Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kutoa hoja kwa kuhoji “Serikali ilitoa msamaha wa kodi kwa Wafanyabiashara wapya ila TRA bado wanakomaa nao, msamaha ulifutwa?”
Kama hukusoma, bofya hapa ~ Serikali ilitoa msamaha wa kodi kwa Wafanyabiashara wapya ila TRA bado wanakomaa nao, msamaha ulifutwa?
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi kwa kueleza kuwa wao wanasimamia na kukusanya kodi kwa mujibu wa Sheria na kanuni zilizopo, na kwamba kuanzia tarehe 1 Julai, 2026 wafanyabiashara wote wanaoanza biashara na kusajiliwa kwa mara ya kwanza wameendelea kupewa msamaha wa kodi unaodumu kwa miezi 12.
Ufafanuzi huo umetolewa na Mkurugenzi wa Elimu na Mawasiliano wa #TRA, Richard Kayombo ambapo ameeleza “Pale kwenye makadirio kama unakidhi sifa zote za mfanyabiashara mdogo anayeanza biashara TRA wanakupa makadirio ya sifuri, na kukuelekeza nini unatakiwa kufanya kwa kipindi chote hizo.”
Ameongeza “Mojawapo ni kutunza kumbukumbu zako za mauzo ikiwezekana hata za taarifa za manunuzi kama zipo, na hapa wamesema hata ukiwa na daftari linatosha kuwa nyenzo ya kutunzia kumbukumbu.
“Cha muhimu kule mwishoni ukisalia mwezi mmoja kabla ya mwaka kupita wapelekee taarifa zako hizo, kwani hapo utakuwa umeshatambua mzunguko wa biashara yako.
“Hii imesaidia sana kutoa motisha ya kufungua biashara tofauti na ile ya awali kwani ukianza tu unakutana na makadirio yako ingawa walikuwa wanaahirisha tu kulipa ile awamu ya kwanza, lakini sasa hivi ni kujiachia mwaka mzima.”