeza ukusanyaji kodi kwa positive reinforcement wawepo wa kutosha. Hii ina maana TRA kunapaswa wawepo psychologists au behaviorists, engineers, medical professionals, walimu n.k. Kukusanya kodi sio kujua namba na kutishia tu. Kuna vitu vingi vya kuzingatia.

Copied kwenye group la O-level
 
Back
Top Bottom