Mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa kushirikiana na shirika la umeme nchini Tanesco, kesho tarehe 20 wataanza kulipisha kodi za nyumba kwa mfumo wa luku
Kwanza ninahakika, hili limekuja baada ya serikali kukosa namna ya kuwabana wamiliki wa majengo ili kuyalipia
Na pia ninahakika, Sheria waliyokuwa wameitunga kwa ajili wamiliki wa majengo kulipia majengo yao, inaipa ugumu serikali kuwabana wamiliki hao kwa sababu wengi wa wamiliki wa majengo makubwa na yanayotakiwa kulipiwa kodi kubwa, ni haohao walioko serikalini
Ninayohakika pia kwamba, hata ukifuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya majengo, utawakuta ni viongozi wa serikali wenye majengo mengi na makubwa yanayolipiwa kodi kubwa
Sasa basi, Serikali inapokuja na mfumo huu mpya wa kila luku itumike kulipia kodi ya jengo, ninahakika kuwa, huu ni mpango wa kinyonyaji na wizi wa wawazi kwa wasio wamiliki wa majengo hayo yaani kodi hii maana yake imeelekezwa kwa walala hoi tena bila huruma
Kwa sababu hiyo, Serikali kupitia TRA na Tanesco, Je wanajua kuwa jengo moja linaweza kuwa na mita no zaidi ya 10?
Je, katika kulipia Jengo moja lenye mita zaidi ya 1, Serikali inaweka mfumo gani kwa nyumba zenye mita zaidi ya moja? au kila mita inahesabika na Jengo lake?
Kama itakuwa kila mita inahesabika iko kwenye jengo linalojitegemea! basi huu utakuwa ni wizi wa Serikali kwa wananchi wake!