Ufanisi ktk bandari ya dar es salaam unategemea sana efficient ya TRA. Mamlaka hii imekuwa ni kikwazo kikubwa kwani imegubikwa na rushwa ktk kila idara.Mfano kwa documents za transit unapozi lod kwenye system yao ya asy scan huchukua mpaka wiki kwa wao tra kuifanyia kazi hasa hasa kwenye department kama documentary na error management. ili documents zako zifanyiwe kazi inakupasa kutoa rushwa ya sh. 20,000 kwa kila documents. ninawaomba taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa walimulike hili swala kwa umakini. pia serikali itambue kwamba kuna trend kubwa sana ya wateja waliokuwa wakitumia banadari yetu hii wanaamia bandari za waivers bay (namibia) darbun (sa), mombasa na mozambique. gharama za kulipia mizigo zimekuwa ni kubwa sana haswa pale mteja anapochelewa kutoa mzigo wake ndani ya siku 14( kwa mizigo ya transit) mfano baada ya cku 14 wanaanza ku charge cutomer warehouse rent ambayao cku za nyuma kama miezi 2 hivi nyuma walikuwa wakicharge baada ya cku 21, hii ni tofauti kabisa na gharama za storage na removal charges. Ukiritimba, ubinafsi na rushwa vinavyofanywa na tra, pta pamoja na watoa huduma za meli ndizo sababu za kuzorota kwa bandari yetu.