TRA Mwanza wapiga marufuku uzalishaji wa Power Banana hadi kiwanda kiwe na mashine ya kuweka stika za TRA

TRA Mwanza wapiga marufuku uzalishaji wa Power Banana hadi kiwanda kiwe na mashine ya kuweka stika za TRA

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Nimeskia kutoka kwa mdau mmoja TRA Mwanza wameipiga marufuku kampuni ya Mwanza Quality Wine Ltd wanatengezaji wa pombe maarufu mkoani Mwanza ya Power Banana wine kusitisha uzalishaji hadi wawe na mashine ya kuweka sticker za TRA ambayo inapatikana kwa M 400 kutokana na taarifa ya mdau

Na hili nasikia ni agizo kwa viwanda vyote vya pombe nchini

Tulizoea kuona sticker za TRA kwenye pombe Kali tena baadhi,sasa baada ya serikali kuona kuna viwanda vingi vya uzalishaji pombe Kali kama Shimha,Kitoko,Smart Gin na nyingine nyingi basi serikali imeamua kuleta fitna iongeze mapato kwa kuwataka wazalishaji wengine wawe na mfumo wa stika wakati wanalipa kodi vizuri.

Kama kuna ofisa TRA humu kutoka mwanza atuambie hili jambo ,manake hiki ni kinywaji pendwa kwa wakazi wa mwanza uwepo wa stika ni kukifanya kipande bei,Je ni kweli hili suala??View attachment 1040421
IMG_20190307_204248.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mashine ya mettler toredo inauzwa 27m tena inaunganishwa na mtandao wa tra inakuwa inatuma hesabu moja kwa moja kama efd.

Hivi pombe za kienyeji kama mnazi ulanzi kangala chimpumu mlamba rubisi nazo zinatakiwa kununua mashine?
 
Hao jamaa wamwandikie kamishna wa TRA awape grace period ya 3-6 months. For the mean time TRA ipeleke maafisa wake watakao kuwa stationed kwenye viwanda vyote visivyo na mashine ya stika na viwanda hivyo vitawajibika kumlipa 'verification officer' mshahara na marupu rupu mengine hadi pale watakapofunga mashine!
Kwa hiyo kila batch ikitoka verification officer atakuwa anarekodi kuwa ni bidhaa kiasi gani zimeingizwa sokoni na hivyo kujua ushuru stahiki ambao kiwanda husika kinatakiwa kuwalipa TRA.

Deal Done!
 
Dunia ni jukwaa, sisi sote ni wasanii.
Ninaweza nikajitekenya mwenyewe nikaanza kucheka, nikitarajia na wengine watacheka.
 
Hilo ni agizo kwa mikoa yote sio Mwanza tuu ni wazo zuri ila wangewapa muda hata mwaka mmoja hicho ni kiwanda watu wamekopa mnakuja na matamko ya muda mfupi mnaua biashara za viwanda vya pombe bila kujua...
 
Hao jamaa wamwandikie kamishna wa TRA awape grace period ya 3-6 months. For the mean time TRA ipeleke maafisa wake watakao kuwa stationed kwenye viwanda vyote visivyo na mashine ya stika na viwanda hivyo vitawajibika kumlipa 'verification officer' mshahara na marupu rupu mengine hadi pale watakapofunga mashine!
Kwa hiyo kila batch ikitoka verification officer atakuwa anarekodi kuwa ni bidhaa kiasi gani zimeingizwa sokoni na hivyo kujua ushuru stahiki ambao kiwanda husika kinatakiwa kuwalipa TRA.

Deal Done!

Mkuu unawazo zuri ila nadhani hapo tra watawatajirisha tu au ma verifiation officers kwa rushwa za kufa mtu.
Wataandaa mahesabu ya sio ya kweli na kulinyima taifa kodi wakati wao watapewa rushwa kubwa na hivyo viwanda.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ili twende mbele, binadamu inabidi tuaminiane tu at some points... Otherwise washushe malaika toka Mbinguni waje wafanye kazi kwa niaba yetu kwa kuwa sie hatuwezi kuaminiana...
 
Ili twende mbele, binadamu inabidi tuaminiane tu at some points... Otherwise washushe malaika toka Mbinguni waje wafanye kazi kwa niaba yetu kwa kuwa sie hatuwezi kuaminiana...
Point yako nzuri (hongera)pale kwenye kupewa grace period,achana na hawa verification officer's wanaweza tengeneza mianya ya kukwepa kodi zaidi!..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mtambo ni sawa na mtaji wa malighafi ya kiwanda. Poor tra..na mbege wakomae ziwekwe stika za tra
 
Back
Top Bottom