DOKEZO TRA Kipata nani anamkingia kifua Thom Lardha/Phares Lardha kupandisha kodi kubwa ghalfa ndani ya muda mfupi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hongera Kwa kujitoa muhanga,Mungu ni Mwema,Atakupigania;!iwe ni kweli sio kwa chuki Wala hasira.
 
Abduli
 
Walau tuwe na Watanzania 200 tu mfano wako mkuu, nchi yetu tutaondaka kwenye ombaomba

Mungu akutunze, na bila shaka mamlaka husika zinachukua hatua sasa
Wapo Watanzania si chini ya milioni moja mfano wa huyo, tatizo ni hatua stahiki hazichukuliwi zaidi ya wewe mtoa taarifa kuanza kubugudhiwa.

Lakini pia, kodi hii ndogo inayolipwa, inatumika vyema au inapigwa!!???
 
wenye nyumba wengi mikataba ya wazi hawataki.Alafu wapangaji wengi ni wanafiki unaweza wewe kusimamia msimamo wakweli wenzako wasikuunge mkono
 
wenye nyumba wengi mikataba ya wazi hawataki.Alafu wapangaji wengi ni wanafiki unaweza wewe kusimamia msimamo wakweli wenzako wasikuunge mkono
Hakika mkuu,kila mtu anajali yake,yakimkuta ndio analalama!
 
Tuanzishe uzi wa kuwafichua wenye nyumba wote ambao wamekuwa wakiongeza kodi alafu mkataba unasomeka tofauti ili wajue kwamba TRA inaitaji hiyo pesa nanamba zao.
 
Alipe tu kodi yake, kama biashara imemshinda aame.

TRA sio wapumbavu wanajua kodi ya pango ya maeneo tofauti au kwenye jengo.

Jirani yako hawezi lipa 20 million wewe ulipe 6 ukiona hivyo kuna ushirikiano wao.

Mambo mengine ni kukubali tu yaishe, kama tumeamua tunataka nchi ya aina hii.

Lakini ukiona unapewa receipt chini ya market rate ya eneo, elewa mwenye biashara ana maelewano na TRA.

Labda hayo malalamiko yako uyapeleke TAKUKURU.

Ni malalamiko yenye hoja, ila mambo kama hayo kwa serikali ya Tanzania kwa ni kama ‘hadithi ya mfa maji, aeshi kutapa-tapa’ nchi imeoza.
 
Hapo lazima kuna baadhi ya watu wa tiaraei wanahusika na wanaujua mpango wote

Ova
 
Hivi yale malalamiko ya yule mfanyabiashara smbdy ntuze yalifikia wapi???
Najuwa ntuze umauti ulimkuta hayupo tena duniani ??

Ova
 
Nadhani TRA wana kitengo cha whistleblowers

Wanawekaga na namba zao za simu
 
Kwa kuwa kaambiwa ahame ndo kaamua kumwaga mboga, mbona amemute siku zote hizo. Sawa nampomgeza kwa kumwaga "Mboga" 😁
 
Hivi yale malalamiko ya yule mfanyabiashara smbdy ntuze yalifikia wapi???
Najuwa ntuze umauti ulimkuta hayupo tena duniani ??

Ova
Ntunze ni nani tena? na assume ni yule mzee wa Tabora alieishia kujinyonga, baada ya kusumbuliwa sana na serikali. Sąd story.

Kama ni yule wa Kariakoo shida yake kubwa ni kutokua na mhasibu makini, na swala lake kutopitia mchakato TRAT/TRAB, shida yake ingepitia mchakato wa mahakama za usuluhishi wa kodi asingepata usumbufu ule.

Madai yake yalikuwa holela na maamuzi ya wanasiasa, ingelikuwa kupitia mahakama asingepata shida vile.

Hao ndio wafanyabiashara watanzania hawaelewi at what point wanahitaji professional accountants.

Na accountants nao hawaoni fursa (hiyo ni story nyingine).
 
Kwanza hongera kwa kujaribu kuwa mzalendo lakini kuna maswali ya kidogo hapa
1: Umejuaje kama analipa kodi kidogo tra kwa sababu hiyo ni siri ya mteja ?
2: Muda wote ulikuwa wapi mpaka baada ya kufukuzwa ndiyo unaleta mtandaoni malalamiko haya?
3: Ulishawahi muona meneja husika wa eneo hilo au hata kamishna yeyote wa tra?
4: Toka lini ukalipa kodi ya zuio withholding tax hali ya kuwa wewe ni mpangaji na siyo mnufaika wa malipo ( mwenye mali)?
5: Kama mkataba ulisema milioni 24 kwanini unakubali lipa 36 kipindi chote hicho hali ya kuwa uanajua mkataba na unacholipa ni tofauti?

Huoni kama ni majungu haya ?
 
Tatizo ni kwamba hao watu wanashirikiana na TRA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…