TRA na PCCB wakiingilia hili suala la yanga TFF hawachomoki hapa

TRA na PCCB wakiingilia hili suala la yanga TFF hawachomoki hapa

Malalamiko yamebadilika tena? Kwa hiyo Yanga haidai tena hela za ubingwa?
kadri TFF wanavyozidi kuwa kichwa ngumu YANGA wanapiga spana mpya....kuna mengi hapo nyuma ya pazia
 
kadri TFF wanavyozidi kuwa kichwa ngumu YANGA wanapiga spana mpya....kuna mengi hapo nyuma ya pazia
Kama kila baada ya muda mfupi inakuja 'spana' mpya, basi yawezekana ile 'spana' iliyotangulia itakuwa haikufanya kazi.
Kuna msemo katika soka unasema "Never change a winning team"
 
Kama kila baada ya muda mfupi inakuja 'spana' mpya, basi yawezekana ile 'spana' iliyotangulia itakuwa haikufanya kazi.
Kuna msemo katika soka unasema "Never change a winning team"
spana zote zinazotolewa na YANGA zinafanya/zitafanya kazi,kuwa na subira ila uwe na akili timamu kuelewa zinafanyaje/zitafanyaje kazi
 
YANGA Vs TFF NGOMA BADO NZITO[emoji91]

Kwenye barua ya Yanga waliyoipeleka TFF leo ambayo Ujumbe wa Yanga uliongozwa na Mtendaji Mkuu, Andre Mtine na Mkurugenzi wa Fedha wameambatanisha INVOICE takribani tano.

YANGA hana tabu na kudai au kudaiwa ila anataka vitu viende kwa mfumo.

1-Invoice za Ubingwa Federation Cup zipo tatu kuanzia msimu wa 2021/22.

2-Invoice ya Fedha za Mapato ya Mlangoni zaMichuano ya CAF ambazo Yanga walikatwa na CAFambazo TFF hawajawalipa Yanga.

3- Invoice za Udhamini wa timu ya Wanawake naMashindano ya Vijana. Yanga pia wamesititiza TFF wapige hesabu zao na wana machaguo mawili baada ya hapo kuhusu Fedha zao

1-Kuweka fedha zote ambazo Yanga wanawadai, inakadiriwa MILLION 426 za Kitanzania, kisha TFFwatume INVOICE za Madeni yao yote Jangwani kisha Yanga walipe madeni hayo.

2- Kama TFF waliwakata fedha zote ambazo wanadaiwa, Yanga wanataka kujulishwa kwa USHAHIDIWA RISITI kama ambavyo Sheria za Kodi za nchi zinavyotaka kisha baki yao waingiziwe kwenye account yao ila Makato yote yawe na RISITI.

KISHA Yanga Msimamo wao ni kuwa hakuna maongezi yoyote na kama kuna maongezi (Reconciliation) basi Yanga wapo tayari maongezi hayo yafanyike mbele ya TRA na Mamlaka za Usalama kuhusu MADENI ilikumbukumbu zikae sawa.

NB: hatuchezi
.......# b[OCTOBERTUNATICK]
View attachment 3364441

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Weka hivyo vielelezo tuvione,acha porojo
 
spana zote zinazotolewa na YANGA zinafanya/zitafanya kazi,kuwa na subira ila uwe na akili timamu kuelewa zinafanyaje/zitafanyaje kazi
Spana ilitolewa moja tu mechi ikaahirishwa. Hiyo ndiyo spana. Sasa kila nusu saa kuna press release mpya, ni spana au mazungumzo? 😂
 
Spana ilitolewa moja tu mechi ikaahirishwa. Hiyo ndiyo spana. Sasa kila nusu saa kuna press release mpya, ni spana au mazungumzo? 😂
huoni swala la madai limeibua baadhi ya marefa kutolipwa stahiki zao
 
Kwahiyo ni Ile ukimwaga ugali mie namwaga mboga na kizima moto na kiberiti kabisa .
 
Hivi Tanzania hamnaga issue muhimu ya kujadili zaidi ya mpira wa Simba na Yanga, nani karoga hi nchi? Ni akili duni elimu duni umasikini ushamba au ujinga.
Ponjoro leo kasema anataka plate number mpya ,
Sasa kama ponjoro kawaza hivyo, kwanini nisiwaze invoice za Yanga?
 
Back
Top Bottom