TRA wamekuja ofisini kwetu wakitaka kukagua hesabu za 2012 Hadi 2017

TRA wamekuja ofisini kwetu wakitaka kukagua hesabu za 2012 Hadi 2017

Umeandika ukitetemeka?

TRA wana haki ya kukagua na kujiridhisha document muhimu kwa mwaka wowote ingawa muda wa ukaguzi hufanyika walau ndani ya miaka mitano ingawa siyo kigezo cha kuwazuia kukukagua.

Toa document na onyesha ushirikiano
 
Unless mshakwaruzana nao before mahakamani mkapatikana na hatia ndio kampuni inatakiwa kutunza record zaidi ya miaka ya sheria; kutokana na kosa lenyewe.

Vinginevyo unatakiwa kuwa na records za muda unaotakiwa kuwanazo kisheria. Tena waje kwa adabu kama ni mlipa kodi mzuri polisi wasiingie ofisini hiyo sio raid na wala udaiwi; vinginevyo wafungulie ya matumizi mabaya ya sheria.
 
Umeandika ukitetemeka?

TRA wana haki ya kukagua na kujiridhisha document muhimu kwa mwaka wowote ingawa muda wa ukaguzi hufanyika walau ndani ya miaka mitano ingawa siyo kigezo cha kuwazuia kukukagua.

Toa document na onyesha ushirikiano
Asante kwa ushauri.

Ushirikiano watapata. Nilitaka kujua tu kisheria hii ni sawa?
 
Hii imekaaje wadau. Hapa tunaulizana mbona wameanzia kote huko. Shida ni nini?

Mi najua sheria ni miaka mitando nyuma.

Wataalamu tuelimishane, maana nibampango wa kuwabishia wakija kukagua.
Kama mahesabu yako yalikaguliwa na hiyo miaka na ukapata Tax clearance certificate basi waonyeshe lakini kama hukukaguliwa kaka unalo hilo kaa nao mezani huna namna.
 
Kisheria audits na examination hua ni miaka mitano. ila kama ni investigation hamna limit ya miaka kwa sababu investigation maranyingi inafanyika pale panapokua na viashiria wa ukwepaji kodi (tax evasion) ambalo ni kosa la jinai na kama tunavyofahamu jinai haina limit ya muda ata kama mtu aliifanya miaka 30 iliyopita mambo yakiaribika itamuhusu tu.

tena mna bahati ilipaswa waje na vifaa vya kunyonya taarifa kutoka kwenye mifumo yenu.
 
Back
Top Bottom