TRA wananiambia niingie VAT

Wewe ni wakala wa kukusanya VAT,
VAT hulipwa na mlaji
 
Muongo

TIN husajiliwa kwa alama za vidole au NIDA
TIN lazima uende kukadiriwa ili upewe ya biashara
TIN ya Msimbazi huwezi itumia Tegeta

Punguza ubishi tin inasajiriwa kwa kitambulisho cha nida na kwenyw coment yangu nimeandika nimekusanya vitambulisho vya ndg ninavyo
Halaf sijawah hangaika kwenda kusajir ndg vishoka ndo kazi yao nawapa kitambulisho na chao wananiletea tin/makadirio na lessen
 
Kuna namna hesabu za ulipaji wa Return(ritani) za VAT hufanyika na ukalipa kiasi kidogo kabisa unachostahili kulipa naa bado ukabakia na faida kubwa ila wengi hawajui,kwa msaada zaidi unaweza nicheck mkuu.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Tra wananiambia wanikadirie mil 3.4 na kila mwezi nalipa vat sasa naona ni makato juu ya tozo
Kuna namna hesabu za ulipaji wa Return(ritani) za VAT hufanyika na ukalipa kiasi kidogo kabisa unachostahili kulipa naa bado ukabakia na faida kubwa ila wengi hawajui,kwa msaada zaidi unaweza nicheck mkuu.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Huwezi kupewa leseni kama huna tax clearance...na tax clearance unapewaje na hata hiyo robo ya makadilio na WHT hujalipa (endapo unapofanyia biashara umepanga).

Unalipa kodi husika, unapewa tax clearance unapeleka halimashauri unakoenda kupewa business licence.

Acha uongo boy
 
Hii point nimesoma mara tatu,naona ina ujumbe sana ila bado sijaelewa vizuri naomba nieleweshe tena.

Kwamba mdau, anatumia laverage kisha anauza kwa receipts? Kama angenunua na akauza kwa receipts ingekuaje? Isingefika 100m?
 
Njoo dm unipe kitambulisho chako then nipe 2days nitakupa tin/lessen/tax clearance za mkoa wa kikodi kinondon au endelea kubishana sababu unaamin kila kitu lazima ukipate kwa utaratibu
 
Hii point nimesoma mara tatu,naona ina ujumbe sana ila bado sijaelewa vizuri naomba nieleweshe tena.
Kwamba mdau, anatumia laverage kisha anauza kwa receipts? Kama angenunua na akauza kwa receipts ingekuaje? Isingefika 100m?
Huku mtaani wapo matajiri wanaoingiza mizigo wanawapa kwa mali kauli vendors,(kama mdau hapa) wao huwa hawana frame mzigo wanautoa store wanampa muhusika kwa makubaliano may be kila siku jioni au kila wiki watapitia pesa kiasi fulani sasa kinachomuumiza huyu yeye ndiye anayekutana moja kwa moja na mteja(anayetaka efd receipt) na mamlaka ya mapato (TRA waki-track mauzo yake kupitia efd) huku anakochukua mzigo risit hapewi kwa ajili ya kufanya return ya kodi TRA!

Kwenye bold,nimemsoma jamaa main post hapo juu anasema mtaji wake ni Tsh 15mill,kwa hela hii ni ngumu kubishana na ma-giant wa biashara kwa kuwataka wampe risiti kwa kila bidhaa na kawaida yao huwa hawatoi wanakata udhamini na hata wakitoa 15 mill atanunua items ngapi za kuzungusha sokoni ili biashara iende?kwa mtaji huo hata angezungusha vipi na faida aliyosema kwa siku ni 12K ndani ya mwaka bado asingefika VAT so ni kusema alitumbukia kwenye shimo baya la utumwa wa kibiashara.
 
Sema hapo kwenye faida ya Elfu 12 ni [emoji477]️ hata muuza matunda tu anakunja faida mara mbili ya hiyo kwa siku
 
Asante,
Nimepata kitu muhimu sana..ubarikiwe
 
Kinacho katisha kulipa kodi ni kwamba wananchi wanalipa sana kodi halafu kodi hizo wanatumia wanasiasa ambao sio walipa kodi hivyo ni afadhari kukwepa tuu kodi
 
Reactions: Tsh
Kinacho katisha kulipa kodi ni kwamba wananchi wanalipa sana kodi halafu kodi hizo wanatumia wanasiasa ambao sio walipa kodi hivyo ni afadhari kukwepa tuu kodi
Mkuu sawa ila,
Ukwepaji wa kodi na ufujaji wa pesa za uma ni kinyume cha sheria. Kwepa kodi au fisadi pesa ya uma ila Jamhuri ikikupata na iwapo huna kinga unapoteza. Uamuzi ni wako boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…