Hili limeishatolewa ufafanuzi kama nyumba moja,kila chumba kina MITA yake,hapo mwenye nyumba inabidi atoe taarifa ni MITA ipi inalipia Kodi ya jengo,kama kiwanja kimoja kina nyumba zaidi ya moja,na kila nyumba ina MITA,MITA zote lazima zilipe Kodi ya jengo,hata kabla ya huu utaratibu kuja,ilikuwa hivyo,unalipa Kodi ya jengo kwa kila jengo lililopo kwenye kiwanja.
Nyumba ya kawaida Kodi yake ni 12000 kwa mwaka,unakatwa 1000 kila mwezi,ukikaa miezi miwili au zaidi bila kununua LuKu,siku ukinunua,unakatwa malipo yote ya miezi ambayo ukufanya manunuzi ya LuKu,hakuna wizi wapo,