TRA na BRELA hamna la maana mfanyalo

TRA na BRELA hamna la maana mfanyalo

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Habari wadau,
Niko napitia gharama za licensing fees pamoja na taratibu.Ninavyoona ni kama vile hii kazi kuwapa halamashauri ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na ni gharama za ziada kwa wafanya biashara.Binafsi naangalia hili kwa mtazamo wa maendeleo ya kiteknolojia ambapo biashara nyingi zina sura ya kitaifa na kimataifa.

Kwanza kabisa gharama za kupata leseni ni kubwa sana yaani nyingine ni zaida ya gharama ya kodi ya mapato najiuliza hizo pesa zinalipia huduma gani hasa ambayo mfanya biashara anapata kutoka katika hamashauri.

Upataji wa leseni tu ya biashara kwa hapa jiji ni Dar es Salaama unahitaji sio chini ya laki mbili kwa biashara ndogo kabisa.Katika hali kama hii unatarajia nani atahitaji kuwa na leseni.Mbaya zaidi kigezo cha kupiwa leseni ni kulipa kodi ya mapato.Yaani serikali inataka watu walipie kodi biashara ambayo hata haijaanza.Unapoenda kwa watoa leseni wanataka uwe na taarifa ya kulipa kodi TRA ndo wakupe leseni.Huu ni ushenzi,ufisadi na unyonyaji ambao haupaswi kufumbiwa macho.

Nilitarajia hawa Brela wangeweka muwakilisha kwenye kila halamashauri au kwenye kila ofisi ya TRA au TRA wawe na hilo jukumu la kutoa leseni ambapo Brela wangesajili tu makampuni na biashara na TRA ambao ndio wakusanya kodi ndio wangehusika na kukadiria mapato na kutoa leseni kwa kuwa wao wana uzoefu wa kodi na aina ya biashara.

Huu usumbufu wa kutembea kwenye ofisi zaidi ya moja kwa ajili ya kutafuta huduma biala sababu ya msingi na kuongezewa ghrama za uendeshaji na upuuzi usiokuwa na maana.

Niwashauri TRA na BRELA na hawa halmashauri kaeni pamoja toeni huduma zenye kiwango sio kuwanyonya wananchi huku hata malengo ya makusanyo hamfikii kwa sababu ya kukosa weledi,ubunifu na uwajibikaji

Kama mnajielewa chukueni ushauri
 
Back
Top Bottom