TRA: Kodi ya Mtandao inawalenga wale ambao hawana usajili wowote na wanafanya biashara kwa njia ya Mtandao

TRA: Kodi ya Mtandao inawalenga wale ambao hawana usajili wowote na wanafanya biashara kwa njia ya Mtandao

JamiiCheck

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2023
Posts
245
Reaction score
267
Julai 24, 2025, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda, alitoa wito kwa wafanyabiashara wa mitandaoni ambao hawajajisajili na TRA kujisajili mara moja ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Kamishna Mkuu Mwenda alisema wametoa mwezi mmoja kuanzia Agosti Mosi mpaka Agosti 31, 2025 wafanyabiashara wote wanaoendesha shughuli zao mtandaoni wajisajili TRA ili waanze kuchangia katika kulipa Kodi wakiwemo wenye nyumba wanaopangisha nyumba zao kutumia Air BNB na hawalipi kodi na watakaoshindwa watachukuliwa hatua kali.

Baada ya kutolewa kwa tangazo hili, kumeibuka mjadala mkali mtandaoni ambapo baadhi ya watu ikiwemo watumiaji wa JamiiForums.com kuhoji juu ya agizo hilo. Soma hapa TRA wakisema wafanyabiashara wa mitandaoni walipe kodi wanakuwa wanamaanisha nini?

photo_2025-07-28_12-50-34.jpg
​
Kutokana na uwepo wa mkanganyiko kuhusu suala hili, JamiiCheck imezungumza na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi - TRA, Richard Kayombo ili kupata ufafanuzi wa kina.

UFAFANUZI WA TRA...
"Utaratibu ambao umetangazwa na TRA unawalenga wale ambao hawana usajili wowote na wanafanya biashara kwa njia ya Mtandao, hivyo inamaanisha wanaikosesha Serikali mapato."

"Wale ambao wana biashara mfano duka na mengine na wanalipa kodi kwa uhalali kabisa wanapotumia mitandao kujitangaza wao hatuna shida nao kwa kuwa tunahesabu kwamba wanatumia mitandao kujitangaza."

"Siku hizi kuna njia nyingi za kutangaza biashara, hivyo suala la kutumia Mtandao ukiwa na biashara yako halali na umejisajili sio tatizo kwetu. Wale ambao hawajajisajili kabisa na hawapo kwenye mifuo ya kodi ndio tunaowatafuta na tumewapa muda wa mwezi mmoja wahakikishe wamejisajili."
 
Back
Top Bottom