Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Klabu ya TRA United imetangaza kusitisha mkataba na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya timu hiyo kuanza vibaya msimu wa 2026/2027 wa Ligi Kuu ya NBC, ikiwa haijapata ushindi katika michezo yake mitano ya mwanzo.
Katika michezo hiyo, TRA United imetoka sare mara tatu na kupoteza miwili, matokeo yanayoifanya kushika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi tatu.
Kwa hatua hiyo, Ndayiragije anakuwa kocha wa kwanza kuondoka katika klabu ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wa 2026/2027.
TRA United imemshukuru Ndayiragije kwa kujitolea, weledi na mchango wake kwa timu, huku ikimtakia kila la heri katika hatua inayofuata ya safari yake ya ukocha.
“Tunashukuru kwa kujitolea kwako, weledi na mchango wako katika timu yetu. Tunakuombea kila la heri na mafanikio katika hatua inayofuata ya safari yako ya ukocha. Asante kwa kila kitu, Kocha Etienne Ndayiragije,” imeeleza taarifa ya klabu hiyo.