TRA: Ukinunua bidhaa na usipodai risiti utapigwa faini ya kati ya Tsh. 30,000 na Tsh. 1,500,000

Nimuhim KWANZA tujuzwe ni bidhaa ya kuanzia sh ngapi inaitaji risiti kwanza
 
Mimi nina shanga wageni wanakuja nchi hii wanapewa leseni ya biashara bila kuwa na efd au pos machine, wauzaji wengi wa vifaa vya ujenzi iwe ceramic, tiles , mbao, vifaa vya computer hada maeneo ya Kariakoo , msimbazi area etc etc , siku hizi mpaka wanapita nyumba kwa nyumba wanauza vyombo vya nyumbani kwa mkopo, nchi zingine dkk mbili tu umeibuliwa na kuondoshwa, hatukatai wafanye biashara lakini kuvunja sheria kwa kukwepa kodi ni kosa kubwa au kufanya uhalifu. Sweden ilikuwa ukiishi miaka 5 bila makosa unapewa uraia kwani Ile fit inn their society
 
Hilo nalielewa..point yangu ni kwa yule anayenunua bidha kwa matumizi yake binafsi?
Mfano umeenda nunua tv ya 300000 hapo akipewa risit itajumuishwa na VAT
Mlaji hapo anabeba risit yake na tv anaenda nayo!
Hpa nimezungumzia upande wa mnunuzi wa bidhaa umuhimu wake wa kuchukua risit kwa upande wake siyo mfanyabiashara

Ova
 
Inategemea na bidhaa unaponunua kitu kama TV chenye warranty kikiaribika jamaa waliahidi wanakuja kutengeneza or somen to do with products ambazo inaweza kuwa mbovu utarudisha vipi kama auna receipt.

Receipt kwa mteja iwe kwa faida yake sio TRA.

Lakini nimetoka kuweka mafuta petrol station kwanini nilazimike kuchukua receipt haya how long am I supposed to keep it after that? wakati kuna watu wanajaza mafuta every 3 days, wengine weekly; what is the point ya kuchukua hizo receipt na kuziweka kwenye magari yao?

TRA waache kutupia watu lawama kwa kukosa mbinu za kuzuia mianya ya kodi, waangaike na wafanyabiashara sio kutaka kuonea raia.

Nakubaliana unaposema wa encourage watu kuomba risiti lakini sio kulazimishana kwa fines; huo sasa unakuwa uonevu.
 
Hahaha umewaza nini lakini fundi25?
Halafu leo ndio kwanza January 7πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Aisee acha tu ninaona nia yao ya kufikisha trillion10 kabla ya 2022 aisee mama D nimepata tarifa kupima Corona ni 100$?
Apo Namanga mpakani na Kenya hawa pimi bure tena kwa kulazimisha au hii ya 100$ ni tofauti?
 
Mkuu nimekuelewa vizuri sana mawazo yetu yako sawa ila wewe umei balance na kuiweka kitaalam sana ....

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Mtaweka nini kwenye ma file mkuu
Hizo risiti za mafuta petroli na vitunguu na nyanya na chumvi na nyama Embu niambie ninunue file ngapi zita tosha maana kuna kila dadali siku moja watakuja kusema tuende serekali za mtaa tunaonyeshe risiti za matumizi ya mwaka au miezi sita!
Waki kukosa na risiti ya sukari itabidi wakupime kama una kisukari vinginevyo una lipa faini pamoja na viboko maana wamesha anza mambo ya kuchapana viboko!
 
Tunapoelekea itakuja "ukikutwa na mwanamke wa mtu, au ambae hujaoa, faini laki 3"[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sheria ipo hiyo ya ugoni mbona
Sema haijafanyiwa kazi [emoji23][emoji23][emoji23]
Naona unawastua sasa ohoooo

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Huu ni usanii tu, maduka mengi hayana hizo risiti Wala kulipa Kodi, hebu adhabu hizo zipelekwe kwa wenye maduka wanatuuzia bidhaa, kingine bidhaa nyingi siku hizi zinauzwa kichinga hivyo watathimini biashara zote ziingizwe kwenye mfumo wa Kodi Ili zipatikane kwa risti Ila kwa mnunuzi kulazimisha risiti ni uonevu, adhabu apewe muuzaji ndo alazimike kutoa risiti kwa mteja Kama wanavyofanya maduka ya supermarket makubwa huwezi kuomba risiti ni wao wanakupa risiti yako.
 
Mungu amemkabidhi mamlaka shetani hasa ya ulimwengu huu, lazima uwe matured enough kutambua hilo, na kutii hizo mamlaka za aina hiyo ni sawa na kutii mamlaka za shetani.
TRA wanatakiwa kutoa elimu kwa wanacnhi si kuwatisha. Kwanza, wafanye ukaguzi wa hizo mashini kwa wafanyabishara walizonazo kama kweli wanatoa risiki halali. Pili, wapanue wigo wa walipa kodi, kuna sehemu nyingin tu amabzo biashara inafanyika lakini haman kodi inayokusanywa, mfano, kuna nyumba bubu ngapi za wageni (gesti), na baa ngapi zinatoa risiti kila wanapouza vinywaji? Je, wenye nyumba ambazo hupangishwa wanalipa kodi maana wanafanya biashara biashara!
 
Basi kama huamini tumia imani yako kufanya yanayokupasa na Mungu atafanya anayoyataka. Usivae viatu vya Mungu bali fuata maagizo yake
Wapi nimevaa viatu vya Mungu? Nyie mnaotaka kuhalalisha uovu kwa kupitia Biblia ndiyo WANAFIKI wakubwa
 
Kwa nini majukumu ya TRA yanahamishiwa kwa raia? Ni jukumu la muuzaji kutoa risiti, na jukumu la TRA kuhakikisha kila mfanyabiashara anatoa risiti. Si jukumu la mlaji kumlazimisha mfanyabiashara atoe risiti. Watulipe basi.
What a great argument!! Hapa wanachemka kabisa kusema watawapiga faini wananchi kwa kutochukua risiti. Wao wanapaswa washughulike na muuzaji. Muuzaji yeyote anayetumia EFD impliedly ni Wakala wa TRA. Its therefore utter nonsense kuwasumbua wananchi kuhusu risiti. Hata kama ni Sheria imetungwa itakuwa ni BAD LAW na ikikutana na manguli wa Sheria wanaipangua
 
Aisee acha tu ninaona nia yao ya kufikisha trillion10 kabla ya 2022 aisee mama D nimepata tarifa kupima Corona ni 100$?
Apo Namanga mpakani na Kenya hawa pimi bure tena kwa kulazimisha au hii ya 100$ ni tofauti?
Hahaha kwani unataka kukimbilia wapi fundi25?
 
Mna ongea ili kumfurahisha mtu. Hivi Machinga hutoa risiti?? Huu mna taka kuleta usumbu tuu kwa watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…