TRA mnalipeleka wapi Taifa? Hali ya hewa sio shwari na wafanyabiashara

TRA mnalipeleka wapi Taifa? Hali ya hewa sio shwari na wafanyabiashara

MLIPAKODI

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
234
Reaction score
89
[10:49pm, 4/27/2015] Mch. Kiondo: HALI YA HEWA SIYO SHWARI MIKOANI.

Ikumbukwe tarehe 6.09.014 mkutano wa kitaifa uliokuwa ni maagizo ya serikali ili kupata wajumbe katika uwakilishi wa kitaifa, watakaounda KAMATI YA PAMOJA KATI YA TRA NA JWT itakayopitia mfumo wa ulipaji kodi nchini, pia ili kufikia maridhiano ya namna bora ya matumizi ya EFDS.

TRA walikwepa kuitisha vikao hivyo vya kamati ya pamoja hadi tarehe 17.03.015 tena kwa kulazimishwa na Kamati ya Bunge ya kudumu ya uchumi viwanda na biashara.

Tarehe 08.04.015 kamati ndogo iliyoundwa na kamati hiyo kubwa, ilitengeneza mpango kazi na kuwasilisha bajeti, ambayo ilibidi itolewe na serikali kupitia TRA chini ya uangalizi wa ofisi ya Waziri Mkuu.
Hata hivyo, kwa taarifa kamili ni kesho tarehe 28.04.015 tutajua lini itaanza kutekeleza majukumu yake kivitendo.

Wakati kamati hii inapitia ulipaji kodi bandarini na namna ya utoaji mizigo bandari, kamati ilipendekeza matumizi ya nguvu ya utekelezaji wa sheria ya EFDS usitishwe, ili kupisha kamati kumaliza kazi yake kwa muda waliopewa.

CHA KUSIKITISHA TRA WAMEKUWA NA LUGHA MBILI MBILI JUU YA HILI.

Sambamba na hilo Wafanyabiashara wanakosa matumaini na hiyo kamati kama kweli mawazo ya kamati yatapewa nafasi na serikali.

Maduka yaliyokuwa yamefungwa 22.04.015 Mbezi yalifunguliwa 24.04.015 baada ya mvutano mkali sana na Kamishna wa EFDS Mama Bateyunga.

Waliokamatiwa mizigo Jangwani Dar es salaam 23.04.015 nasikitika maana baada ya mvutano mkubwa na Ma. Bateyunga alitoa utaratibu wa jinsi gani tufanye na kuagiza Meneja TRA Chipata ili aruhusu hiyo mizigo itoke.

Ndivyo, tulivyofanya na tulienda na wahusika mpaka ofisi ya TRA Chipata Meneja msaidizi kutoa maagizo kwa staff wa TRA awape mizigo yao.

Viongozi baada ya kuondoka hadi napoandika ujumbe huu hawajawapa mizigo yao.

Dodoma leo wamewapitishia Barua za notice za kununua EFDS wafanyabiashara wa eneo la Majengo ambapo leo ni tarehe 27.04.015 siku 3 baada ya TRA kusema wanasimamisha usumbufu kwa wafanyabiashara ili kuipa nafasi kamati.
[11:40pm, 4/27/2015] Mch. Kiondo: Mkoa wa Manyara:

Watu leo wamefungiwa maduka taarifa kamili kuhusu idadi nitatoa kesho.
Maofisa wa TRA wamemfuata mmojawapo wa kiongozi wa JWT Babati kwa vitisho vya maneno ikiwa ni pamoja na kumpa Barua ya kutaka arudi nyuma katika harakati.

Mkoa wa Katavi TRA, wamekuwa wakitangaza kwa magari na kutishia wafanyabiashara kwenda kulipa kodi ya ongezeko la aslimia 100% bila ya muongozo unaoeleweka, kwani JWT iliiandikia Wizara ya Fedha kutoa ufafanuzi, kwa barua ya tarehe 24.02.015 ambapo mpaka sasa hawajatujibu kiofisi.

Mkoa wa Iringa vivyo hivyo, ila kwa Iringa TRA wameenda mbali zaidi kwa kuwaandikia viongozi wote wa JWT mkoa wa Iringa kwamba wajieleze pamoja na kupeleka taarifa zao za kodi za miaka ya nyuma.

YALE YALE KWA M/KITI JWT TAIFA SASA YAMEHAMIA MIKOANI TUSUBIRI NA KESI NYINGI ZITAFUNGULIWA.

Mkoa wa Pwani, vivyo hivyo kuna mfanyabiashara alikamatiwa mizigo yake tangu tarehe 22.04.015 hadi sasa ni utata mtupu.

MASHAKA YANGU:

Tukikata tamaa wakati huu tujiandae kutafuta mashamba turudi vijijini maana zimwi limeingia TRA limekusudia kuua uchumi wa nchi na hamna kwenye meno ya kulimeza hili zimwi.

TRA haina nia ya dhati kumaliza mgogoro juu ya EFDS.

Jambo hili wanataka kulifanya la kisiasa tusikubali, tusirudi nyuma.

Tusipokuwa na mshikamano wa pamoja TRA hawana nia njema na wazawa wa nchi hii.

Pia, ni vema tukajiandaa saa ye yote kumalizwa na TRA.

HITIMISHO.

MUNGU AKIWA UPANDE WETU NANI ZAIDI AWEZAYE TENA KUTURUDISHA NYUMA - ni vitisho, kodi za kubambikizwa? au kifoo?
HAKUNA HAKUNA.

Nakuwa njia panda sijui kamati hii kama ina umuhimu kwa TRA au ni shinikizo tuu, ila wao naju haswa wale watakaomulikwa hawapo tayari kufunuliwa nguo.
Na hapa ndipo penye shimo linalofilisi nchi hii.

MUNGU NUSURU TAIFA HILI NAKUOMBA - AMEN.

Lazima tulikomboe Taifa letu tusiwaachie Wachina.

Imetolewa na Katibu Mkuu JWT - Taifa.

My take kwanini wasiharakishe hiyo kamati iliyoundwa ili itafute ufumbizi wa matatizo yaliyopo na TRA kwanini hawafuati makubaliano waliyokubaliana na JWT?
 
Hii migogoro kila kukicha shilingi itaacha kuporomoka kweli? Sijui kwa nn hii nchi wanapenda siasa kuliko uchumi, longolongo za nini? waseme kuwa hizo mashine hazitafutwa perid wafanya biashara wajue moja kuwadanganya kama watoto ni ubwege wa hali ya juu kwa hawa TRA.
 
Siku zote Hakuna mtu anayefurahia Kulipa Kodi duniani kodi huwa inachukiwa tuu Kinachotokea sasa hivi kwa wafanyabiashara walikua wamezoea ku underestimate Income ili walipe kodi Ndogo so hizi machine za Electronic Fiscal Device (EFD)

Zinasaidia sana kwani sasa hivi wanashindwa ku hide profit na sales zao then ndo maana wahaha! TRA kazeni Aisee Taifa haliwezi kuendelea kwa walipa kodi Wahuni.. Lipa Kodi kwa Maendeleo ya Taifa!s
 
Siku zote Hakuna mtu anayefurahia Kulipa Kodi duniani kodi huwa inachukiwa tuu Kinachotokea sasa hivi kwa wafanyabiashara walikua wamezoea ku underestimate Income ili walipe kodi Ndogo so hizi machine za Electronic Fiscal Device (EFD)

Zinasaidia sana kwani sasa hivi wanashindwa ku hide profit na sales zao then ndo maana wahaha! TRA kazeni Aisee Taifa haliwezi kuendelea kwa walipa kodi Wahuni.. Lipa Kodi kwa Maendeleo ya Taifa!s
Nimeipenda hii, utakuta mfanyabiashara anaigiza faida ya zaidi ya sh 10m kwa mwezi analipa kodi ya 150000 au chin ya hapo. Ukiangalia upande mwingine, mfanyakazi wa kipato sawa na hcho analipa kodi ya zaidi ya sh 2.5m. Wiz wa kodi ndio unafanya wafanyabiashara kuogopa kutumia EFDs machines
 
Back
Top Bottom