TRA Pwani wanarudisha nyuma juhudi za Rais Magufuli

TRA Pwani wanarudisha nyuma juhudi za Rais Magufuli

Prisoner 46664

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2010
Posts
1,948
Reaction score
1,238
Wale walioko kwenye sekta za usafirishaji, uchimbaji wa malighafi ujenzi na ujenzi kwa ujumla watakuwa wamegundua kuwepo kwa uhaba wa ghafla wa mchanga unaotumika kujengea hivi Karibuni maeneo ya Dar na sehemu jirani. Kwa kipindi cha kama wiki moja hivi, TRA Pwani imekuwa ikikamata magari yote ya mchanga yasiyokuwa na mashine za kielektroniki za risiti (EFD). Hii imesababisha magari yote yanayobeba mchanga kutoka machimbo ya msangani Kibaha kwa Mathias kujificha na kushindwa kuendelea kusambaza bidhaa hii iliyo chachu kubwa ya kuendeleza shughuli mbali mbali za ujenzi kama ambavyo imekuwa kwa kipindi chote cha serikali ya awamu ya tano ya Mhe. John Pombe Magufuli.

Wakati tukiunga mkono juhudi za mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) za kupanua wigo wa kodi, ni lazima mabadiliko yanayofanywa yawe shirikishi, yenye tathmini pana juu ya uchumi na pia yafanywe kimkakati kuhakikisha wadau/walipakodi wanaelewa malengo na mabadiliko tajwa na kuyaunga mkono ili yafanikiwe. Mfano kwenye sakata hili, TRA wangeweza kuwadhamini wamiliki wa magari waweze kupata mashine na kuendelea kukatwa fedha za kulipia mashine kidogo kidogo. Mpaka ninapoandika uzi huu, hakuna wamiliki wa magari waliokwisha kufanikiwa kupata mashine hizo na hivyo kupelekea shughuli za uchimbaji na usafirishaji mchanga sambamba na zile za ujenzi kusimama kwa muda.

Athari za harakaharaka zinazotokana na maamuzi haya ya TRA ni pamoja na kukosa mapato kwa muda kwa wafuatao;

1. Madereva wa malori
2. Wamiliki wa malori
3. Wafanyakazi wa machimbo
4. Wafanyakazi wa sekta ya ujenzi
5. Halmashauri (Tozo za maliasili zinazotozwa kwenye malighafi ujenzi)

Hili linalotokea linanikumbusha walichofanya TRA Morogoro mwanzoni mwa mwaka huu ambapo waliwaagiza vijana waliokuwa wanauza mishkaki kama ya Coco pale Nyumbani Park (Samaki Morogoro) watafute mashine za kielektroniki baada ya kuona wanauza sana. Matokeo yake vijana wale walilazimika kupandisha bei ya mishkaki toka shillingi 300 mpaka 500. Wateja nao wakashindwa kumudu bei mpya na hatimae vijana wakalazimika kufunga biashara. Hii ilinisikitisha sana na inaonesha namna ambavyo maaumuzi yanayohusiana na kodi yanavyotakiwa kufanywa kimkakati na kwa kuzingatia tija.

Tunashauri TRA Pwani wachukue hatua za haraka za kuondoa changamoto hii kuzuia athari kubwa inayokaribia kuukumba uchumi mpana wa sekta ya ujenzi.
 
TRA ubunifu sijui ndio umefika ukomo, instead ya kutengeneza mazingira mazuri kwa walipa kodi, wao wanataka kukomoa......inamaana sasa hivi hata kile kidogo ambacho walikua wanapata hawatopata tena.
 
Kwa mujibu wa sheria za ukusanyaji mapato inayosimamiwa na TRA ni kwamba kama unabiashara yeyote ambayo mauzo yake kwa siku ni zaidi ya Tsh 45000/= ni lazima uwe na mashine ya kielekitroniki ya utoaji risiti (EFD)

Mkuu waambie hao wabeba mchanga walipe kodi waache janja janja
 
Wauza mishikaki morogoro Tra walienda mbali sana au kupitiwa wakasahau kuwa vitambulisho vya machinga ndivyo vinavyowafanya walalahoi wote wajione biashara za Mia tatu tatu hasistahili kulipa kodi.?
 
Kwa mujibu wa sheria za ukusanyaji mapato inayosimamiwa na TRA ni kwamba kama unabiashara yeyote ambayo mauzo yake kwa siku ni zaidi ya Tsh 45000/= ni lazima uwe na mashine ya kielekitroniki ya utoaji risiti (EFD)

Mkuu waambie hao wabeba mchanga walipe kodi waache janja janja

Mashine ya EFD ni bei gani?
Tuanzie hapo.
 
Huu mkoa sijui una nuksi gani km hatukuwahi kumtoa Rais wa nchi. Hivi ile barabara ya Mlandizi Bagamoyo imewakosea nini halafu hivi kuna mbunge kweli huko Bagamoyo sijawahi hata kumsikia
 
Kwa mujibu wa sheria za ukusanyaji mapato inayosimamiwa na TRA ni kwamba kama unabiashara yeyote ambayo mauzo yake kwa siku ni zaidi ya Tsh 45000/= ni lazima uwe na mashine ya kielekitroniki ya utoaji risiti (EFD)

Mkuu waambie hao wabeba mchanga walipe kodi waache janja janja

Mkuu sisi wote tunaunga mkono hili kwa sababu linasaidia sana kuongeza uwazi na utii kwenye kulipa kodi. Tatizo hapa ni namna ya utekelezaji wa mabadiliko haya. Ninadhani busara, elimu na “phasing” approach vinahitajika la sivyo kinachoathirika ni uchumi wetu..sidhani kama hii ndiyo njia sahihi ya kuuendesha uchumi wa Kati.
 
Kwa mujibu wa sheria za ukusanyaji mapato inayosimamiwa na TRA ni kwamba kama unabiashara yeyote ambayo mauzo yake kwa siku ni zaidi ya Tsh 45000/= ni lazima uwe na mashine ya kielekitroniki ya utoaji risiti (EFD)

Mkuu waambie hao wabeba mchanga walipe kodi waache janja janja
Hiyo ni elfu arobaini na tano au ni laki nne na nusu
 
Walau tzs 690,000/- ninaamini..ni ngumu sana kwa mfanyabiashara wa kawaida kuimudu hii kwa haraka
Na ndiyo maana sheria imetambua kila anaye uza kwa siku zaidi ya ELFU AROBAINI NA TANO (45,OOO/=)inapaswa awe na mashine kwa maana haiwezi kumshinda kununua,na pia wenye mitaji kuanzia milioni 4 na kuendelea inapaswa wawe na mashine
 
Back
Top Bottom