TRA kwa hili sijawaelewa mwenye ujuzi anisaidie

Bugududu Sududu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2014
Posts
594
Reaction score
691
Habari zenu wakuu,
Mi nimeshindwa kuielewa hii kodi,
Huu mwezi wa 11
nimefanikiwa kuanzisha biashara yangu sasa nimefuatilia kila kitu na kwa levo yangu kodi nikaambiwa ni 150000 ambayo unaweza kuigawa mara 4,

Sasa ilipofika wakati wa kukadiriwa kodi naambiwa nilipe yote laki na nusu ambayo ni kodi ya mwaka mzima kabla ya tar 31 desemba eti nikichelewa napigwa faini.

Kinachonishangaza sijauza kitu chochote, afu natakiwa eti nilipe laki na nusu ambayo ni kodi kuanzia mwez januari hadi desemba wakati mimi biashara nimeanza mwez huu
Mwenye uelewa anijuze au kuna janja inachezwa??
 
Ndiyo ilivyo,,, na bado mwakani itakuwa 318,000/= kila mwaka inapanda tu,,, yalishatukuta,, mpaka sasa kwa sisi wengine tunaona TRA siyo rafiki
 
Ndiyo ilivyo,,, na bado mwakani itakuwa 318,000/= kila mwaka inapanda tu,,, yalishatukuta,, mpaka sasa kwa sisi wengine tunaona TRA siyo rafiki
Dah! Ni bora ningeamua kuwa machinga tu, natembea na duka langu mkononi,
Kuliko hili balaa nilo jitakia!!
 
Hicho ndio kiwango cha chini kabisa cha kulipa kodi, tatizo ni huyo aliyekukadilia kwani kama umebaki mwezi mmoja tu wa ki kodi angekushauri uende january 2019,ndio wakupe makadirio hayo, ya mwaka mzima! Na wewe pia ungekuwa na uelewa usingekwenda mwezi huu, ungesubiria hadi january. Hakuna ujanja hapo kama wamesha kukadiria ninlazima tu uilipe, pole sana mkuu
 
Asante ila niamua kuondoka na sirud tena TRA hadi januari kama fain na iwe tu!
 
Wale hua wana kimbilia kuangalia Tarehe gani umepata usajili, wanaanza kuhesabia hio siku ya kusajiliwa TRA. Hata kama vyeti uliweka kwenye kabati bila kuanza kazi muda wote wakati ukitafuta MTAJI na PANGO la kufungua biashara.

Cha msingi, nenda Makao Makuu Ya Wilaya (TRA) kapeleke malalamiko yako.
 
Asante ila niamua kuondoka na sirud tena TRA hadi januari kama fain na iwe tu!
Zile fomu walizokupa za makadilio ukalipie bank ulibaki nazo au? Uliwaachia, kama unazo au uliwaachia na bank hukwenda kulipa umepona, subilia january tu, kwani kwenye system hujaingizwa, na hiyo january nenda kama mteja mpya kabisa, na ikiwezekana usirudi kwa huyo aliyekukadiria nenda kwa mwingine. Japi kodi itakuwa ni hiyo hiyo ila utailipa kwa awamu nne!!
 
Kiongozi pale niliwaachia kila kitu mi nilichoondoka nacho ni TIN namba tu,

maana niliwaambia kuwa nitarudi basi nikaondoka moja kwa moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…