KERO TRA wananitumia meseji nikafanyiwe makadirio wakati hatukufikia makubaliano

KERO TRA wananitumia meseji nikafanyiwe makadirio wakati hatukufikia makubaliano

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
817
Reaction score
2,180
Iko hivi, nina biashara ambayo niliifungua kupitia familia, wakati huo nilikuwa bize na shule na umri haukuruhusu kupewa nyaraka na gavoo, pia familia hawakutaka nijihusishe na side hustle ila walisapoti wakawa wanasimamia show zangu.

Wanasema cha mtu mavi, ukitaka ubaya kabidhi ndugu mali, sikutaka ifike huko nilipomalizana na shule nikataka nibadili biashara irudi kwangu ki documents.

Mimi ni wale watu wasiopenda shida na karaha na taabu, so niliingia TRA portal nikachange TIN yangu kuwa BUSINESS TIN, nikaenda TRA wakaniletea longo longo na hesabu zao za kodi za kitapeli (makadilio ya kodi kwenye biashara yakawa makubwa kuliko kodi tuliyokuwa tunalipa tayari kama familia )

Niliwasilisha tu taarifa za mtaji na vitu muhimu lakini sikuwaambia kama nabadili umiliki wa biashara na wala sikuhusisha kuitaja ile biashara kuwa ipo chini ya familia, nilitaka wakinipa nyaraka then ile nyingine familia waandikie imefirisika.

Hatukufikia muafaka na kwa kuwa biashara ilikuwa inaenda good nikaon aniache kwanza kufatilia TRA na pia nilipata ajira nikawa bize siku za kwenda TRA ikawa issue.

AJABU YA TRA
Mwaka huu May wameanza kunitumia meseji niende kufanya makadilio ya kodi na nilipe kabla ya 31 may kuepuka adhabu, hii wametoa wapi kama hatukufikia muafaka wa mimi na wao kuhusu kodi na hata nilipojaribu kufosi nipate mashine ya EFD kwa jna langu la ofisi waligoma wakasema sijakamilisha taratibu zao.

Familia inalipa kodi kwa mujibu wa makadilio na mimi sihusiki nayo kabisa kwa sasa.
 
Candela my friend hujaeleza vizuri shida ni nini? Umeficha sana kwaiyo inakua ngumu kwasisi kukushauri nini ufanye au wapi uanzie.jaribu kuweka wazi ni aina gani ya biashara na imeanza lini na uko nyuma kuna return yeyote ushawai fanya au familia ishafanya.Hapo sasa tutajua tukushauri vp
 
TRA kwasasa ni noma ,washamzingua Niffer na yeye kashafunga ofisi yake kwanza.

Ila nawashauri vijana wanaopata fedha wakiwa bado wana utoto wanatakiwa walay low ,mambo ya kuanika mafanikio yako mitandaoni ni mabaya sana...Niffer showoff zimemponza.

Hao kina Chief Godlove na Yule Ney nani sijui kama mganga wale ni Project za Serikali zile ,wataendelea kufanya utumbo mitandaoni bila kubuguziwa ila ukiwaiga wewe lazima TEA-R-A ,TEETH waruke na wewe.
 
Kosa lako ni wao kubaki na namba yako .hizo sms ata uki acha ki memo chenye no zako pale TRA desk ..ndani ya week una tumiwa hizo sms
 
Aliyeelewa anieleweshe.
Nadaiwa kodi na natakiwa kwenda kufanya makadirio kwa mwaka mpya wa fedha na sina biashara nayoendesha kwa jina au taarifa zangu. Iliyopo ipo chini ya familia na kodi zote wanalipa kama familia japo mwanzilishi ni mimi.
 
Candela my friend hujaeleza vizuri shida ni nini? Umeficha sana kwaiyo inakua ngumu kwasisi kukushauri nini ufanye au wapi uanzie.jaribu kuweka wazi ni aina gani ya biashara na imeanza lini na uko nyuma kuna return yeyote ushawai fanya au familia ishafanya.Hapo sasa tutajua tukushauri vp
Kisheria sina biashara ila wananidai nikalipe kodi na nifanye makadilio kwa mwaka wa fedha uliopo. Biashara niliyoanzisha huko nyuma ilisajiliwa na familia na hiyo inaendelea kama kawaida na haina shida na kisheria sina link nayo tofauti na urithi kama likitokea la kutokea. Mwaka jana nilienda nifanye makadilio ya kodi nichukue sehemu ya ile biashara iwe chini yangu, kodi ikawa kubwa sana nikaona niache kwanza. Sasa sikurudi tena TRA ila tayari wao wanadai nilipe kodi ya biashara ambayo walinikazia.
 
Mimi ni wale watu wasiopenda shida na karaha na taabu, so niliingia TRA portal nikachange TIN yangu kuwa BUSINESS TIN, nikaenda TRA wakaniletea longo longo na hesabu zao za kodi za kitapeli (makadilio ya kodi kwenye biashara yakawa makubwa kuliko kodi tuliyokuwa tunalipa tayari kama familia )

Niliwasilisha tu taarifa za mtaji na vitu muhimu lakini sikuwaambia kama nabadili umiliki wa biashara na wala sikuhusisha kuitaja ile biashara kuwa ipo chini ya familia, nilitaka wakinipa nyaraka then ile nyingine familia waandikie imefirisika.
Kijana ulikurupuka sana. Kwenda kubadilisha TIN kuwa ya biashara tayari ni kosa la kiufundi. Pia kuwasilisha taarifa ya mtaji wako ina maana tayari TRA wanajua unafanya biashara. Bora uende ofisini kwao mkaongee muwekane sawa. Maofisa pia ni binadamu isitoshe una ushahidi wa familia kulipa kodi. Hapo hauna jinsi. Pia usiwachukulie TRA poa kuwaona mafala. Hao ni hatari kuliko unavyodhani.
 
Nadaiwa kodi na natakiwa kwenda kufanya makadirio kwa mwaka mpya wa fedha na sina biashara nayoendesha kwa jina au taarifa zangu. Iliyopo ipo chini ya familia na kodi zote wanalipa kama familia japo mwanzilishi ni mimi.
Naomba ukome kusema hiyo biashara ni yako! In short biashara hiyo ni ya familia!
 
TRA ,kwahapo wameinesha hawanatofauti Vodacom bima afya

Nilipigiwa cm nikaulizwa majina yangu ,mkewangu idadi yawatoto

Na nilimkatalia muhudumu ,usifanye chochote ,mwezi uliofatwa katwa 7000 ,nitageuka kuwa msauzi afrika wa nipige tafu
 
Kisheria sina biashara ila wananidai nikalipe kodi na nifanye makadilio kwa mwaka wa fedha uliopo. Biashara niliyoanzisha huko nyuma ilisajiliwa na familia na hiyo inaendelea kama kawaida na haina shida na kisheria sina link nayo tofauti na urithi kama likitokea la kutokea. Mwaka jana nilienda nifanye makadilio ya kodi nichukue sehemu ya ile biashara iwe chini yangu, kodi ikawa kubwa sana nikaona niache kwanza. Sasa sikurudi tena TRA ila tayari wao wanadai nilipe kodi ya biashara ambayo walinikazia.
Wewe ndiye umeyakanyaga! Yaani unaandika mpaka kwamba eti biashara ihamie kwenye jina lako halafu familia waandike kwamba wamefirisika? Nyie ndio huwa tunawatafuta! Jumatatu ukaripoti TRA haraka sana!
 
Back
Top Bottom