TRA Wamekanusha Taarifa zilizoandikwa JamiiForums zilizodai Mtandao wao kusumbua.
Wamesema ni taarifa ya Uongo na Uzushi. Kwani imelenga kupotosha na kuleta taharuki miongoni mwa Walipa Kodi pamoja na kuidhalilisha taasisi na Watumishi wake.
Katika kipindi cha mwezi mzima, TRA haikuwa na Hitilafu yoyote.
TRA imewataka Waipa Kodi kuendelea kulipa kodi.
Wamesema ni taarifa ya Uongo na Uzushi. Kwani imelenga kupotosha na kuleta taharuki miongoni mwa Walipa Kodi pamoja na kuidhalilisha taasisi na Watumishi wake.
Katika kipindi cha mwezi mzima, TRA haikuwa na Hitilafu yoyote.
TRA imewataka Waipa Kodi kuendelea kulipa kodi.
- Tunachokijua
- Jamii Forums inatoa uwanja kwa watu kuweka malamiko, ushauri na maoni ili kuleta mabadiliko kwenye jamii na uongozi. Mei 27, 2021 mmoja wa wanachama wa Jamii Forums aliandika uzi wa kumtaarifu Rais Samia kuhusu uozo unaoendelea Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) ambapo pamoja na malalamiko mengi alizungumzia suala la mtandao kusumbua nchi zima siku ya Mei 26, 2021 hali aliyoitaja kuleta usumbufu kwa walipa kodi.
Uzi huo ulikuwa na kichwa cha habari kinachosema "Rais Samia ingilia kati, TRA watatukwamisha"
Mei 28, 2021, ikiwa ni siku moja baada ya mwanachama huyo kuweka uzi wa tuhuma hizo TRA walitoa andiko kukanusha suala la mtandao kutopatikana nchi nzima. Na waliandika kuwa mtandao wao ulikuwa unapatikana kwa wiki nzima bila usumbufu wowote na kuutaka umaa kupuuzia tuhuma zilizotolewa na member wa JamiiForums.
Barua ya TRA kukanusha madaiKwenye Madai yake msingi Mwanachama wa JamiiForums alisema ikibidi ifanyiwe uchunguzi (Analysis) ya mapato kwa miezi miwili nyuma yaani Aprili na Mei ili kuangalia mtiririko wa mapato kwa mwezi kama yana utofauti mkubwa baina yake.
Katika majibu yao, TRA hawakuonesha trend iliyodaiwa na mwanachama wa Jamii Forums bali walitoa mawasiliano ya mtu kuwasilisha malalamiko.
Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianzishwa kwa sheria ya Bunge Na.11 ya mwaka 1995, na ilianza kufanya kazi tarehe 1 Julai 1996. Katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria, TRA inaongozwa kwa sheria na ina jukumu la kusimamia kwa uadilifu kodi mbalimbali za Serikali Kuu