TRA na thamani ya magari

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
1,334
Reaction score
1,466
TRA kwenye calculation tool yao tayari wameweka thamani ya magari na kukokotoa kodi kutumia thamani yao wakitumia mwaka wa gari, CC na aina ya gari tu.

Je, hii ni sahihi? na kama thamani halisi ya chombo husika sio kama TRA walivyoweka kwenye historia ya bei na ukokotuaji wao nini hutukeo?

Naomba kuwasilisha
 
Na kuna wakati wanatoza kodi kubwa kuliko hiyo inayoonekana kwenye calculator yao. wizi kila kona
 
wameamua kufanya hivyo baada ya kupitia changamoto nyingi sana ujanja ujanja na udanganyifu wa waafrica..

na hii sio tanzania tu hata kenya,uganda, rwanda nao wanafanya hivyo...

mtu gari unanua dola 100 unadanganya umenunua dola 10... so kuepusha shari wameweka bei zao wenyewe
 
Sasa huoni hapo kuna shida au unakubali na hiyo hali kisa Kenya na Uganda wanafanya ?

Je hii haiwezi kuwa ndio sababu ya kuwa na ushawishi wa rushwa na ulaghai???
 
Sasa huoni hapo kuna shida au unakubali na hiyo hali kisa Kenya na Uganda wanafanya ?

Je hii haiwezi kuwa ndio sababu ya kuwa na ushawishi wa rushwa na ulaghai???

rushwa ya nini? hii style mtoa rushwa na asiyetoa rushwa kodi analipa sawa sawa.. sababu system ina calculate kodi kwa kufuata bei iliyowekwa.. afisa wa tra hana ruhusa ya kubadili chochote..

hii ndio njia ya kuepusha double standards... na ndio imepunguza rushwa na udanganyifu
 
Nilinunua SUV kutoka kampuni moja ya magari hapa tz kwa u.s dollas 3300 roughly hivi.. Kodi nikatozwa 10 mil. Na zaidi..

Nikasema labda kwakuwa ni ya 1997. Cc zake sio kubwa sana cc 1900.
 
Nilinunua SUV kutoka kampuni moja ya magari hapa tz kwa u.s dollas 3300 roughly hivi.. Kodi nikatozwa 10 mil. Na zaidi..

Nikasema labda kwakuwa ni ya 1997. Cc zake sio kubwa sana cc 1900.

Hongera kwa kumiliki SUV
 
Sasa huoni hapo kuna shida au unakubali na hiyo hali kisa Kenya na Uganda wanafanya ?

Je hii haiwezi kuwa ndio sababu ya kuwa na ushawishi wa rushwa na ulaghai???
Usikariri sio kitu ni rushwa TRA wanashauri kabla hujanunua gari nje ni lazima uangalie kodi utakayolipa, kwa hiyo wewe kama umeona kodi ni milion labda 5 alafu ukapewa bei kubwa unahaki ya kuikataa kwenye IQS. Kwa hyo acha kupotosha rushwa inakujaje hapo??
 
Bila shaka unawakilisha kitengo
 
Mkuu......mambo yanapigwa sana mbona.......hii nchi bado sanaaaaaaaaaaaaa.......kumaliza rushwa...........wewe jua tu hivyo........
 
Na kuna wakati wanatoza kodi kubwa kuliko hiyo inayoonekana kwenye calculator yao. wizi kila kona

mkuu......hii kitu nadhani ipo hivi.......

tuseme tra CIF yao inasema mwaka fulani.....cc kadhaa.....gari aina hii......na bla bla kibao ni $ 2300......kodi itakuwa 2,500,000..........wewe gari hilo hilo.......likaja CIF $ 3000.......hapo wanachokifanya ni kukukadiria juu ya CIF yao.........au gari hilo hilo........likawa CIF mpaka hapa ni $ 1200.......wanachokifanya ni kuiuplift ikaribiane na yao.......

hivyo ndivyo nilivyowaza labda ndicho wanachofanya...........
 
Mkuu......mambo yanapigwa sana mbona.......hii nchi bado sanaaaaaaaaaaaaa.......kumaliza rushwa...........wewe jua tu hivyo........

Mimi nasema mwanya wa rushwa kwenye magari ni mdogo sana na labda wewe mteja uwe unalazimishwa uliwe rushwa lakini kama unaamua usimamie gari yako inatoka bila rushwa
 
Ni sawa kabisa
 
Mimi nasema mwanya wa rushwa kwenye magari ni mdogo sana na labda wewe mteja uwe unalazimishwa uliwe rushwa lakini kama unaamua usimamie gari yako inatoka bila rushwa

Rushwa mara nyingi inazaliwa hapo kwenye makadirio.......hasa ya juu........
 
Mbona kodi nikubwa kuliko manunuzi?

Mkuu makadirio ya kodi kwa upande wa magari ulianzia mbali sana, mwanzoni walikuwa wanakadiria kwa ku-base kwenye mileage ilikuwa kama factor kubwa, ilileta shida na malalamiko yasiyo ya msingi, baadae wakahamia kwenye cif za gari za mteja...hapa pia ulikuwa uchochoro maana watu walikuwa wanadai kwamba wengine wamepewa magari na ndugu zao sasa utamtozaje kodi mtu aliyepewa gari buree...sasa baadae TRA ikaja na huo mfumo wa Bei ya gari likiwa jipya toa uchakavu ndio unapata thamani ya gari ambao kwa kiasi fulani umekuwa fair kwa watu wote ukiondoa hayo malalamiko ya kodi kuwa kubwa nadhan watu wa sera ndio wanamajibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…