TRA wana jambo lao, Sio kwa watu maarufu tu, ndugu yangu alieanza biashara 2015 kwa mara ya kwanza kapigwa faini nzito ya kukwepa kodi,

Na hapa umezungumzia Compliance za TRA pekee.

Bado mfanya biashara huyo huyo anadaiwa Leseni, Fire, Afya, Ulinzi Shirikishi, Wakala wa Vipimo, TBS, Usafi, Parking n.k n.k..

Na wote hao kila mmoja anakuja au unamfata kwa wakati wake.

Hii nchi mfanyabiashara ili Ufanikiwe ni lazima utaonekana haramia tu..

Wakati huo huo Ripoti za CAG kila mwaka zinataja matumizi mabaya ya Pesa za Umma miongoni mwa Watendaji wa Umma. Na hakuna hatua zinachukuliwa kudhibiti hili
 
Sasa serikali inajiweza kifedha!!?..makusanyo kiasi gani na bajeti kiasi gani!?
 
Mkuu,
Achana na uchumi wa makaratasi,
Twende kwenye vitu vyenye uhalisia.

Ndo maana nmekuuliza hivi unajua

1. cement mfuko mmoja unauzwaje nawe unapaswa ukauzeje?

2. Soda/bia kreti moja Inauzwa sh. Ngapi na Ina faida sh ngapi?

3. Sukari kiroba kimoja kinauzwa sh. Ngap,unatakiwa kuuza sh. Ngap na faida itakua Kias gani.

4. Mchele kiroba kimoja kg100 kinanunuliwa sh ngapi, unatakiwa kuuza sh ngapi na faida Kia's gani?

Hivi unadhan wafanyabiashara wakiamua kuuza kwa kutaka faida unazosema wewe kwenye makaratasi, unadhan Kuna mwananchi atalimika uko mtaani?

Au Ndo mtakuja mitandaoni kulalamika makali ya maisha, serikali itangaze Bei elekezi na iweke taski force kukamata na kuonea wafanyabiashara.
 
Tatizo umesoma tu kichwa cha habari hujasoma post, soma kila neno kwenye post uniambie ni wapi nomefurahia
Hapa unaemlaumu kwa uzembe Ni Nani?

Hiki Umeandika wewe au mwingine?[emoji116]

"Ila nikowa muwazi bila kupepesa macho, kapigwa faini kwa uzembe wake maana haiingii nimeshangaa inakuwaje anunue mzigo wenye kodi ya vat alafu asitoe risiti"
 
Umepiga mahesabu yako kitoto Sana

Haya mahesabu yako wanapiga sn watoto wa pale IFM kila siku, ila ukiingia mtaani Hali Ni tofauti kabisa.

Bado mfanya biashara huyo huyo anadaiwa BIMA, Leseni, Fire, Afya, Ulinzi Shirikishi, Wakala wa Vipimo, TBS, Usafi, Parking n.k n.k..
 
Watu walipe Kodi ,TRA inadekeza Sana wafanyabiashara na Wananchi ambao hawadai Risiti.
 
Nikukwepa tu hakuna namna
 
Nilitaka kuandika hivi ila nimepita kimya. Kuna thread ingine huko nimefafanua hivi nimeshambuliwa sijui kitu ni mwajiriwa tu.
 
We jamaa ulishawahi kufanya biashara kweli au unategemea dirishani mwisho wa mwez
 
Wewe ndie unaeleta utoto, umeona nimekuja na facts na mifano halisi ya hesabu za vat umekosa cha kujibu umeanza umeanza kuzungumzia bima, leseni, fire, ulinzi, n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…