Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nimesikiliza viongozi wa serikali wakiongeoa kwenye msiba wa anayedaiwa kuwa mtumishi wa TRA aliyefariki katika tukio lililohusishwa na utekaji. Viongozi walijikita kuongelea yaliyotokea hapo kwenye hilo tukio tu, hawakuzungumzia mazingira gani yaliyosababisha.
Pia ilikuwa ni wakati mzuri wa kuonyesha jinsi gani watazuia hayo yasitokee tena, kwa bahati mbaya mkuu wa mkoa wa Dar, Chalamila kama kawaida yake aliishia kutoa vitisho zaidi akijionyesha kuwa yeye ni mwamba, dola inatakiwa kuogopwa, mtu aliyepiga kelele kutekwa anashughulikiwa na eneo tukio lililotokea litasafishwa.
Ushauri wangu kwa serikali na TRA ni kwamba sasa katika elimu mnayotoa muwafundishe raia pia jinsi ya utaratibu wa kisheria wa kukamatwa wao binafsi au mali zao na mfanyakazi wa TRA.
Wafanyakazi wa TRA wanaoenda kukamata watu au mali wavae sare(uniforms) rasmi wakiwa na vitambulisho vyao.
Magari ya TRA yawe na namba zake rasmi za utambulisho kuepusha taharuki na mikanganyiko isiyo ya lazima.