TRA-tozo mpya za parcel zinazo pitia posta ziangiliwe upya

yani kodi ipo sawa na bei ya bidhaa basi lengo lake ni kukatisha tamaa kuingiza vitu toka nje.
 
Wazalendo husema lipa kodi kwa manufaa ya nchi !
 
Daah kuna gauni la mwanamke wangu nimeagiza kwa $8 sijui watanitoza bei gani?.. ila nataka nikakomae nao kwa hoja.. endapo watanipa hiyo bili ya kulipa 27,000 watanieleza vizuri kwa kweli kwenye maandishi
 
Safi sana.., kujitetea hivi ndio tunatakiwa kufanya watanzania..
Sio kuwaacha watendaji wa serikali kufanyaa watakavyo..
Andaa ushahidi wako wa manunuzi ili uutumie kama ushahidi ktk kujitetea wakikuongozea makodi...
 
Kwa hali hiyo hata viwanda havitajengwa maana kama mtu kakaa pale posta kavaa tai na kuipatia kipato haram serikali yetu hapo sioni sababu ya serikali kiujenga kiwanda chochote wakati wanaweza kupata hela bila kuwekeza
 
Hili Shirika la Posta na TTCL kuna mchawi kajificha nyuma ya pazia.
Hadi aje kumulikwa kwa kung'olewa kidhalilishaji bila huruma.
Haya mashirika yalikuwa ni kimbilio sana siku za nyuma.
Lakini aliopoingia mchawi huduma zikawa za hovyo sana. Mfano huduma za posta za ems!
Mtu akitumiwa pesa, inachukua muda mrefu sana mhusika kufikiwa. Mpaka ikawa inadaiwa kuwa, wanajikopesha wao kwanza hela za watu, hadi wapate mishahara ndiyo wafidie, ems ikapoteza maana na kupelekea kufa kifo cha kawaida na kufanya miamala ya kampuni za simu za mkononi inawiri. Ems wamebakia na huduma za kusafirisha vishurushi kwa bei za ajabu ajabu.
Mfano, bahasha size ya A4, kwenye mabasi wanasafirisha kwa gharama ya sh.5,000/= tu, lakini wao ni Sh.12,000/=.
Tukija Ttcl, pamoja na ushindani mkubwa wa vyombo na bidhaa za mawasiliano ilivyo kubwa duniani kwa sasa, mhujumu mmoja akalazimisha mobile phone pamoja fwt zote ziwe za mtandao mmoja!
Maana yake alidhamiria kuua hilo shirika la umma ili kuwezesha kampuni binafsi ziweze kutawala, nadhani walikuwa na hisa kwenye kampuni hizo!
Tuseme tu kuwa, menejimenti yote hiyo ya posta na ttcl kuna vigogo wahujumu walioshika remote kuchezesha shirika watakavyo kwa ajili ya matumbo yao.
Afanye awezavyo, JPM amulike kurunzi yake na kisha ashushe rungu, ili mambo yaweze kukaa sawa.
 
Mkuu, una import viatu vya mtoto bado unajiita malala hoi???

Kama kiberiti kwa mangi kinalipiwa kodi basi hata wewe uki import flash disk basi utuchangie kodi
 
Safi sana.., kujitetea hivi ndio tunatakiwa kufanya watanzania..
Sio kuwaacha watendaji wa serikali kufanyaa watakavyo..
Andaa ushahidi wako wa manunuzi ili uutumie kama ushahidi ktk kujitetea wakikuongozea makodi...
Najua wanaweza kutumia ubabe kwa mwamvuli wa serikali ila ki vyovyote vile watakuwa wanakosea sana.. Haya mambo yana athiri kwa kiasi kikubwa sana uchumi wetu
 
Mkuu, una import viatu vya mtoto bado unajiita malala hoi???

Kama kiberiti kwa mangi kinalipiwa kodi basi hata wewe uki import flash disk basi utuchangie kodi
Muheshimiwa unaweza kuta kuna sale unanunua kitu kizuri $8 au $5 na shipping free pia vijana wengi walijiari kupitia eBay, Alibaba na masoko mengine mengine . Pia kuna black Friday kama jana unanunua vitu kwa nusu ya bei. Hamna ajira kwa sababu serikali haiwezi ajiri watu wote hata hizi loop hole ndogondogo mnakaba.

Kunafursa ya kodi mfano kurasimisha sekta ya usafiri mfano madereva na makonda wawe wanalipa kodi pia wapate bima za afya.

Vile madereva wa maroli na magari makubwa warasimishe haya makundi yana watu wengi let say walipe 10k kwa kichwa utajua kwa mwezi inaingia ngapi.

Wanao import wengi ni vijana wanaouza smartwatch , pendrive na external hdd ebu wasomi wakodi mrasimishe kwanza sekta kubwa ya usafirishaji itachangia zaidi kuliko na kudeal na mtu alienunua pendrive za 50k kwa $1 hadi $5
 
Mkuu, una import viatu vya mtoto bado unajiita malala hoi???

Kama kiberiti kwa mangi kinalipiwa kodi basi hata wewe uki import flash disk basi utuchangie kodi
Kwa mawazo ya watu kama wewe Tanzania yenye neema tusubir sana. Mtoa Uzi sidhan kama kuna sehemu amesema hataki kuchangia kodi. Yeye amelalamika kodi aliyokadiriwa kwa kulinganisha na bidhaa aliyoiimport.
 
Tatizo watu wengi hawafahamu kununua nje ni cheap kuliko kununua hapa, kwanza bidhaa zetu hapa madukani nyingi ni fake na bei zake ni kubwa kuliko original za nje. Mimi nina miaka zaidi ya kumi sijawahi kununua bidhaa za electronics hapa tz, na Nina save kiasi kikubwa cha pesa eg TV ya USD 400 hapa kwetu bei yake ni almost 3 times. Tatizo la tra huwa wanakadiria tu thamani ya mizigo changamoto hii utaipata tu hata ukitumia courier eg dhl , ups atc
 
Me kuna mzigo wangu umefika pale.. naenda nawapa tracking number wanasema eti kwenye system unaonyesha umefika ila hawajui ulipo..

Yani hapa sijui nifanyeje. Kila siku story ni zile zile.
 
Kwa mawazo ya watu kama wewe Tanzania yenye neema tusubir sana. Mtoa Uzi sidhan kama kuna sehemu amesema hataki kuchangia kodi. Yeye amelalamika kodi aliyokadiriwa kwa kulinganisha na bidhaa aliyoiimport.
Kama ana receipt na evidence kwanin kodi ikadiriwe??? Percent ya kodi inajulikana. Mtu anapoficha gharama za bidhaa aliyonunua ndo hukadiriwa kodi
 
Me kuna mzigo wangu umefika pale.. naenda nawapa tracking number wanasema eti kwenye system unaonyesha umefika ila hawajui ulipo..

Yani hapa sijui nifanyeje. Kila siku story ni zile zile.
fungua kesi mahakamani... mtafute mwanasheria... iwe funzo kwa shirika... ili tukamate mali za shirika na wateja wao... kama wacanada
 
Me kuna mzigo wangu umefika pale.. naenda nawapa tracking number wanasema eti kwenye system unaonyesha umefika ila hawajui ulipo..

Yani hapa sijui nifanyeje. Kila siku story ni zile zile.
Swala la uaminifu linatushishia heshima sana hata wanaoshinda makanisani na misikitini ndio maana baadhi ya nchi wanakataa shipping za kuja nchi zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…