Mwenye nyumba Kariakoo (Mtaa wa Sikukuu/Kipata) anataka kuvuruga watu. Hapo nyuma alikuwa anapokea kodi ya TZS 24,000,000/= p.a, lakini yeye analazimisha na mwanasheria wake kuandika kodi ya TZS 6,000,000 tu p.a.
Mwaka jana akasema kodi imepanda kutoka Mil 24 mpaka Mil 36! Akaambiwa kama anataka watu watoe hiyo pesa lazima zionekane kwenye mkataba.
Katika mambo yote hayo, akaamua kutoa vitisho kwa kutoa notice ili watu wahame, akaambiwa hilo halina shida lakini kodi ya serikali lazima ilipwe.
Sasa mikataba imeisha, mamlaka husika nendeni haraka mchukue kodi stahiki ya jengo zima lenye Frame zaidi ya 10, Godowns pamoja na Nyumba za kulala, rental apartments. Kodi kwa mwaka kwa jengo zima ni zaidi ya Mil 600, lakini kodi inayoripotiwa TRA haifiki milioni 100.
Watu wamekuwa wakifanya biashara katika kipindi kigumu sana kukiwa na rundo la malimbikizo ya kodi (Fine and charges) kutokana na reporting na mikataba ya ukwepaji kodi ya huyu bwana. Uthibitisho wa kutosha upo kuhakikisha suala hili linachukuliwa hatua stahiki.
Wageni hawatakiwi kuwanyonya hivi wenyeji wakaendelea kutamba tu kama vile hakuna kinachoendelea. Lazima wawajibishwe, tukitambua kwamba ni wajibu wa kila mtanzania mwenye kipato kulipa kodi stahiki. Fanyeni haraka ili mpata vithibitisho vyote vinavyohitajika kwenye suala hili.
Jamaa anatamba kuwa haogopi mahakama na kila siku yupo mahakamani, wao ni matajir wa mafuta, na kwamba asichezewe! Anaonekana kuwa mwenye kiburi na kujiona yupo juu ya sheria.
Wasalaam.
cc. @TRA Tanzania @Dr. Mwigulu Nchemba