TRA kulipia kodi scrapers tunaonewa?

Ndumbayeye

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2009
Posts
7,413
Reaction score
4,020
Natoka Tra nakuta tozo la kodi la sh laki tatu kwa miaka 4 iliyopita kwa pikipiki iliyokwisha kufa zamani. Naona sio haki kulipa kodi kwa chombo kilicho kwisha kufa
 
Kufanya kosa sio kosa... ila kurudia kosa hilo hilo ndio kosa.

Itumie vyema kadi yako ya kupigia kura ikifika 2020.
 
Natoka Tra nakuta tozo la kodi la sh laki tatu kwa miaka 4 iliyopita kwa pikipiki iliyokwisha kufa zamani. Naona sio haki kulipa kodi kwa chombo kilicho kwisha kufa
Mkuu, walikuita au ulijipeleka mwenyewe?. Yahani ilikuwaje hadi ukaenda tra kupigiwa hesabu za kitu kisicho kuwepo?
 
Kwan sheria inasemaje kama chombo kimekufa na hakiwezi kitengenezeks tena!? Tukishajua tutajua kama umeonewa ama lah
 
Natoka Tra nakuta tozo la kodi la sh laki tatu kwa miaka 4 iliyopita kwa pikipiki iliyokwisha kufa zamani. Naona sio haki kulipa kodi kwa chombo kilicho kwisha kufa

Kwan Tyre za boda boda yako uliziunganisha na Mfumo wa kodi wa TRA kiasi cha kujua kuwa sasa hivi huitumii?

Taratibu zinataka unapoacha biashara au kutumia chombo cha Moto kuijulisha TRA ndani ya siku 7
 
Tin no ni moja ukienda kulipia ya dukani inakutwa ulikuwa na bajaj mwaka 1998!
 
Kwan sheria inasemaje kama chombo kimekufa na hakiwezi kitengenezeks tena!? Tukishajua tutajua kama umeonewa ama lah
kuna utaratibu juu ya chombo kilicho kufa kutolewa taarifa pindi kinapokuwa kimekufa, wanakirekodi kuanzia hapo hutozwi kodi, km ulikaa kimya bila kuwajulisha unahesabika kuwa wewe ni mkwepaji wa kulipa kodi, period
 
TRA wanatumia sana ule usemi kuwa "kutijua sheria sio utetezi". Sheria iko wazi kuwa chombo kikiharibika kiasi cha kutoweza kutembea barabarani basi taarifa zake zipelekwe TRA ili malipo ya tozo la barabara (road lisence) yasimamishwe. Pia sheria hiyo inamtaka mmiliki wa chombo cha barabarani akiona chombo chake hakiwezi kutengenezeka atoe taarifa TRA aombe kufuta usajili wa chombo hicho.
Kutofanya hivyo kutasababisha chombo hicho kuelendela kutozwa tozo hiyo kila mwaka.
Kwa utaratibu wa sasa, ikiwa unadaiwa tozo ya barabara ya chombo chako na ukaenda TRA kwa shughuli nyingine kama kutaka kibali cha kufanya buashara au kulipa leseni ya udereva, wanakunasa hapohapo.
Ni ushauri wangu kwa TRA kuweka angalizo kwenye kadi za magari ili kuwakumbusha wamiliki wajibu huu.
 
Kufanya kosa sio kosa... ila kurudia kosa hilo hilo ndio kosa.

Itumie vyema kadi yako ya kupigia kura ikifika 2020.

Vitu vingine mtumie akili sio kila kitu Siasa EBBO.

Hivi nyie mnamiliki Chombo cha moto hata sheria zake hamjui?

TRA utataribu upo wazi,unapouza,unapopata ajali ambayo chombo kinakuwa W-off,kinapokufa yaani hakitumiki tena.Lazima utoe taarifa ili wakifute kwenye usajili wao.La Sivyo ni lazima utalipa na utatakiwa kulipa bila mjadala.Na kama mpo humu wengine mliouza magari yenu au pikipiki zenu bila kubadilisha na kutoa taarifa TRA basi mjue madeni yanawahusu na TRA kwa kasi hii wengi hamtoki.
Watanzania tupende kutafuta taarifa,TRA ukienda pale TRA unapokelewa vizuri sana na wamejipanga kweli kwenye kitengo cha maelezo kwa Mlipa kodi,unapewa maelezo mpaka basi.
Na utaratibu huo ni rahisi sana kuufanya.Matatizo mengine tunayataka wenyewe,kisha unalalamikia Serikali kwa uzembe wako mwenyewe.

Sasa kama unaishi mjini na hili hulijui,unaishije,aiseeee,kaaazi kweli,duhhhh

Ushauri:
Kama uliuza,uliibiwa,gari bovu halifanyi kazi tena.
Basi hakikisha kwamba unafuata utaratibu wa kutaarifu TRA juu ya hilo
La sivyo,unaelekea kuingia kwenye Janga na tatizo kubwa Mno.
Mbaya zaidi kuna watu wameuza gari kwa mtu na huyo mtu kauza na alieuziwa nae kauza.Bila kubadilisha Jina,hawa kwanza Jela nje nje gari ikifanya tukio la uhalifu kama Ujambazi,Kubeba nyara za Serikali nk,na pili TRA wanakuhusu mmiliki wa awali alie kwenye kumbukumbu zao.Na watu wengi na wahalifu wengi,siku hizi hutumia Mbinu hii kwa zile gari ambazo usajili wake ni wa mtu wa mbali ili wakutupie mshipa.
Tufuate Utaratibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…