DOKEZO TRA Kipata nani anamkingia kifua Thom Lardha/Phares Lardha kupandisha kodi kubwa ghalfa ndani ya muda mfupi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Fortilo

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
5,807
Reaction score
17,416
Mwenye nyumba Kariakoo (Mtaa wa Sikukuu/Kipata) anataka kuvuruga watu. Hapo nyuma alikuwa anapokea kodi ya TZS 24,000,000/= p.a, lakini yeye analazimisha na mwanasheria wake kuandika kodi ya TZS 6,000,000 tu p.a.

Mwaka jana akasema kodi imepanda kutoka Mil 24 mpaka Mil 36! Akaambiwa kama anataka watu watoe hiyo pesa lazima zionekane kwenye mkataba.

Katika mambo yote hayo, akaamua kutoa vitisho kwa kutoa notice ili watu wahame, akaambiwa hilo halina shida lakini kodi ya serikali lazima ilipwe.

Sasa mikataba imeisha, mamlaka husika nendeni haraka mchukue kodi stahiki ya jengo zima lenye Frame zaidi ya 10, Godowns pamoja na Nyumba za kulala, rental apartments. Kodi kwa mwaka kwa jengo zima ni zaidi ya Mil 600, lakini kodi inayoripotiwa TRA haifiki milioni 100.

Watu wamekuwa wakifanya biashara katika kipindi kigumu sana kukiwa na rundo la malimbikizo ya kodi (Fine and charges) kutokana na reporting na mikataba ya ukwepaji kodi ya huyu bwana. Uthibitisho wa kutosha upo kuhakikisha suala hili linachukuliwa hatua stahiki.

Wageni hawatakiwi kuwanyonya hivi wenyeji wakaendelea kutamba tu kama vile hakuna kinachoendelea. Lazima wawajibishwe, tukitambua kwamba ni wajibu wa kila mtanzania mwenye kipato kulipa kodi stahiki. Fanyeni haraka ili mpata vithibitisho vyote vinavyohitajika kwenye suala hili.

Jamaa anatamba kuwa haogopi mahakama na kila siku yupo mahakamani, wao ni matajir wa mafuta, na kwamba asichezewe! Anaonekana kuwa mwenye kiburi na kujiona yupo juu ya sheria.

Wasalaam.

cc. TRA Tanzania Dr. Mwigulu Nchemba
 
Uzalendo wa hali juu tuone dana dana hapo....
 
Naona kama unajihatarishia mkuu,ungeachana nayo tu,huyo anakula na watu wazito
 
TRA hii labda ya zamani nyuma miaka kama 4 hv. Sio y sasa.
Na utakuta ni chawa wa CHURA uyo mwenye jengo KESI akuna.
KAZI ni kipimo cha utu TRA Tanzania oneni aibu basi fanyieni kazi tuhuma hz.
 
Wamiliki wa majengo ya biashara wana tabia hiyo.
Kodi inayoandikwa kwenye mkataba siyo inayolipwa .
Huu ni ukwepaji mkubwa sana wa kadi unaofanywa na hao wamiliki
Ni rahisi sana kukamatwa kama TRA wako serious.

Mfano, mkataba ameandika 6m lakini actual ni 50m, kama hiyo hela inalipwa at once kwenye bank account, ni rahisi kuomba evidence ya hiyo 50m imetoka wapi, kumtafta alielipa na atoe ushahidi wa mkataba wa kulipa 50m, haraka tu ukweli utajulikana.

Ama kufanya investigation ya chanzo kingine cha mapato cha mhusika, kuchukua mapato yake yote kwa mwaka kutoka vyanzo alivyovitaja na kuangalia inflows kwenye bank account yake, kisha kumuomba ushahidi wa extra income.
 
Mkuu una hoja na ni kweli ni kwa faida ya Taifa na sio faida yako. Sema tu ni wrong timing... Kwa maana inaonekana ulikua mnufaika wa hii situation toka zamani kabla ya ishu za kufukuzwa kwenye nyumba.

Ingekua umeitoa zamani ukiwa bado u mpangaji hapo then sawa. Ila kwa sasa inapunguza sana mashiko.

Anyway, hongera kwa uzalendo wako. Lakini kama wapo wengine kama wewe wenye kujua habari nyeti za ukwepaji kodi tuwaombe wazitoe sasa zifanyiwe kazi na sio kusubiri wakati wana bifu na mmiliki wa jengo. Taarifa nyingi yamkini zikawa ngumu kuzipata.

Asante!!
 
Huwa nawaza namna viongozi wetu wanavyojilimbikizia Mali za walipa Kodi Huwa nakosa kabisa uzalendo kama wa mleta mada wa kufichuwa wakwepa Kodi.Na tetesi inasemekana huyo jamaa ni rafiki sana wa abdul
 
Umejitolea hasa kuanika huu wizi sadly hii ni fursa kwa wakulungwa wa TRA.

Kwa hakika walikuwa wanajua kinachoendelea ila kulikuwa na fungu lao, kupitia uzi huu fungu limeongezeka sasa.

Wanaobariki huu upuuzi ni wale wale waliopaswa kuwa wanakemea.
 
Hongera sana kwa uzalendo wako.

Nyie ndo Watanzania mnaojitambua.

Nakushauri suala lako washirikishe pia Taasisi za Haki za Binadamu kama Legal and Human Rights Centre pamoja na watetezi wa Haki kama CHADEMA maana CCM walivyo madhalimu unaweza kukuta wakakugeuzia kibao ukatekwa na hata kuuwawa kutokana na kula na hao wahindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…