TRA wana jambo lao, Sio kwa watu maarufu tu, ndugu yangu alieanza biashara 2015 kwa mara ya kwanza kapigwa faini nzito ya kukwepa kodi,

Zinatumikaje!?..acheni kuimbaimba vibwagizo msivyovijua
Mfano mdogo tu,kuna kituo cha afya huku niliko ilishindikana kuzinduliwa na mwenge wa uhuru kwasababu kimejengwa chini ya kiwango,yaani hata mtu ambae syo fundi alikuwa hawezi kujenga kajengo ka namna hii.

Huduma za dharula kama kujifungua kutoka hapa nilipo mpaka kituo cha afya cha jirani kama huna 100,000/= husafirishi mgonjwa wako. Sasa niambie kwa namna ambavyo jengo hili linachelewesha huduma kwa wananchi tena kwa kwa makusudi ya wajanja wachache unahisi mtu kama mm nikiona watu wanshikwa mashati kuhusu makusanyo ya kodi najiskia vipi?
 
Huyo jamaa ni mpumbavu, mim ningeweza kumpanya asikutwe na huo msala.
Kwa mfumo wa TRA na Efd machine unavyofanya kazi ni ujanja kidogo tu ushahidi ungepotea
 
Sera na sheria zetu za kikodi ndio miyeyusho kuna vipengele viiingi na mahesabu meengi yasio na kichwa wala miguu ndio maana mtu anapopata upenyo wa kuwa piga anawapiga! Shida una piga alafu unajisahau ndio mtihani
 
Mfumo wetu wa vat ni wa kijinga mno. Mlipa vat sio muuzazi ni mnunuzi wa mwisho. Inatakiwa ukishanunua bidhaa kwa vile uneilipia vat ikifika kufile ulipe ile difference ya vat tu. Maana kuna asilimia tayari umeshalipa uliponunua mzigo. Hizo refund siamini kama tra wanazifanya maana inabidi mwisho wa mwezi akurudishie kilichozidi.
 
Unazunguka Sana issue ni kuna wafanyabiashara wawili wote wanauza cement mmoja ana VAT na mwingine Hana vat registration.

Bei zitakuwa

1. 50,000 VAT Exclusive
2. 59,000 VAT Inclusive


Je mteja ataenda kununua hiyo cement kwenye Duka lipi Kati ya hayo mawili ?

Jibu la harakaharaka ataenda kwenye ofisi inayouza bei bila vat - Kwa mfanyabiashara ambae hajasajiliwa kwenye VAT. Je, huoni hiyo inaathiri mfanyabiashara aliesajiliwa na vat kutokufanya biashara?


Haya ndio mazingira yaliyoko mtaani. Nenda kariakoo uoneshwe wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa na VAT.

Acheni kukalili madesa ya nyambari nyangwine kuwa ukifikia Total turnover ya milion 100 au 50 Kwa miezi 6 lazima iwe Vat registered. Futeni huo upuuzi kichwani ingieni mitaani muone uhalisia nyie wasomi uchwara ndio maana mnadharaulika Kwasababu mnachokijua sio kilicho mtaani
 
Kwahiyo wanaolipa kodi za miamala ya simu hawalipi kodi? Hivi kuna mtu anaweza kununua hata soda tu halafu usema hajalipa kodi? Tanzania hii kila mtu analipa kodi, hata mtoto mdogo anaekula pipi, ile pipi kailipia kodi
 
Nimeogopa mno kariakoo wafanyabiashara wengi, about 60-70% suppliers wao ni unknowns, lakini risiti wanatoa za mashine sijui itakuwaje?
 
SEREKALI IJITAHIDI KUONDOA MFUMO WA MALIPO YA ULIPAJI BY CASH, IONGEZE BIDII KATIKA A. I, WATANZANIA WATUMIE E-CARDS KWENYE MALIPO MBALIMBALI HATA SISI TUNAOPANDA MADALADALA TUWEZE KU SWAP, TUOMBE WATAALAMU TOKA EUROPE WAJE WAPEMBUE HILI KWA KINA UONE JINSI NCHI ITAKAVYOPAA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…