HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 70,791
- 98,334
Wewe ni wakala wa kukusanya VAT,TRA wanamatatizo sana,
Tatizo kubwa hawatoi elimu kabisa watu wanahangaika kutafuta elimu wenyewe.Na hili wanalifanya kusudi ili wapate mwanya wa kuwatisha watu wawape rushwa.
Kikiubwa inapswa iwe wazi namna wanavyokokotoa 18% ya VAT,je wanapiga kwenye mauzo ama kwenye faida?
Kama VAT itakua inafanyiwa hesabu kwenye mauzo huu utakua ni wendawazimu,ila kama watakua wanafanya hesabu kwenye faida si mbaya.
Chukua mfano Mimi na Juma tuwe na biashara zinazo fanana kwa kila namna,Mimi niwe kwenye VAT na Juma awe kwenye kodi ya mapato,bidhaa ikiwa na thamani mf 10,000/=,nitalazimika kuweka 18% ya VAT ambayo ni 1800/=,nikiijumlisha kwenye bei nitalazimika niuze 11800,
Kwa mfano huo wa mimi na juma utaona kwamba Juma yeye kwakua hayupo kwenye VAT anauwezo wakuuza kwa 11,000 akapata faida ya 1000,je .Mimi nitapata wateja?
Hii ndio hofu ya mtoa mada na wafanyabiashara wengi.
Tatizo kubwa kwenye biashara, ni hizi mambo za kutengeneza makundi,kama ilivyosasa hawa wa VAT na hawa sio wa VAT.Hapa kuna leta unfair competition na hili ndio tatizo kubwa linaloua biashara za watu.
Kinachotakiwa watu wote wawekwe kwenye mfumo mmoja,mfano watu wote wawe kwenye VAT na wote wawe na EFD machine.Na hizi machine zitolewe bure TRA.
Unfair competition inaua sana biashara,naamini kama kila mfanya biashara akipewa EFD mashine inawezekana kabisa VAT ikashuka hata 5% na makusanyo yakawa maradufu kuliko ilivyosasa.
VAT hulipwa na mlaji