TRA toeni elimu ya ukamataji na watumishi wenu wavae sare maalum ili kuepusha taharuki mkiwa mnakamata raia na mali zao

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Nimesikiliza viongozi wa serikali wakiongeoa kwenye msiba wa anayedaiwa kuwa mtumishi wa TRA aliyefariki katika tukio lililohusishwa na utekaji. Viongozi walijikita kuongelea yaliyotokea hapo kwenye hilo tukio tu, hawakuzungumzia mazingira gani yaliyosababisha.

Pia ilikuwa ni wakati mzuri wa kuonyesha jinsi gani watazuia hayo yasitokee tena, kwa bahati mbaya mkuu wa mkoa wa Dar, Chalamila kama kawaida yake aliishia kutoa vitisho zaidi akijionyesha kuwa yeye ni mwamba, dola inatakiwa kuogopwa, mtu aliyepiga kelele kutekwa anashughulikiwa na eneo tukio lililotokea litasafishwa.

Ushauri wangu kwa serikali na TRA ni kwamba sasa katika elimu mnayotoa muwafundishe raia pia jinsi ya utaratibu wa kisheria wa kukamatwa wao binafsi au mali zao na mfanyakazi wa TRA.

Wafanyakazi wa TRA wanaoenda kukamata watu au mali wavae sare(uniforms) rasmi wakiwa na vitambulisho vyao.

Magari ya TRA yawe na namba zake rasmi za utambulisho kuepusha taharuki na mikanganyiko isiyo ya lazima.
 
Acha wapigwe tu. Tatizo la hii nchi ni kwamba CCM imelea tabia ya kila mtu nchini kuwa na mentality ya "unajua mimi nani", TISS, TRA, Polisi, mawaziri, Makatibu wakuu, nk. Angalia jinsi barabarani gari zenye vimulimuli vya bluu zinavoongezeka kila siku wakitaka kuonyesha "mnajua mimi nani". Juzi hapa huko Iringa hii tabia hadi imezua ugomvi kati ya Polisi na Magereza. Kwa hiyo nao waache wajue wananchi wenye hasira ni nani.
 
Nimesikiliza viongozi wa serikali wakiongeoa kwenye msiba wa anayedaiwa kuwa mtumishi wa TRA aliyefariki katika tukio lililohusishwa na utekaji. Viongozi walijikita kuongelea yaliyotokea hapo kwenye hilo tukio tu, hawakuzungumzia mazingira gani yaliyosababisha.

Pia ilikuwa ni wakati mzuri wa kuonyesha jinsi gani watazuia hayo yasitokee tena, kwa bahati mbaya mkuu wa mkoa wa Dar, Chalamila kama kawaida yake aliishia kutoa vitisho zaidi akijionyesha kuwa yeye ni mwamba, dola inatakiwa kuogopwa, mtu aliyepiga kelele kutekwa anashughulikiwa na eneo tukio lililotokea litasafishwa.

Ushauri wangu kwa serikali na TRA ni kwamba sasa katika elimu mnayotoa muwafundishe raia pia jinsi ya utaratibu wa kisheria wa kukamatwa wao binafsi au mali zao na mfanyakazi wa TRA.

Wafanyakazi wa TRA wanaoenda kukamata watu au mali wavae sare(uniforms) rasmi wakiwa na vitambulisho vyao.

Magari ya TRA yawe na namba zake rasmi za utambulisho kuepusha taharuki na mikanganyiko isiyo ya lazima.
Kwanza nianzne kwa kutoa pole kwa wale wote waliopoteza ndugu na jamaa zao kutokana na kuuliwa. Niungane nawe eneo moja la elimu izidi kutolewa mara kwa mara .
Labda swali langu moja hapa ni kuwa nimeangalia ile gari ilikuwa na namba za serikali na ikanishangaza watu ambao wangekwenda kwa nia mbaya na gari lenye namba za serikali? maana taarifa za nyuma tumesikia na kuona picha gari kama ile Toyota Raum. Pili magendo siyo tu hapa Tanzania hata kwengine kote ni kazi ngumu sana kuzuia. Wito tra wawapitishe watumishi wao kwenye mafunzo maalum na zana za kufanyia kazi. Hofu kama magendo ni kuwavizia wapitishaji je wakiwa na gari zinazojulikana wataweza fanikiwa wapata hao wanaopitisha? Mfano ukiwa wewe ndiyo mtu wa magendo halafu unaliona gari linalozuia magendo eneo lako utapitisha muda huo au utasubiri mpaka waondoke? pia nimeona wengi wakiuliza muda waliokuwa wakifanya doria huo muda unaonekana ndiyo muda ambao magendo yanapita.
Ni wazo zuri sana la elimu kuhusu magendo ikaendelea tolewa ila na sisi wananchi tuwe tayari kuiskia maana kuna baadhi huwa tunakejeli acha tra watupe elimu na tuwe wepesi kuifahamu ili kuepuka mengi tu .
 
Mamlaka wanajua ni nini hasa kimewatokea wale ndugu zetu waliouawa na pia wanajua hofu iliyomo ndani ya Watanzania. Pole kwa wafiwa na familia zao hawakupaswa kufa kwa style ile, ila mamlaka zikae zikujua bila kurejesha hali ya kua na imani nazo haya mambo yatazidi kutokea na huwezi kuwalaumu wananchi.​
 
Wanachukua rushwa magari yanapita bandarini hapo harafu wao wenyewe wanakuja kukamata badala ya kutengeneza mazingira ya mizigo ipite kwa kulipiwa kodi mnasema watengeneze sare hata hao watekaji watatengeneza sare za TRA kama kawaida..
 
Kiongozi magendo ninavyojua mimi hayapiti bandarini temeblea mwambao wa bahari nchi yetu inaeneo kubwa sana watu wanatumia kama chaka kupitisha magendo. na wengi wanavizia usiku kwa kujua si rahisi kuonekana.
 
Mwaisengela amka ndugu yangu magendo yanapita sehemu nyingi na sehemu zingine za wazi hizo hizo ambazo unadhani zina usalama..
 
da hatari sana na huwa hatujui tu haya madude kama yapo sawa kwa nini wanapitisha huku uchochoroni? tusije letewa mavitu yame expire au madude ya p diddy na mbaya zaidi hata silaha zikapita kinyemela. Nadhani muhimu serikali ikaliangalia hili suala la magendo kwa jicho la karibu. Kuwe na timu maalum kama ilivyo Zanzibar .
 
Nimesikiliza viongozi wa serikali wakiongeoa kwenye msiba wa anayedaiwa kuwa mtumishi wa TRA aliyefariki katika tukio lililohusishwa na utekaji. Viongozi walijikita kuongelea yaliyotokea hapo kwenye hilo tukio tu, hawakuzungumzia mazingira gani yaliyosababisha.

Pia ilikuwa ni wakati mzuri wa kuonyesha jinsi gani watazuia hayo yasitokee tena, kwa bahati mbaya mkuu wa mkoa wa Dar, Chalamila kama kawaida yake aliishia kutoa vitisho zaidi akijionyesha kuwa yeye ni mwamba, dola inatakiwa kuogopwa, mtu aliyepiga kelele kutekwa anashughulikiwa na eneo tukio lililotokea litasafishwa.

Ushauri wangu kwa serikali na TRA ni kwamba sasa katika elimu mnayotoa muwafundishe raia pia jinsi ya utaratibu wa kisheria wa kukamatwa wao binafsi au mali zao na mfanyakazi wa TRA.

Wafanyakazi wa TRA wanaoenda kukamata watu au mali wavae sare(uniforms) rasmi wakiwa na vitambulisho vyao.

Magari ya TRA yawe na namba zake rasmi za utambulisho kuepusha taharuki na mikanganyiko isiyo ya lazima.
Ukamataji wanTRA usiruhusi maafisa wa TRA kufukuza magari kwa Namna ya mashindano, ni Bora kutumia vizuizi rasmi. Mkiwa mnafukuza Gari ya MTU ni rahisi MTU kuhisi anafukuzwa Na watekaji
 
Kwanza nianzne kwa kutoa pole kwa wale wote waliopoteza ndugu na jamaa zao kutokana na kuuliwa. Niungane nawe eneo moja la elimu izidi kutolewa mara kwa mara .
Labda swali langu moja hapa ni kuwa nimeangalia ile gari ilikuwa na namba za serikali na ikanishangaza watu ambao wangekwenda kwa nia mbaya na gari lenye namba za serikali? maana taarifa za nyuma tumesikia na kuona picha gari kama ile Toyota Raum. Pili magendo siyo tu hapa Tanzania hata kwengine kote ni kazi ngumu sana kuzuia. Wito tra wawapitishe watumishi wao kwenye mafunzo maalum na zana za kufanyia kazi. Hofu kama magendo ni kuwavizia wapitishaji je wakiwa na gari zinazojulikana wataweza fanikiwa wapata hao wanaopitisha? Mfano ukiwa wewe ndiyo mtu wa magendo halafu unaliona gari linalozuia magendo eneo lako utapitisha muda huo au utasubiri mpaka waondoke? pia nimeona wengi wakiuliza muda waliokuwa wakifanya doria huo muda unaonekana ndiyo muda ambao magendo yanapita.
Ni wazo zuri sana la elimu kuhusu magendo ikaendelea tolewa ila na sisi wananchi tuwe tayari kuiskia maana kuna baadhi huwa tunakejeli acha tra watupe elimu na tuwe wepesi kuifahamu ili kuepuka mengi tu .
Magendo yanafikaje Dar es Salaam??
 
TRA nao waweke hadharani "PGO " yao inayohusu ukamataji wao ili wananchi tuijue. Vinginevyo yaliyotokea yanaweza kujirudia na yamkini yakawa ni makubwa zaidi.
 
Wanachukua rushwa magari yanapita bandarini hapo harafu wao wenyewe wanakuja kukamata badala ya kutengeneza mazingira ya mizigo ipite kwa kulipiwa kodi mnasema watengeneze sare hata hao watekaji watatengeneza sare za TRA kama kawaida..
"hata hao watekaji watatengeneza sare za TRA kama kawaida,"
 
Back
Top Bottom