carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepanga kuchunguza changamoto zinazowakabili wakulima wa miwa kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), kwa lengo la kurahisisha shughuli zao za biashara na kuwawezesha kutimiza wajibu wa kodi bila vikwazo visivyo vya lazima.
Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, amesema timu ya wataalamu itafanya uchunguzi huo kwa siku 30, ikipitia kanzidata za viwanda vya sukari na taarifa za wakulima wanaouza miwa viwandani ili kubaini njia bora za kurahisisha upatikanaji wa TIN.
Mwenda ameyasema hayo alipotembelea Kiwanda cha Sukari cha Kilombero mkoani Morogoro, akisisitiza kuwa TRA inalenga kuboresha mazingira ya biashara nchini.
Pia, ameipongeza Kampuni ya Sukari ya Kilombero kwa kuzingatia sheria za kodi na kusisitiza ushirikiano kati ya mamlaka hiyo, viwanda na wakulima.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero, Fakihi Fadhili, ameishukuru TRA kwa juhudi za kuboresha mazingira ya biashara, akieleza kuwa kiwanda hicho kinaendelea kuchangia upatikanaji wa sukari ya kutosha nchini, sambamba na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050
Chanzo : Tbc Online