TRA: Taarifa kuhusu madai ya Diamond Platnumz

Dah we jamaa mshamba kweli yani kujibiwa na TRA unaona kwako ni heshima .
Ni heshima na ukitaka kujua ni heshima sio kila mtu huwa anajibiwa na TRA umeona Pck pamoja na malalamiko yake yote aliyotoa Tena katoa kabla ya diamond lakini diamond ndio kaja kujibiwa
 
Mwambieni huyo Diamond alipe kodi anayotakiwa kulipa huko TRA. Aache ujanja ujanja wa kutaka kukwepa, kisa tu ni kada wa ccm, na pia mpiga kampeni wao wakati wa uchaguzi.
 
 
Ndg kuongoza Nchi ni shughuli pevu sana. Bila kuwa kauzu lazima upoteane,ni swala la muda tu wafanyabiashara wana mbinu nyingi sana za kukwepa kodi. Ukiwachekea unapoteana
Kwanini Unawaza tu kila mfanyabiashara ni mkwepa kodi?
 
Naona TRA mmeanza kufungia tena account za Wafanyabiashara ila jueni tu principles ni kutoa hizo pesa kwenye account tunaanza ku operate manually.

Hatuwezi kuwa victim of poor thinking personnel, watanzania tunakabiliana na matatizo mengi sana yanayosababishwa na hawa Hawa maafisa so jueni kuwa mkiamua hili na sisi tunaamua vinginevyo mpaka mtakapotuliza akili na kujua namna ya kwenda sawa na watanzania
 
 
Inatakiwa mtu aitwe haojiwe siyo unafunguka account hata mhusika hajui kwanini account yake imefungwa.
Hii nchi ngumu sana kuishi. Fuatane sheria
Ni kama kuweka kufuli la pili kwenye nyumba ya mtu yeye akiwa hayupo, anarudi usiku anakuta kufuli mlangoni anakosa kwa kulala, je hiyo hasara ya kulala guest house atalipa nani
 
KWA NINI MSITAFUTE MAZUNGUMZO NA MTU KABL HAMJAENDA KUMVAMIA AUKUVAMIA AKAUNTI ZAKE ? WHY MNAENDESHA MAMBO KIKABURU ? NYIE NI WATANZANIA MNAFANYA KAZI NA WATANZANIA MSISAHAU HILO

View attachment 2464144
Kabla ya account kufungiwa ametumiwa notifications mara kadhaa amepuuza.
Ana makosa ya kukwepa kodi.
Lipa kodi kwa maendeleo ya taifa.
 
Uwezo wako wa kufikiri upo chini sana, ongeza bidii ya ulaji wa samaki.
Ila tusiwe wanafki swala lakodi wafanya biashara wengi wanalikwepa mukumbuke kipindi jpm anaingia kwa madaraka company nyingi zilikutwa azilipi kod ilipelekea company nyingi kufungwa na watu kupoteza hajira [emoji117] lakin waliokuwa wanalipa kodi bila kushurutishwa maisha hayakua magumu mfano ofisin yetu aijakutwa na seckendo yoyote ila jiran yetu alipata tabu sana ,shda kubwa munaleta ushabik pia ktk mambo ya seriouse .
 
Yap, hapo ukiweka CPF na RDL ndio inakaribia kwenye hiyo 50% anayosema na kulalama wakati ndio kitu halisi hicho.

My point ni kwamba, huyo diamond asije kutumia hao chawa wake na ku endelea kupiga kelele kwenye media kama mwehu. Amalizane na TRA huko huko walikokutania.

Kutaka huruma Kwa wananchi haisaidii na kutumia media zake ajue ni treason.. Hawwezi kupambana na Mamlaka na asijaribu kuaminisha umma kwamba Mamlaka inamletea uonevu.

Na ajifunze Sasa kutunza hesabu zake vizuri na kuajiri watunza vitabu na kumbukumbu za akaunti Kwa usahihi na Kwa weledi. Akicheza watamfilisi akiona..

Sheria haitaki huruma huruma na kulia lia.. Apambane kiume... Raha sana kupitisha vibunda vya Watu ila sasaaaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…