TRA na Kodi ya Majengo (Property Tax) naombeni ufafanuzi katika hili

Hivi hawa watu wanashindwa kuweka karatasi mlangoni mpaka wanamua kuchora ukuta wa nyumba yangu ambayo nishapiga plasta? Sheria ikoje hapo? Je nikilipa watakuja wafute hizo rangi zao?
 
Nadhani hili eneo TRA walifanyie kazi, mimi niko Namtumbo kijijini huku kibali cha ujenzi napata wapi
Hapa ni mtendaji. Ukijenga unatakiwa upate kibali na ulipe kwa jengo unalotaka kujenga kwani wengine wanajenga maeneo yasiyoruhusiwa kama eneo la barabara nk. Vijijini pi kuna mipango ya maendeleo.
 
sio lazima uwe na TIN ili uweze kulipa kodi ya majengo, kodi utalipa kama umenga ndani jiji, manispaa, makao makuu ya wilaya au township zilizoainishwa
 
Nyumba zote za makazi ya kawaida isipokuwa migorofa, gharama za property tax ni TSHS. 10,000 kwa mwaka. Magorofa ni 50,000

Baada ya kuandikiwa nyumba yangu kwamba niwakilishe kibari, hatimae leo nimeenda jiji, wameniambia nitoe elfu 50, nikaenda kulipia beki wakanipa skatabadhi ya malipo, baada ya hapo wakaniambia KIBARI bado hatujakupa wakasema nitakuja na ramani ya nyumba ndani ya siku 60, sasa najiuliza kama ramani ya kutoka jiji sina, na nilipewa ramani na mtu nikajenga nyumba, utaratibu ukoje? Maana wanaomba ninavyosikia ramani inatakiwa iwe na mhuri wa mchoraji.
 
Mkuu sikuizi serikali ilishapitisha sheria ya kurasmisha makazi. Yaani unakuwa tayari ulishajenga nyumba yako bila kibali, hivyo katika kuirasmisha unachofanya ni kulipia pedsa ya kibali cha ujenzi TSHS 30,000 na kuwasilisha ramani za nyumba yako, kisha zinaidhinishwa! Hawawezi kuanza kukuchorea ramani nyingine wakati nyumba tayri ishajengwa! Hapo ni kurasmisha makazi tu!
 
Ahsante mkuu, lakini wanasema ramani iwe na muhuri sasa najiuliza huo mhuri nautoa wapi?
 
Kawalize wao wenyewe wanataka muhuri wa nani! Maana nijuavyo mimi watu wa halmashauri ndo huwanagonga mihuri ramani wakati wakizipisha. Kama ni muhuri wa mchoraji, azima hiyo ramani ulikoazima awali kisha itoe copy kisha mtafute mchoraji unaongea nae fresh najua kama ni pesa atakutoa kidogo sana kisha ipeleke!
 
Ahsante mkuu, leo nimeenda na ramani yangu wakasema ramani haijakamilika, ikabidi nitafute mchoraji, mchoraji nae kanambia elfu 50 nimeamua kuweka ndani kwanza maana procesa zinakuwa ndefu
 
Pole mkuu! Ila Wizara ya ardhi ilishatoa utaratibu rafiki sana wa kushugulikia jambo hilo sema tu kuna watu ndani ya halmashauri za miji na majii bado wanaendekeza sana urasimu!
 
Back
Top Bottom