TRA: Wafanyabiashara wa Mitandaoni mjisajili Ndani ya Mwezi Mmoja!

Duh
Unafikiri kilichowakimbiza UBER ni nini?? Kodi mzee BOLT na UBER wanagongwa kodi tena kubwa mnoo yani zamani ilikua 10% LATRA na TRA wakaongeza mpaka 15 to 20% Uber yakawashinda wakatupa taulo wakamuachia BOLT
 
Kuna hawa, TRA mnapaswa kukusanya kodi asilimia 50 ili wajue uchungu wake kama raia
1. Rais, Makamu wake, waziri mkuu, mawaziri na watendaji wakuu.
2. Spika wa bunge na wabunge wote wakatwe Kodi asilimia 40
3. Jaji mkuu, Mkuu wa majeshi na ma CEO wa mashirika ya umma na makampuni wakatwe asilimia 40 ya mishahara Yao
Wengine ni hawa wasanii kama Diamond, makanisa kama Mwaposa na yule mzee wa upako na wengine wengi tu, wakatwe kodi asilimia 30 ya makusanyo yao..... Lakini zaidi sana TRA wanapaswa kuzingatia matumizi zaidi. Hakuna maana ya kukusanya sana kwa ajili ya matumizi makubwa ya hovyo!
 
Na wale wajasiriamali wa kimya kimya, wa uficho na wa uwazi, kutwa kutuonyesha mitako, mihips mikubwa mikubwa.. Itakuaje?
Halafu machine moja laki, hao kipato chao kinazidi 4m kwa mwaka lazima walipe kodi.
Ila mtaji wao sijui una thamani gani.
 
Inasikitisha sana
 
Aah Wapi
Wapunguze mishahara ya wabunge tu
 
Mimi Kama Nina duka Ila nauza kupitia online je unataka nilipo kodi mara mbili? Dukani na online.
Kama umeisajili TRA hamna shida mkuu kodi utalipa mara moja tu hapa wameongelewa wale ambao hawajazisajili biashara zao na wanategemea kuuza kupitia online
 
Bora maana biashara wote tulipe kodi siyo wengine kwa kuwa tupo kwenye maduka ndiyo tulipe tu. Uzuri biashara zinatakiwa tulipe kodi sioni cha ajabu dunia sasa hivi inaenda kidigitali naona na kodi nayo inakusanywa kidigitali hongereni tra.
 
Mie biashara zangu zipo twitter au x, mtandao walio ufungia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…