Sio kila mmoja wetu anaweza kuzungumzia kodi kisa tu amepata TECNO yake Phantom au ITEL au INFINIX.
Kodi ya Zuio inalipwa na mmiliki halisi wa JENGO/FRAME/STORE yako.
Kwakuwa umelipa pango kwa mwenye Frame, hapa maana yake ni kwamba mwenye Frams ameingiza kipato hivyo ana wajibu wa kulipa kodi. So kutokana na urahisi wa Mfanyabiashara kwenda TRA basi sheria ikamtaka kuzuia 10% ya Pango aliyopaswa kumlipa mwenye frame na kuiwasilisha TRA kwa niaba ya MMILIKI.
Kama frame ni yako, basi utapeleka uthibitisho wa umiliki huo ikiwa sambamba na hati ya jengo hilo au kama imesajiliwa kwenye mfumo wa majengo wa TRA basi unasema na hukatwi kodi hiyo.
Ndugu zangu, kama hamjui kitu ni bora kumtafuta jirani yako akupe elimu sahihi, au anzisha uzi ambao utakufanya ueleweshwe na sio unafungua uzi as if unauelewa na unachokisema kumbe ni BOGAZ SIMAMA TUOMBE.