TRA ondoeni Kodi ya Pango kwa mfanyabiashara

Wewe ndiyo bogasi, kwann wenywewe Tra wasiweke mfumo wakudai Kodi kwa mwenye frem wambane MFANYABIASHARA,
Alaf mwenye nyumba Gani atakubali kukurudishia
TRA inapaswa kuweka mfumo yenyewe ya kudai hii Kodi kwa mwenye nyumba!
Pia hv zile pesa zinakatwa kwny luku huwa ni za nn vile?.....
 
Hyo bila shaka ni Chawa wa TRA .....moja ya wasababishi wa mgomo kariakoo....wanajfanya wanajua kumbe wapuuz fulan....
 
Yaan wee acha,
Ukiwa na mtaji mdogo m10 kwenda chini ukataka tin esabu siku tu!
Ukiritimba mkubwa sana unatuumiza! Unakuja kusumbuliwa na mtu ambae tangu ametoka kwao, mateso aliyoyapata ni kukaa hostel[emoji23][emoji2960] baada ya hapo kapata kazi ya connection, alafu anaokuja kupambana nao hawajawahi kufika popote na wana mafanikio kuliko yeye anaekinga mshahara [emoji2959][emoji2959][emoji2959]
 
TRA wanatakiwa wamjue mmiliki, as long as jengo linatambulika kama jengo la biashara. Kama hawawezi maana yake huo ni udhaifu wanaotakiwa kuurekebisha badala ya kumtwika mzigo mpagaji.

Mimi nimlipie kodi mmiliki kisha nikamdai yeye, wewe unaona kuna logic hapo? Kila mmoja alipe kodi inayomhusu sio maswala ya kulipiana.
 

Kwa hiyo nimeshamlipa mtu kodi amenipa mkataba niende nikamdai Kodi ya Pango?

Does it make any sense to you?
 
Pia hv zile pesa zinakatwa kwny luku huwa ni za nn vile?.....
PROPERTY TAX... Ile ni kodi ya MAJENGO. Kodi hii haina uhusiano na biashara, iwe nyumba ya makazi, biashara, Store, kiwanda au chochote italipwa tu.

Nyumba za kawaida ni 12000 kwa mwaka (1000 kwa mwezi)

Na zile za Ghorofa ni 60000 kwa floor moja (5000 kwa mwezi kwa kila floor)

Hizi kodi hazi uhusiano wowote.

Hii ya PANGO unatozwa kwa kuwa umepangisha hivyo umefanya biashara.

Kama Frame ipo kwenye nyumba yako mwenyewe, basi hukatwi hulipi kodi hii. Kwa maana umetumia jengo lako mwenyewe.
 
Kwa hiyo nimeshamlipa mtu kodi amenipa mkataba niende nikamdai Kodi ya Pango?

Does it make any sense to you?
Yes it make. Usichoelewa ni kwamba, Before kumlipa unapaswa uikate kabisa, hawezi kukataa na hiyo ndio sheria.

Umekaza ubongo tu, ni logic simple sana hii.

Fikiria Umechukua fedha, umempa mwenye frame, then mwenye frame aende TRA akalipe 10% ya fedha hiyo. Huoni umeweka mlolongo mrefu wa kikodi?

Moja ya kanuni ya kodi ni kutokuwa na mlolongo mrefu wa ulipaji wake.

Hivyo wewe unayelipia frame, kwa namna yoyote utaenda TRA kwa ajili ya makadirio ya kodi ya biashara yako, hapo sasa ndipo unabeba na pesa ya 10% ya pango ulimkata mmiliki wa frams ile ili kupunguza mlolongo usio na ulazima.
 
Wewe humlipii, analipa yeye. Wewe ni kama mjumbe au agent tu wa serikali kama ilivyo kwa VAT, mfanyabiashara sio yeye anayelipa kodi hiyo.

Fedha yake ya kodi ww unaikata 10% kisha unapeleka TRA kwa niaba yake kama kodi kutokana na kipato alichopata mara baada ya kukupangisha wewe.
 
Tafuta frem kwanza ndiyo uje uropoke hapa
 
Of course unavyosema ni sahihi, in short TRA wanakwepa majukumu yao.

Hapa kuna tofauti kubwa sana kwa wale wanaofananisha PAYEE na huo upuuzi.

Kwenye PAYEE Boss/muajiri anamkata mtumishi wake.
Lakini kwenye hiyo kodi ya TRA ni sawa na mtumishi kumkata Boss wake/Mwenye maamuzi juu yake, muda wowote inaweza kuvuruga maafikiano kati ya mpangaji na mmiliki
 
Kata kwenye PANGO usichoelewa nini? Kama pango kwa mwezi ni 1 Milion basi 100k unapelekea TRA na 900k unampa mwenye fremu hapo shida hiyo ndio maana ya WITHHOLDING TAX
Nina hakika huna frem ya biashara ndio maana unarahisisha mambo hivi kama watunga sheria wanavyo rahisisha. Hakuna mwenye frem anaekubali zaidi kama unataka kupandishiwa Kodi na wengine kabla hujaingia anakwambia kabisaa TRA utajua mwenyewe.

Hiyo sheria mngeangalia namna ya kumkata mwenye nyumba Moja kwa Moja Ila kwa hiyo sheria yenu ya sasa mnawaumiza tu wafanyabiashara
 
Halafu Lameck Madelu anasema ni mchumi namba moja daraja la kwanza Phd Holder!

"Serikali corrupt haikusanyi kodi ,itabaki kukimbiza na wamachinga na mama ntilie" - Nyerer 1922-1999
 
Msitake urahis wa kupata kodi zenu kwa kumuumiza asiyehusika,mfateni mwenye jengo na siyo kumbana mfanyabiashara

Kwann wenye majengo mnawaogopa au ni baba zenu
 
Unavyoongea kama ni rahis vile,nyie watoto wa kishua ni tatzo,yaan umetoka shule moja kwa moja ukaingia ofisini hujui hata wanaume huko mtaani wanapambanaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…