berylyn
JF-Expert Member
- Dec 26, 2021
- 877
- 2,618
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mfano mdogo tu,kuna kituo cha afya huku niliko ilishindikana kuzinduliwa na mwenge wa uhuru kwasababu kimejengwa chini ya kiwango,yaani hata mtu ambae syo fundi alikuwa hawezi kujenga kajengo ka namna hii.Zinatumikaje!?..acheni kuimbaimba vibwagizo msivyovijua
Hamna penalties za kufika 160m
Efd machine penalty ni 3 au 4.5 mSema kaongeza 0
Fine yake ni 4.3 m
Mfumo wetu wa vat ni wa kijinga mno. Mlipa vat sio muuzazi ni mnunuzi wa mwisho. Inatakiwa ukishanunua bidhaa kwa vile uneilipia vat ikifika kufile ulipe ile difference ya vat tu. Maana kuna asilimia tayari umeshalipa uliponunua mzigo. Hizo refund siamini kama tra wanazifanya maana inabidi mwisho wa mwezi akurudishie kilichozidi.Niwaambie TU wanajf
Hamna mfanyabiashara anapenda kukwepa Kodi kwa maendeleo ya nchi yake
Tatizo Ni
1. mfumo wetu wa Kodi umekaa kinyonyaji sana, anaetunga sheria na kanuni za Kodi ni mwanasiasa bill kumhusisha mfanyabiashara na hayajui mazingira halisi ya biashara.
Ukiifuata sheria ya Kodi inavotaka unafilisika mchana kweupe na hakuna anaekuonea huruma, kiukweli Kodi zetu sio rafiki kwa mfanyabiashara yeyote mzalendo.
2. Matumizi ya Kodi,
Inaumiza Sana unalipa Kodi kizalendo afu unaskia Kodi yako uliolipa Kuna wahuni wanafuja fuja TU kwa maslahi Yao binafsi Tena kwa majigambo lukuki wakiitana majina wanayojua wao kana kwamba sisi wengine hatuna akili wametupa limbwata.Inaumiza sana na kuvunja Moyo.
Unazunguka Sana issue ni kuna wafanyabiashara wawili wote wanauza cement mmoja ana VAT na mwingine Hana vat registration.Unaongea vitu vipo out of context kuhusu vat na inaonekana wazi hujui hata vat inavyofanya kazi.
Hata mfuko wa cement uuzwe elf 50, kama mtu kanunua kwa risiti ya tra yenye vat na akaenda kuuza kwa kutoa risiti ya tra yenye vat atapata faida + kukomboa vat aliyolipia..
Nilichoona ni kwamba suala zima la vat bado huna elimu ya kutosha.
Halafu kuwa na akili hata kidogo basi, kwa akili yako umeona makampuni makubwa kama ya soda ndio yakwepe vat!! Haupo serious kuwafananisha cocacola / pepsi na wafanyabiashara ambao hawana hata wahasibu.
Kwahiyo wanaolipa kodi za miamala ya simu hawalipi kodi? Hivi kuna mtu anaweza kununua hata soda tu halafu usema hajalipa kodi? Tanzania hii kila mtu analipa kodi, hata mtoto mdogo anaekula pipi, ile pipi kailipia kodiTatizo la Tanzania walipa kodi hawafiki 6mil.
Hivyo ni asilimia 10 tu ndo hulipa, tungeongeza wigo wa kodi kelele zisingekuwa nyingi.
Leo mfanyabiashara akisema atoe risiti kamili ataumia yeye maana atakosa wateja kwani itabidi aongeze ile 18%
Viwanda ndo vinafaidi kwenye VAT ila biashara ndogo ndogo ambazo hesabu zake hazijulikani ni ngumu sana
Nimeogopa mno kariakoo wafanyabiashara wengi, about 60-70% suppliers wao ni unknowns, lakini risiti wanatoa za mashine sijui itakuwaje?Nimejiridhisha kwamba kwa sasa TRA wana jambo lao kwa wakwepa kodi maana si kwa kelele hizi, wakiona unakwepa wanapita na wewe.
Mwezi uliopitwa nilipatwa na simanzi baada ya kuona ndugu yangu kapatwa na pigo zito la kulipa faini ya TRA, masikitiko yake yamenigusa na mwanzoni nilidhani kaonewa lakini hali ni tofauti.
Hawa kina diamond na huyo pck wanaolalamika ni kwasababu ni maarufu ndio maana wanasikika lakini wakae wakijua sio wao tu, hii ni operation kubwa sana iliyonasa wengi tena kihalali bila uonevu wala mabavu.
Binafsi nina ndugu yangu alianza biashara kwenye mwaka 2015 hivi, Enzi hizo Magu kaingia na msisitizo watu watoe risiti kwa mashine, hapa waliokuwa hawana mashine ndio walikiona cha mtemakuni, kukwepa huu mhaho wengi ilibidi wanunue hizo mashine ila wakawa wanatoa risiti chache za kuzugia, ila kwa sasa hali ni tofauti kabisa, hio style ya kutoa risiti za kuzugia utapigwa pini tu,
yaani kwa sasa wanafatilia mfano biashara za kuuza bidhaa inabidi mzigo ulionunua uwe na risiti yake ya mashine ya tra na pia uwe unauza kwa kutoa risiti kwa mashine, huyu ndugu yangu alipodakwa ni kwamba alikuwa ananunua bidhaa na alikuwa anapewa risiti lakini yeye anatoa tu risiti chache za kuzugia kwa bidhaa alizouza, Tra wakastuka wakaenda dukani kwake kukagua mzigo wakamwambia wameona kwenye system yao anauziwa bidhaa nyingi na watu wanaomuuzia kwa risiti lakini yeye vitu anavyouza kwa risiti ni vichache, mzigo uliobaki uko wapi ? Akaanza kupiga kiswahili pale lakini haikusaidia, TRA wakahitimisha kihalali kwamba anauza bila kutoa risiti a.k.a anasaidia ukwepaji wa kodi.
Wakati anasubiri hatma ya kitachomkuta alitumia connections zake na kwenda kuwabembeleza Tra kwenye ofisi zao lakini wapi... Kwanza hata huko akagundua wapo wengi.
mwezi uliopita kapigwa faini ya takribani milioni 160, hio faini ni mchanganyiko wa VAT walizokadiria kakwepa + interest + efd penalty, n.k.
Cha kushukuru ni kwamba hawakufunga akaunti zake ama kumpeleka mahakamani, hadi hapa alipo imebidi aanze kurejesha mdogo mdogo kwa maumivu makali sana, yaani kwa sasa yupo makini sana kuuza bidhaa kwa kutoa risiti za vat.
Ila nikowa muwazi bila kupepesa macho, kapigwa faini kwa uzembe wake maana haiingii nimeshangaa inakuwaje anunue mzigo wenye kodi ya vat alafu asitoe risiti jli kuikomboa vat, nimeumia sana hapa maana hili lilikuwa linakwepeka.
Kimbembe kipo kwa wanaonunua mizigo isiyo na risiti za tra, hii mara nyingi ni kwa wale wanaouza magendo yaliyoingizwa nchini bila vibali, Yani hapa utayaita maji Mma!!